Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mnalaumu bure polisi kwanini wasiwahoji hao makamanda wa chama hao wazee wa kuzusha kila jambo? Ukifuatilia hata post zao hao majamaa ni uzushi, chuki na kejeli za kila aina kwa watu wasiofuata itikadi za chama chao.
Ifike mahala tuache kutetea mtu kisa yuko upande wa chama chako, kama kazingua acha sheria zimshughulikie, hili pia liwafikie wale wafuasi wa vyama vya kisiasa wasiojua kujenga hoja zaidi ya matusi na lugha chafu.
Sheria ifuate mkondo wake kwa yeyote anayeivunja
Hivi tumekwishasahau tuna Jeshi la Polisi la namna gani?
Kuna mstari mwembamba sana wa kuwatenganisha majambazi na polisi wa Tanzania.
Nani waliwaua wafanyabiashara wa madini, na kisha kupora pesa zao?
Nani walimwua yule mfanyabiashara ndugu yake PM kule Mtwara, na kisha kumpora pesa zao?
Tuna Jeshi la polisi lililojaa majambazi.