Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Jeshi la polisi limethibitisha kuwakamata na kuwashkilia vijana waliofanya ukatili Kwa kubaka na kumsodimise Binti anaesadikika kutokea yombo
Jeshi Hilo pia limethibitisha kumshikilia Binti huyo Kwa mustakabali mwema wa maisha yake na kuonya watu wanapenda kumtafuta yeye ama ndugu zake ili wamhoji

=====

Jeshi la Polisi nchini limewakata watu wanne kati ya sita wanaotuhumiwa kumbaka na kumlawiti binti mkazi wa Yombo Dovya Dar es Salaam ambaye video yake ilisambaa mitandaoni hivi karibuni akifanyiwa ukatili huo na wanaume watano.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime, imeeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mkoani Dodoma na Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu la Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nikson Idala Jakson.

"Uchunguzi uliofanyika hadi sasa umefanikisha kumpata binti aliyefanyiwa ukatili huo na amehifadhiwa eneo salama na anaendelea kupata huduma zinazostahili kupewa mtu aliyefanyiwa ukatili wa aina hiyo, aidha uchunguzi umebaini tukio hilo lilifanyikia eneo la Swaswa katika Jiji la Dodoma mwezi Mei 2024," imeeleza taarifa hiyo.

Aidha DCP Misime amesema kuwa, "Jeshi la Polisi lingependa kueleza pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne huko Dar es Salaam waliokiuka sheria na kusambaza picha mjongeo wa tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii ambao ni Frora Mlombola, Aghatha Mchome, Madatha Jeremiah Budodi na James Nyanda Paulo,".
IMG_20240809_170358.jpg
IMG_20240809_170315.jpg
 
MTUHUMIA NAMBA MOJA NI AFANDE WA KIKE ALIYEWATUMA, HUYO HAWEZI KUKIMBIA MKAMATENI NA YEYE ACHENI DOUBLE STANDARDs.
Kuna utaratibu wa kijeshi wa kufuatwa. Tulia kilakitu kitawekwa wazi baada ya ofisi ya mkuu wa kambi CO kwenda kwa CoS na kuombewa vibali wahusika kukamilika na kukabidhiwa kwa jeshi la polisi
 
Hili jeshi la polisi sio poa kwa kukamata watu! Ww jifanye tu invincible utajikuta kituo cha polisi hutaamini.
Halafu inaonekana wale wendawazimu wamepanda mtumbwi wa vibwengo hadi majina yao yametajwa sio kawaida hapa naona watu wakila 50+ years in prison

:BLELELE:
Ni hivi jeshi la polisi la Tanzania liko vizur sana kwa upelelezi ,yaan ukiona jambo halijafanyika labda ujue hawajaamua tu

Kuna ishu moja ya karibu naifahamu,kuna mwamba alikabidhiwa gar kisha akaiuza,na laini akatupa akawa hapatikani ,lkn ulifanyika upelelezi wa maana,siku akanunua umeme wa luku huko lushoto,akasomeka na watu wakatia timu saa tisa au kumi usiku na kudakwa,wapo vizur sana ila basi tu
 
MTUHUMIA NAMBA MOJA NI AFANDE WA KIKE ALIYEWATUMA, HUYO HAWEZI KUKIMBIA MKAMATENI NA YEYE ACHENI DOUBLE STANDARDs.
Kuna utaratibu wa kijeshi wa kufuatwa. Tulia kilakitu kitawekwa wazi baada ya ofisi ya mkuu wa kambi CO kwenda kwa CoS na kuombewa vibali wahusika kukamilika na kukabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa utaratibu wa kisheria uraiani kufuatwa.
 
Hii haiko sawa sasa hao waliosambaza hizo video si ndo wamesaidia wananchi na wao jeshi la polisi kujua ukatili wanaofanyiwa wananchi?? Au sababu wahusika ni watu wao?? Tanpol acheni double standard bana!!
 
Jeshi la polisi limethibitisha kuwakamata na kuwashkilia vijana waliofanya ukatili Kwa kubaka na kumsodimise Binti anaesadikika kutokea yombo
Jeshi Hilo pia limethibitisha kumshikilia Binti huyo Kwa mustakabali mwema wa maisha yake na kuonya watu wanapenda kumtafuta yeye ama ndugu zake ili wamhoji
ETI NI YA MEI 2024
 
Back
Top Bottom