Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya #77Nyeupe kudai Tume Huru ya Uchaguzi

Jeshi la Polisi lapiga marufuku maandamano ya #77Nyeupe kudai Tume Huru ya Uchaguzi

Tume inaundwa kwa sheria, watunga sheria wameshavunja bunge sasa hiyo tume huru unaidai wapi na ipatikane lini. Mmeacha miaka yoye minne ipite bila kuwa na mchakato wa tume huru halafu mnajitia wajuaji kudai tume huru sasa hivi. Practically hicho kitu hakiwezekani kutokea kabla ya uchaguzi ujao wa Oktoba 2020. Kama ni ushauri basi jipangeni kupata hiyo mnayoita tume huru kwa ajili ya uchaguzi wa 2025.

Unachekesha ile mbaya, watunga sheria haiwataki tume huru vya uchaguzi maana haiwabebi, hivyo walikuwa wanapiga chenga makusudi. Inabidi ufahamu kuwa madai halali hayana muda. Isitoshe kulikuwa na katiba pendekezwa iliyokuwa inasubiri kupigiwa kura, lakini rais huyu aliigomea ili aendeshe nchi kwa katiba yenye mapungufu. Na humo ndani ya katiba pendekezwa kuna jinsi ya kuunda tume huru ya uchaguzi. Hivyo wakujilaumu ni wale waliogoma kutekeleza wajibu wao. Madai ya tume huru yake palepale, kisingizio cha muda hakina nafasi.
 
Namhakikishia kamanda Lazaru tarehe 7/7 navaa suti yangu nyeupu bila shuruti. Watch this space nitarusha picha live live.
 
Owomkyalo bwana, you claim English is your native language but I can see your English in great trouble. But great to support independent electoral committee, we are together.
My Government is very worse , so Police order is against over our constitution. On 07 /07 #Nyeupe must be take place
Mkuu Wewe naye ni mzigo pamoja na chadema yako,must be take place ulimaanisha nini?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Please I don't understand Swahili can you write ur rubbish by using My mother tongue English language.
 
Ea9ssyNWAAAOacJ.jpeg
 
Owomkyalo bwana, you claim English is your native language but I can see your English in great trouble. But great to support independent electoral committee, we are together.

I agree with you , Independent electrol committee, is inevitable.
 
ONYO KUHUSU MAANDAMANO YANAYOHAMASISHWA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote atakayeshiriki maandamano hayo batili tarehe 07/07/2020 kwa madai ya kudai Tume huru ya uchaguzi waaache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

LAZARO B. MAMBOSASA- SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

06/07/2020
1594027876982.png

Lazaro Mambosasa​
 
#HABARI Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi jijini Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa onyo kwa wanaojiandaa kufanya maandamano siku ya tarehe saba kwa lengo la Kudai Tume huru ya Uchaguzi.
Tutaandamana mtake msitake

Hata magetini mwetu tutaandamana...nguo nyeupe tutavaa...

Ni ujinga kufikiri unaweza zima kitu inaitwa civil disobedience!

You will not!

Good luck with that nonsense!
 
Muhimu Mamlaka itoe muongozo juu ya kuvaa kanzu siku ya 7/7 . Je waumini tunaruhusiwa kuvaa kanzu 7/7?
 
My Government is very worse , so Police order is against over our constitution. On 07 /07 #Nyeupe must be take place
Si ungeandika Kiswahili tu? Au hata Kiswahili pia ni cha hivyo hivyo? Nilipoona lugha iliyotumika, sikuwa hata na tamaa ya kuchambua hoja iliyokuwa ikijengwa.
 
Nimeandaa nyeupe kuanzia kiatu, suruali mpaka shati. Na wife naye atapiga dera jeupe hiyo kesho. Bila tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi chini ya hiyo tume ya kihuni.
Tume ipo huru watanzania na dunia nzima wanajua. Huko kupiga white ni ujifurahisha na kupoteza muda.
 
Askofu alietoa wazo hili la kuandamana kwa kuvaa nguo nyeupe awepo mstari wa mbele siku hiyo.
asihimize kisha yeye akabaki.
 
U
Unachekesha ile mbaya, watunga sheria haiwataki tume huru vya uchaguzi maana haiwabebi, hivyo walikuwa wanapiga chenga makusudi. Inabidi ufahamu kuwa madai halali hayana muda. Isitoshe kulikuwa na katiba pendekezwa iliyokuwa inasubiri kupigiwa kura, lakini rais huyu aliigomea ili aendeshe nchi kwa katiba yenye mapungufu. Na humo ndani ya katiba pendekezwa kuna jinsi ya kuunda tume huru ya uchaguzi. Hivyo wakujilaumu ni wale waliogoma kutekeleza wajibu wao. Madai ya tume huru yake palepale, kisingizio cha muda hakina nafasi.
Ukweli ni kwamba mwaka huu upinzani umejua unaenda kushindwa. Maana hamna hoja yoyote ya msingi itayowabeba. Hili la tume huru ni kisingizio tu. Mwaka 2015 mbona hakumleta hiki kisingizio?
 
Sasa maandamano ya nini kipindi hiki cha #covid19.Na ukivunjika mguu gharama ni juu yako!
Bora mpigwe marufuku tu!
Unaweza usiunge mkono maandamano ila sio kwa akili za ubinafsi hivi. Unapoumizwa kudai mabadiliko fulani ni kwa ajili ya faida ya wengine so hta ukiumia basi ukiimgia gharama it was for greater course.

Kma kila mtu akijiangalia ananufaikaje basi sidhani hta Nyerere angerisk maisha yake kuharakisha uhuru. Tuache hizi kauli za ubinafsi.
 
U

Ukweli ni kwamba mwaka huu upinzani umejua unaenda kushindwa. Maana hamna hoja yoyote ya msingi itayowabeba. Hili la tume huru ni kisingizio tu. Mwaka 2015 mbona hakumleta hiki kisingizio?

Tume huru ya uchaguzi imeanza kudaiwa toka mfumo wa vyama vingi urejee hapa nchini. Sasa hivi inadaiwa kwa nguvu zaidi, baada ya Magufuli kuiingilia waziwazi. Huko siku za nyuma wangalau ilikuwa na soni. Ni hivi, tunahitaji tume huru ya uchaguzi maana hii sio huru fullstop.
 
Unaweza usiunge mkono maandamano ila sio kwa akili za ubinafsi hivi. Unapoumizwa kudai mabadiliko fulani ni kwa ajili ya faida ya wengine so hta ukiumia basi ukiimgia gharama it was for greater course.

Kma kila mtu akijiangalia ananufaikaje basi sidhani hta Nyerere angerisk maisha yake kuharakisha uhuru. Tuache hizi kauli za ubinafsi.
Sijatoa kauli za kibinafsi nimetoa tahadhari tu.
 
Back
Top Bottom