Jeshi la Polisi lapekua nyumba ya Boniface Jacob, laenda na GJ Malisa Moshi kupekua nyumba yake

Jeshi la Polisi lapekua nyumba ya Boniface Jacob, laenda na GJ Malisa Moshi kupekua nyumba yake

Wako watu walipendekeza Jeshi la Polisi Livunjwe na Kuundwa upya , lengo likiwa ni kuliboresha kwa kutimua hawa waliopo wenye akili za kizamani wakiwemo akina Muliro na wenzake na kuleta Askari wapya wenye akili ya kisasa .

Mwanzo nilipinga wazo hili lakini sasa naamini waliowaza vile waliona Mbali sana .

Anayetuhumiwa kupotosha mitandaoni amekuja ili mumuonyeshe upotoshaji wake halafu mnaenda kupekuwa nyumbani kwake ili mupate upotoshaji kwenye makabati au mnataka kukagua thamani ya nyumba yake ? Hivi ndivyo Police wa Nchi zote wanavyofanya au ni hawa wa CCP MOSHI pekee ?

View attachment 2973785
Huyu jamaa kumbe ni mnene hivi??,ndo mana kumbe uwa anaandikaga Ujinga mana watu wanene wataalam wanasema wanakuwaga na akili Finyu.
 
Safi sana Kamanda Murilo

Huyu Dogo Malisa sifa zimelevya sana
Jaribu kutumia akili kidogo kabla ya kusifia, tuhuma wanazotuhumiwa nazo Jeshi la la Polisi kuhusu suala hili ni nzito, kuua mtu. Hili siyo Jambo dogo hata kidogo, jaribu kufikiria huyo aliyeuawa angekuwa mtoto wako, baba yako, Kaka au mdogo wako, Je, ungejisikiaje? Ungemsifia Kamanda Muliro kws kutuhumiwa kumuua ndugu yako?
 
Mnalaumu bure polisi kwanini wasiwahoji hao makamanda wa chama hao wazee wa kuzusha kila jambo? Ukifuatilia hata post zao hao majamaa ni uzushi, chuki na kejeli za kila aina kwa watu wasiofuata itikadi za chama chao.

Ifike mahala tuache kutetea mtu kisa yuko upande wa chama chako, kama kazingua acha sheria zimshughulikie, hili pia liwafikie wale wafuasi wa vyama vya kisiasa wasiojua kujenga hoja zaidi ya matusi na lugha chafu.

Sheria ifuate mkondo wake kwa yeyote anayeivunja
 
Mmmh sasa upekuzi huko majumbani kwann? Au ndo kutaka kubambikiana case, maana mmmh
Fuatilia post zao hao jamaa kila muda wanapost mambo yanayozua taharuki, lengo la polisi ni kupata simu zao wapate ushahidi wa yale wanayoyasambaza katika jamii.

Hii mitandao sometime watu wanaitumia vibaya sana, serikali ikiwashughulikia wanaanza kujiliza
 
Huyu jamaa kumbe ni mnene hivi??,ndo mana kumbe uwa anaandikaga Ujinga mana watu wanene wataalam wanasema wanakuwaga na akili Finyu.
Huyo jamaa ni kama Wale wajapan wa SUMO ni mwepesi ni balaa , anapiga karate utadhani Jack Chan , Polisi hawa wa kibongo wanaokula Ugali dagaa bila Bunduki za kutosha hawampeleki popote
 
Wanamtafuta marehemu au wanapekua nini? CCM imewaharibu vichwa hawa polisi wetu.
 
Mnalaumu bure polisi kwanini wasiwahoji hao makamanda wa chama hao wazee wa kuzusha kila jambo? Ukifuatilia hata post zao hao majamaa ni uzushi, chuki na kejeli za kila aina kwa watu wasiofuata itikadi za chama chao.

Ifike mahala tuache kutetea mtu kisa yuko upande wa chama chako, kama kazingua acha sheria zimshughulikie, hili pia liwafikie wale wafuasi wa vyama vya kisiasa wasiojua kujenga hoja zaidi ya matusi na lugha chafu.

