Hoja zipo nyingi tu mkuu ndio maana kila chama ina kitabu cha sera zake mfano CHADEMA wanayo ya ugatuzi maeneo kma kusini waliotengwa wakieleweshwa lazima waunge mkono.
Napoongea hapa kila mwaka vijana laki 9 wanaingia kwenye soko la ajira sasa hao wote hawana sababu ya kuichagua CCM. Wakieleweshwa kuwa taifa limejikita kujenga miundombinu na imesahau enteprise development ya mtu mmoja mmoja kma upatikanaji wa mitaji, interns kwa vijana n.k lazima wote waikatae CCM.
Mtiririko huo unaendelea kwa wakulima ukianzia wa korosho mpaka pamba wakieleweshwa kuwa serikali imeshindwa kumuokoa mkulima kuanzia kumsogezea kilimo cha kisasa mpka kumtafutia masoko nje ama kutoa export subisidies ili kuua ushindani lazima ainyime kura CCM.
waTZ wa sasa wanajitambua wanaelewa majukumu ya upinzani Vs Bunge Vs Serikali. Kituko mnataka mshindane eti nmejenga reli kwa mtu ambaye hakusanyi kodi. Ni kwamba kila mtu atajinadi kulingana na job description yake. Mbunge ataeleza alivyosimamia serikali, upinzani utaeleza sera mbadala na ilivyoishauri na kukosoa serikali, na serikali itajieleza ilivyotekeleza ahadi zake.
Wananchi wataamua