Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Jeshi la Polisi Tanzania limewakamata Watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walipanga na kutekeleza uhalifu wa kumbaka na kumlawiti Msichana na kusambaza video yake mitandaoni ambapo imebainika tukio lilifanyika Swaswa Dodoma mwezi May 2024.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliyoitoa leo August 09,2024 imesema “Watuhumiwa hao wamekamatwa Mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jakson”

“Uchunguzi unaendelea kukamilishwa sambamba na kuwasaka Watuhumiwa wawili ambao bado wamejificha ili wafikishwe Mahakamani,
kwa hawa ambao bado wamejificha kama kuna yeyote anayefahamu wamejificha kwake atoe taarifa na asipofanya hivyo wakikamatwa wakiwa nyumbani au kwenye makazi yake atakamatwa na kufikishwa Mahakamani”
20240809_175059.jpg
 
Polisi waongo.kama kweli wamewakamata watuonyeshe sura zao.Na Kwa Nini hawataji nyazifa zao.kwa Nini wakikamata raia huwa wanasema mtu Fulani jina,kabila na kazi anayojishughulisha kama muuza machungwa watasema Kwa Nini Hawa hawataki nyazifa zao?wanataka kuficha Nini?.
 
Aliyewatuma ni mwanamke,na katika majina yaliyotajwa hapo hakuna la kike,hivyo ni wazi kuwa hajamatwa
Na idadi ya wanaume waliodaiwa kufanya kitendo hicho si ilisemekana ni watano mbona hapo wametajwa wanne tu na hakuna maelezo kuhusu huyo wa tano?
 
Bila kutuonesha picha za hao watuhumiwa wakiwa ndani ya pingu, siwezi kukubalii huu uongo wa mchana kweupee.

Polisi waache janja janja, tena wamkamate na huyo Captain aliowatuma hao vibakaa, wamuweke wazi tumfahamu Shetanii kuu hilo.

Mxxxxxiiiiieeeeew
 
Hili jeshi la polisi sio poa kwa kukamata watu! Ww jifanye tu invincible utajikuta kituo cha polisi hutaamini.
Halafu inaonekana wale wendawazimu wamepanda mtumbwi wa vibwengo hadi majina yao yametajwa sio kawaida hapa naona watu wakila 50+ years in prison
Polisi hawahawa!?? Wawakamate wasiwaonyeshe .... hawahawa.., !?? .... Mshapigwa hapo....
 
Back
Top Bottom