Sheria ifuate mkondo wake kwa yeyote anayeivunja
Kabla yakuandika ungesikiliza au kusoma kwanza maelezo ya jeshi la polisi kisha sasa kama una akili timamu uje uandike huu upuuzi ulioandika. Kiujumla maelezo ya jeshi la polisi ndio yana mkanganyiko na ndio maana watu wenye akili tunahoji inakuwaje?
 
Sema Nini... Jus say what...
Malisa aliwatafuta Sana Hawa jamaa... Yaanii ileerr...

Anyway. Tusubiri.
 
Mnalaumu bure polisi kwanini wasiwahoji hao makamanda wa chama hao wazee wa kuzusha kila jambo? Ukifuatilia hata post zao hao majamaa ni uzushi, chuki na kejeli za kila aina kwa watu wasiofuata itikadi za chama chao.

Ifike mahala tuache kutetea mtu kisa yuko upande wa chama chako, kama kazingua acha sheria zimshughulikie, hili pia liwafikie wale wafuasi wa vyama vya kisiasa wasiojua kujenga hoja zaidi ya matusi na lugha chafu.

Sheria ifuate mkondo wake kwa yeyote anayeivunja
Achana na Wanaa haoo...
 
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam bado linaendelea kuwashikilia Boniface Jacob na Godlisten Malisa. Wanatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi na kuzua taharuki katika jamii.

Polisi wameondoka na Godlisten Malisa kwenda naye Moshi, Kilimanjaro usiku huu ili kufanya upekuzi nyumbani kwao wakitafuta simu ambayo polisi wamesema wanaitaka kwa ajili ya uchunguzi.

Polisi wamekwenda nyumbani kwa Boniface Jacob, Mbezi-Msakuzi, Dar es Salaam pia kufanya upekuzi ikiwa ni pamoja na kutafuta simu ambayo polisi wamesema wanahitaji ili kufanya uchunguzi.

Jeshi la polisi limesema kwamba wao ndiyo walalamikaji katika jambo hili, na kwamba Boniface Jacob na Godlisten Malisa wamefanya uchochezi na kuzua taharuki katika jamii dhidi ya Jeshi la Polisi.

Pia, jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Saalam limesema kwamba, kuna makachero wa jeshi la Polisi kutoka mkoa wa Arusha ambao wanatoka Arusha kuja Dar es Saalam ili kumuhoji Boniface Jacob.

Tuteendelea kuwajulisha kwa ambayo yanaendelea. MSIOGOPE. MSIOGOPE. MSIOGOPE. MSIOGOPE.

MMM, Mtikila.

PIA SOMA
- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

- Boniface Jackob afika kituo cha Polisi cha Oysterbay ili akamatwe kama alivyoagiza RPC
Kama upo karibu na jeshi la polisi wakumbushe habari za Dokta Ulimboka,Ben Saanane,Roma na Tundu Lisu!!!
 
Wako watu walipendekeza Jeshi la Polisi Livunjwe na Kuundwa upya , lengo likiwa ni kuliboresha kwa kutimua hawa waliopo wenye akili za kizamani wakiwemo akina Muliro na wenzake na kuleta Askari wapya wenye akili ya kisasa .

Mwanzo nilipinga wazo hili lakini sasa naamini waliowaza vile waliona Mbali sana .

Anayetuhumiwa kupotosha mitandaoni amekuja ili mumuonyeshe upotoshaji wake halafu mnaenda kupekuwa nyumbani kwake ili mupate upotoshaji kwenye makabati au mnataka kukagua thamani ya nyumba yake ? Hivi ndivyo Police wa Nchi zote wanavyofanya au ni hawa wa CCP MOSHI pekee ?

View attachment 2973785
Polisi wangewapa tu onyo na maisha yaendelee.
 
Bonifasi Jacob ni hazina kwa taifa kwa macho ya nyama.

Bonifasi Jacob ni mwanaCCM damu kwa macho ya rohoni,mimi sijalewa nipo timamu CCM ni chama ambacho kina mbinu nyingi za kucheza na wapinzani wa nchi hii
Macho ya rohoni ndo yapi ? Acha ngojera sema hayo ni mawazo yako tu macho rohoni ni blah blah tu.
 
