Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya #77Nyeupe kudai Tume Huru ya Uchaguzi

Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya #77Nyeupe kudai Tume Huru ya Uchaguzi

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
ONYO KUHUSU MAANDAMANO YANAYOHAMASISHWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

7.jpg

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa onyo kali kwa wananchi waliopanga kufanya maandamano leo yakihamasisha uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini.

RPC Mambosasa amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa wananchi hao watafanya maandamano leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mambosasa amesema Tume Huru ya Uchaguzi haipo mkoani Dar es Salaam na kwa hiyo watu hao hawatakiwi kulipima Jeshi la Polisi.

“Nitoe onyo Tume Huru inayodaiwa haipo Dar es Salaam, lakini Tume ya Uchaguzi pia haipo Dar es Salaam Makao Makuu yake yapo Dodoma, kitendo cha watu kuja kufanya maandamano Dar es Salaam ni uchokozi wa kupimana,” amesema.

Amesema kupimana huko si kwa namna nzuri kwani matokeo yake hayatakuwa mazuri kwa atakayejaribu kufanya maandamao hayo. “Niwaonye wote wanaohamasishana waishie huko huko kwenye mitandao ya kijamii, wasijaribu kutoka kwenye mitandao wakaenda kwenye ardhi hii ambayo tumekabidhiwa kuhakikisha watu wetu wanaendelea kuwa salama hawataenda zaidi ya hatua tano,” amesema.

Ameongeza kuwa matokeo ya kukaidi kutokufanya maandamano ni kilio, kwani ni kinyume na sheria. Amesema hajapata maombi yoyote kuhusiana na kuwepo kwa maandamano hayo katika mikoa yote mitatu ya Kipolisi ya Ilala, Kinondoni na Temeke.

Amesema Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati hivyo ni muhimu kila mwananchi akachangamkia fursa ya kutafuta kipato kilicho halali, kwani atakayejaribu kuwapima uwezo wao kwa kuleta fujo mkoani mwake, wamejipanga kuwathibiti.

“Tumejipanga si tu katika maandamano hayo, lakini tumejipanga kuhakikisha kipindi chote cha mchakato kuelekea uchaguzi mkuu, mchakato wa upigaji kura, uhesabuji kura na lile shangilio la aliyeshinda kwa usawa,”amesema.

“Niwaombe Watanzania waendelee kuheshimu sheria za nchi bila kushurutishwa, anayetaka kushurutishwa tupo tutamuwezesha kutii sheria, lakini anayetii sheria kwa hiari ataendelea kuwa salama na kuheshimika,” amesema.

LAZARO B. MAMBOSASA- SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

06/07/2020
 
Sasa maandamano ya nini kipindi hiki cha #covid19.Na ukivunjika mguu gharama ni juu yako!
Bora mpigwe marufuku tu!
 
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi jijini Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa onyo kwa wanaojiandaa kufanya maandamano siku ya tarehe saba kwa lengo la Kudai Tume huru ya Uchaguzi.

EastAfricaRadio

Mzukulu nilidhani kuwa hawa wanaopanga Kuandamana ndiyo Wazalendo na Watanzania wakweli wenye Uchungu na Taifa lao hivyo wangepewa Ulinzi na ikibidi hata wasindikizwe mpaka Ofisi husika za Tume matokeo yake wanaonekana ni Wakorofi na Wahuni tu!
 
My Government is very worse , so Police order is against over our constitution. On 07 /07 #Nyeupe must be take place
Tume inaundwa kwa sheria, watunga sheria wameshavunja bunge sasa hiyo tume huru unaidai wapi na ipatikane lini. Mmeacha miaka yoye minne ipite bila kuwa na mchakato wa tume huru halafu mnajitia wajuaji kudai tume huru sasa hivi.

Practically hicho kitu hakiwezekani kutokea kabla ya uchaguzi ujao wa Oktoba 2020. Kama ni ushauri basi jipangeni kupata hiyo mnayoita tume huru kwa ajili ya uchaguzi wa 2025.
 
Please I don't understand Swahili can you write ur rubbish by using My mother tongue English language.
Unajuaje kama alichokiandika ni rubbish kama hujui Kiswahili? Halafu lugha ya taifa ni Kiswahili na siyo hiyo lugha ya mabeberu wenu. Kama unataka mother tongue language basi akuandikie kihaya cha kwenu Katerero.
 
Wewe ndio huijui ila mnaogopa kupingwa njia mojawapo ni maandamano
Basi nendeni mkaandamane halafu mtakachokutana nacho basi si vibaya mkaenda kuishtaki serikali kwa kuvunja katiba.
 
Tume inaundwa kwa sheria, watunga sheria wameshavunja bunge sasa hiyo tume huru unaidai wapi na ipatikane lini. Mmeacha miaka yoye minne ipite bila kuwa na mchakato wa tume huru halafu mnajitia wajuaji kudai tume huru sasa hivi. Practically hicho kitu hakiwezekani kutokea kabla ya uchaguzi ujao wa Oktoba 2020. Kama ni ushauri basi jipangeni kupata hiyo mnayoita tume huru kwa ajili ya uchaguzi wa 2025.



Nyeupe will occur tomorrow so relux without Independent committee no General Election.
 
Back
Top Bottom