Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya #77Nyeupe kudai Tume Huru ya Uchaguzi

ONYO KUHUSU MAANDAMANO YANAYOHAMASISHWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

View attachment 1498960

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote atakayeshiriki maandamano hayo batili tarehe 07/07/2020 kwa madai ya kudai Tume huru ya uchaguzi waaache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

LAZARO B. MAMBOSASA- SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

06/07/2020
Kwani polisi wakiwalinda waandamanaji na wao wataonekana wanaandamana? Si wawalinde tu ili sauti zao zisikike, au hawataki sauti zao zisikike. Nyerere aliposhinda kesi wananchi waliandamana na polisi hawakushughulika nao.
 
Ukweli ni kwamba mwaka huu upinzani umejua unaenda kushindwa. Maana hamna hoja yoyote ya msingi itayowabeba.
Hoja zipo nyingi tu mkuu ndio maana kila chama ina kitabu cha sera zake mfano CHADEMA wanayo ya ugatuzi maeneo kma kusini waliotengwa wakieleweshwa lazima waunge mkono.

Napoongea hapa kila mwaka vijana laki 9 wanaingia kwenye soko la ajira sasa hao wote hawana sababu ya kuichagua CCM. Wakieleweshwa kuwa taifa limejikita kujenga miundombinu na imesahau enteprise development ya mtu mmoja mmoja kma upatikanaji wa mitaji, interns kwa vijana n.k lazima wote waikatae CCM.

Mtiririko huo unaendelea kwa wakulima ukianzia wa korosho mpaka pamba wakieleweshwa kuwa serikali imeshindwa kumuokoa mkulima kuanzia kumsogezea kilimo cha kisasa mpka kumtafutia masoko nje ama kutoa export subisidies ili kuua ushindani lazima ainyime kura CCM.

waTZ wa sasa wanajitambua wanaelewa majukumu ya upinzani Vs Bunge Vs Serikali. Kituko mnataka mshindane eti nmejenga reli kwa mtu ambaye hakusanyi kodi. Ni kwamba kila mtu atajinadi kulingana na job description yake. Mbunge ataeleza alivyosimamia serikali, upinzani utaeleza sera mbadala na ilivyoishauri na kukosoa serikali, na serikali itajieleza ilivyotekeleza ahadi zake.

Wananchi wataamua
 
Sijatoa kauli za kibinafsi nimetoa tahadhari tu.
Kwahiyo Maxence Melo angemfichua FUHRER kisa tu tahadhari kwamba ataenda jela mwenyewe na familia yake itateseka yenyewe huku JF users tukiendelea kudunda kma kawa??

Hii tabia muache..... Hta utaskia ooh Mbowe akiandamana amtangulize mkewe na watoto. Sasa unajiuliza Mbowe anaandamana kwa ajili ya familia yake au maslahi ya chama na taifa kwa ujumla. Alipoingia jela mbona aliingia mwenyewe sisi wengine tupo uraiani kma kawa?

Tubadilike
 
Sidhani kama umenielewa kaka.
 
Hoja zipo nyingi tu mkuu ndio maana kila chama ina kitabu cha sera zake mfano CHADEMA wanayo ya ugatuzi maeneo kma kusini waliotengwa wakieleweshwa lazima waunge mkono.

Napoongea hapa kila mwaka vijana laki 9 wanaingia kwenye soko la ajira sasa hao wote hawana sababu ya kuichagua CCM. Wakieleweshwa kuwa taifa limejikita kujenga miundombinu na imesahau enteprise development ya mtu mmoja mmoja kma upatikanaji wa mitaji, interns kwa vijana n.k lazima wote waikatae CCM.

Mtiririko huo unaendelea kwa wakulima ukianzia wa korosho mpaka pamba wakieleweshwa kuwa serikali imeshindwa kumuokoa mkulima kuanzia kumsogezea kilimo cha kisasa mpka kumtafutia masoko nje ama kutoa export subisidies ili kuua ushindani lazima ainyime kura CCM.

waTZ wa sasa wanajitambua wanaelewa majukumu ya upinzani Vs Bunge Vs Serikali. Kituko mnataka mshindane eti nmejenga reli kwa mtu ambaye hakusanyi kodi. Ni kwamba kila mtu atajinadi kulingana na job description yake. Mbunge ataeleza alivyosimamia serikali, upinzani utaeleza sera mbadala na ilivyoishauri na kukosoa serikali, na serikali itajieleza ilivyotekeleza ahadi zake.

Wananchi wataamua
Serikali itajieleza ilivyotekeleza ahadi na sera zake. Na kwa namna ilivyotekeleza sidhani kama wapinzani mtaeleweka kwa waanchi.
Kuhusu ajira nadhani hakuna serikali duniani inayoajiri raia wake wote na sidhani kuwa eti serikali imejikita kujenga miundo mbinu na imesahau kuajiri vijana. Miradi kama Sgr na JNHPP inazalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja nyingi tu. Na hii ni baadhi ya mifano tu.
Na kusema eti serikali haijatilia mkazo kilimo sio kweli ndio maana kuna programu endelevu za kuhakikisha kilimo kinakuwa na wakulima wanafaidika. Na ndio maana zaidi ya bil 253 zilitumika kuhakikisha kilimo kinakua. Na hata huko kusini unaposema pamesahaulika ni ni wakubwa wa Asdp 1 & 2.
 