Safi sana Kamanda Murilo

Huyu Dogo Malisa sifa zimelevya sana
Hata aibu huna?
Comment zote zinaliponda jeshi la polisi. Au wewe ndio Muliro? Malisa for your information is a force to recon with.
Nitafurahi Sana hii kesi wakiipeleka mahakamani ili kwa Mara ya pili polisi wa michongo waonyeshe ukilaza wao hadharani.
Mnakumbuka walisemaha Mbowe alitaka kupindua nchi kwa kukata miti na kuitupa barabarani.
Polisi hakikisheni Malisa anafika Moshi salama.
 
"ulikuwa unaokoa wenzako....sasa jiokoe na wewe......"
This is absolutely hogwash. Kweli common sense is a rarity. Halafu baadae wapumbavu kama nyinyi mkipotea ndugu zenu wanaanza kulia lia mitandaoni na kutuma picha zenu kwenye WhatsApp groups. Unaongea ujinga sababu wewe sio muathirika wa matukio hayo..
 
NCHI HII KUBWA: Bora Taharuki kuliko Mauaji.

ANAANDIKA BABA ASKOFU BENSON BAGONZA

Sifa moja muhimu ya kiongozi ni kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa jamii.

Nyumba inapoungua moto, ni bora kuokoa hata godoro moja kuliko kuua panya wanaokimbia moto unaounguza nyumba.

Mitandao ya kijamii usiku wa leo (25/4/2024) imejaa habari za Mwanaharakati wa haki za kijamii Malisa GJ na Mwanasiasa/Mwanaharakati Jacob Boniface kukamatwa na polisi kwa KUSABABISHA TAHARUKI wakati wanaripoti “mauaji” ya mtu mmoja aitwaye Mushi.

Kama ningelikuwa jeshi la polisi ningetafakari haya kabla ya kufanya maamuzi:

1. Nchi hii ni kubwa sana. Jeshi la polisi ni dogo kuliko uhalifu. Wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu ningewafanya marafiki kuliko maadui.

2. Ni kweli Mushi amekufa. Ningeshughulika na wauaji kuliko kushughulika na waliosababisha taharuki.

3. Ningejiuliza; taharuki imesababishwa na ripoti ya kifo au kifo chenyewe? Kifo kisicholeta taharuki si kifo kamili.

4. Malisa GJ ameisharipoti matukio mengi ya kihalifu ambayo jeshi la polisi ama halikujua au lingepata taabu sana kujua. Kwa hili la kifo cha Robert Mushi, Jeshi la polisi lingemzawadia nishani ya utumishi wa kujipendekeza kwa polisi kuliko kumkamata na kumpekua.

5. Badala ya kumpekua Malisa GJ na Boniface Jacob, ningewatumia na mitandao yao kutafuta na kujua gari linalodaiwa kumgonga marehemu Moshi.

6. Kwa kuwa nchi ni kubwa sana; ningetumia muda kuchunguza ndani na nje ya jeshi la polisi kuhusu uwezekano wa polisi vishoka wanaodaiwa kumkamata marehemu Robert Mushi kabla ya kifo chake!

7. Ningeazimia kuwalinda wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu kuliko wanaodaiwa kukosea katika kutoa taarifa za uhalifu ili kwa njia hiyo niongeze wigo wa watoa taarifa za uhalifu.

Lakini kwa kuwa mimi si Jeshi la polisi bali ni mtu ninayejifanya Askofu wakati hata uaskofu umenishinda, nabakia kutamani kuwa polisi huku nikijua kuna polisi wanatamani kuwa Askofu.

Natamani Jeshi la polisi liwaachie huru Malisa GJ na Boniface Jacob ili linufaike na harakati zao katika kukomesha uhalifu wa kidola na kiraia.
 
mimi kuliunga mkono jeshi la polisi umeumia?

mwanaume fanya mambo yako

Wenye akili hawaungi mkono mtu au taasisi bali matendo ya mtu au taasisi.

Sasa wewe sema kama unaunga mkono uharamia wa polisi wa kuua raia. Wewe kuunga mkono uovu, wala haitakuwa ajabu maana hata shetani ana wafuasi wengi. Yawezekana wewe ni miongoni mwa waovu, kwa nini usiunge mkono uovu? Muuaji siku zote huwaunga mkono wauaji wenzake na hujifunza hata mbinu za kuua kutoka kwa wauaji wenzake. Kwake wauaji ni mashujaa.
 
Back
Top Bottom