Jeshi la Polisi latangaza uchunguzi wa video ya Askari kulala chini, madai ya rushwa na mateso

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
IMG_6304.jpeg

Video inayoonyesha askari polisi akiwa amelala chini imezua taharuki mitandaoni, huku ikidaiwa imerekodiwa katika kituo cha polisi bandari. Katika ujumbe ulioambatana na video hiyo, askari wanaodai kuwa wa kituo hicho walieleza kuwa wanakabiliwa na unyanyasaji mkubwa kutoka kwa viongozi wao, wakimtaja OCS kama chanzo cha rushwa na mateso.

Wamedai kuwa baadhi ya askari wamekuwa wakifungwa mahabusu bila kosa kwa sababu tu hawajatoa rushwa, hali inayosababisha msongo wa mawazo, kukata tamaa na hata kufikiria kuacha kazi au kujiua.

Jeshi la Polisi, kupitia taarifa yake rasmi ya tarehe 24 Septemba 2025, limesema limeona video hiyo na kuanzisha uchunguzi wa kubaini ukweli wake, wapi imetengenezwa, na ni akina nani waliohusika kuiandaa. Polisi wamesisitiza kuwa baada ya uchunguzi kukamilika, hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Kwa sasa, Jeshi la Polisi limewataka wananchi kusubiri matokeo ya uchunguzi huo na kuahidi kuchukua hatua stahiki mara moja.

View attachment 3478409

View attachment 3478408
Matokeo ya uchunguzi kibao, mdude vipi?
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Msongo wa mawazo tu, hakuna kosa hapo, walipwe tu stahiki zao
 
Baba wa familia anatuhumiwa na familia yake dhidi ya maovu kwa familia,ili baba akipatikana na makosa aadhibiwe vikali
Je baba atakubali kupatikana na kosa hata kama ni kweli?😷😷
 
Hata wakitaka wachinjane ni juu yao hakuna anaejali
 
Back
Top Bottom