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi jijini Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa onyo kwa wanaojiandaa kufanya maandamano siku ya tarehe saba kwa lengo la Kudai Tume huru ya Uchaguzi.

EastAfricaRadio

Mzukulu nilidhani kuwa hawa wanaopanga Kuandamana ndiyo Wazalendo na Watanzania wakweli wenye Uchungu na Taifa lao hivyo wangepewa Ulinzi na ikibidi hata wasindikizwe mpaka Ofisi husika za Tume matokeo yake wanaonekana ni Wakorofi na Wahuni tu!
Ubunge unagombea wapi nikuletee kura yangu
 
Tume huru ya uchaguzi imeanza kudaiwa toka mfumo wa vyama vingi urejee hapa nchini. Sasa hivi inadaiwa kwa nguvu zaidi, baada ya Magufuli kuiingilia waziwazi. Huko siku za nyuma wangalau ilikuwa na soni. Ni hivi, tunahitaji tume huru ya uchaguzi maana hii sio huru fullstop.
Huko kujiingiza wazi wazi kwenye uchaguzi kupo vipi? Maana sikuelewi unataka kusema JPM huwa anawashika mikono wananchi waichague Ccm?
 
Serikali itajieleza ilivyotekeleza ahadi na sera zake. Na kwa namna ilivyotekeleza sidhani kama wapinzani mtaeleweka kwa waanchi.
Kuhusu ajira nadhani hakuna serikali duniani inayoajiri raia wake wote na sidhani kuwa eti serikali imejikita kujenga miundo mbinu na imesahau kuajiri vijana. Miradi kama Sgr na JNHPP inazalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja nyingi tu. Na hii ni baadhi ya mifano tu.
Na kusema eti serikali haijatilia mkazo kilimo sio kweli ndio maana kuna programu endelevu za kuhakikisha kilimo kinakuwa na wakulima wanafaidika. Na ndio maana zaidi ya bil 253 zilitumika kuhakikisha kilimo kinakua. Na hata huko kusini unaposema pamesahaulika ni ni wakubwa wa Asdp 1 & 2.
1. Kma mlijua hamtoi ajira kwanini mliahidi kwenye ilani yenu page ya 4 kuwa mtatengeneza ajira mamilion? Vijana wakieleweshwa kuwa waliingizwa mkenge sioni wapi mkipenya.

2. Kuhusu kilimo ilani yenu page 14 mliahidi hektw zaidi ya 1 million kuwa za umwagiliaji na kwamba wakulima wataacha rasmi kutegemea mvua alafu hapa unasema eti programu endelevu. Ilihi 93% ya wakulima wanategemea mvua bado!! Mtadanganyaje wakulima wawape kura?

3. JNHPP 80% inaenda nje sababu material na technology/ experts wanatolewa huko so ajira ni vibarua tu. Spillover effect ni chini ya 20% kwahiyo sio kweli itasolve tatizo la ajira ambapo vijana laki 9 wanaingia soko la ajira.

Ajira + Kilimo ndio kifo chenu. Hapo kumbuka vijana ndio wengi nchi hii na Wakulima ndio labor force kubwa. Sioni mkitoboa kma watu wakichagua kwa hoja sio ushabiki.
 
ONYO KUHUSU MAANDAMANO YANAYOHAMASISHWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

View attachment 1498960

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote atakayeshiriki maandamano hayo batili tarehe 07/07/2020 kwa madai ya kudai Tume huru ya uchaguzi waaache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

LAZARO B. MAMBOSASA- SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

06/07/2020
Kamanda hajaelewa.. Watu hawataingia barabarani wataingia fikirani na rohoni na kuandamana huko.. Ni maandamano ya kiroho kuliko ya kimwili
 
Yaani CCM ukiwaambia habari ya kudai tume huru ya uchaguzi au katiba mpya ni kama unamwambia mtu kuwa....."Sasa unatakiwa Ufe kesho, Tukuzike keshokutwa!" Lakini siku jeshi letu litakapokuja kutambua kuwa wajibu wake sio kupambana na waandamanaji, bali ni kuwalinda na kuhakikisha wanayafikisha madai yao kunakohusika ndipo hapa tutakuwa tumepata ukombozi kamili!
 
Nimeandaa nyeupe kuanzia kiatu, suruali mpaka shati. Na wife naye atapiga dera jeupe hiyo kesho. Bila tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi chini ya hiyo tume ya kihuni.
Utavaa nyuma ya keyboard bodi [emoji23][emoji1787][emoji2960]
 
Back
Top Bottom