Jeshi la Polisi lapewa siku 90 kuhakikisha mitambo ya LUGUMI inafanya kazi vituo vyote

Kumbe jpm hapambani na ufisadi bali mahasim wake ccm ni ile ile
 
Ñchi hii hata wezi wa fedha nyingi hadi billioni 37 wanapewa muda wa kuficha wizi wao kwa kuruhusiwa kupandikiza kompyuta mbovu hivi hivi kadamnasi. Nani alichota pesa ya Lugumi? Iweje mtu aliyefunga kompyuta 14 tu katika miaka mi 3 aweze kufunga mifumo madhubuti ya kompyuta 98 ndani ya siku 90? Aliyehamisha hela kupitia mradi wa Lugumi atajwe.
 

Usihofu ndugu yangu CAG namuaminia taenda tena huko na akikuta bado ataripoti kama kawaida yake.
 
Eeh Mungu wangu. Nimegundua kwa nini vikundi vya kigaidi hujitokeza, nimegundua ni kwanini yule kijana wa Kiarabu alijichoma Moto mbele ya ofisi za Serikali, nimegundua ni kwa nini mtiifu wa ccm anaweza kujiunga Chadema, nimegundua kwa nini anataka aombewe. Jamani issue ya Lugumi ndo imeisha hivi hivi bila mtu kutiwa hatiani!!!?? Kweli? Nchi inaenda wapi? Mbona sioni tofauti ya JK na JPM? Mungu bora uiangamize Taifa hili tujue moja. Izame kama gharika.
 
Usishangilie upuuzi wewe .... hio ni pesa yetu sote. hivi watu wengine sijui akili zenu mnaweka wapi aiseee, shame on you, mnaleta siasa hata kwenye mambo ya muhimu....
Watu wa aina hii hata akisikia mamaa ya watoto anaselebuka na kiongozi wa chama chake atajisikia fahari kuwa ndio ukada wenyewe huo. Huwezi kumbadili huyo, ni brain washed
 
kweli tanzania hakuna kiongozi wa kweli wa kutukomboa wote ni wasanii tuu, hivi huyu lugumi anatofauti gani na mkurugenzi aliyefukuzwa TRA, engineer wa mkoa aliyefukuzwa na makonda, mkurugenzi wa TCRA n.k. Iweje yeye wampe muda wa kusawazisha makosa yake wakati hata mtoto mdogo anatambua kama wamepiga pesa
 
Kuna mambo mengine kuchangia ni kuongeza hasira tu kitu ambacho ni kibaya sana kiafya.
 

Usikute Pombe na Kitwanga wote wana hisa ndani ya Lugumi. At last ile true colour ya hapa kazi tu inajipambanua tartiiibu.
 
Hii ndo maana halisi ya "huu mchezo hautaki hasira na Sio kila jipu ni la kutumbua"

Hahahaahaahahahahahahaha Only in Tanzania,hongera sana Lugumi kwa kutimiza makubaliano yako kwenye mkataba. Safari bado ni ndefu tutafika tuu chini ya Sirikali yetu tukufu.
 
Lugumi ni nani nchi hii?hata mzee wa mbwembwe kachemka?
 
hilo ndilo bunge letu.....sema ndiooooooo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…