To yeye
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 35,686
- 86,968
Ndo Ivo...ukipata chance itumieLeo siku ya 3 kila siku mada hiyo hiyo.
Au naye MUliro anataka ampindue Wambura?
Sirro alipata u IGP kwa kiki za media Magufuli akaingia King
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndo Ivo...ukipata chance itumieLeo siku ya 3 kila siku mada hiyo hiyo.
Au naye MUliro anataka ampindue Wambura?
Sirro alipata u IGP kwa kiki za media Magufuli akaingia King
Inawezekana tukio lilifanyika huko nyuma. Na eneo pia lilikuwa ni dodoma? sio Dar es salaam, yombo dovya?Inawezekana tukio lilifanyika mwezi may,ila video clips zikavuja mwezi huu. It's possible.
Jambo la umuhimu ni kuwa haki itendeke na Binti afanyiwe counselling asije kujizulu.
Ahsante ila hoja hapo ni dada kubakwa na polisi kuja na sarakasi kila kukicha...= wahalifu
sasa tutatoa taarifa vipi na nyie mnazuia video kusambazwa!sasa mm nitawajuaje watuhumiwa bila kuangalia videoJeshi la Polisi ningependa kutoa taarifa ya uchunguzi wa tukio ambalo lilisambazwa katika mitandao ya kijamii kupitia picha mjongeo (video clip) kuanzia Agosti 2, 2024 ikimwonyesha binti mmoja akifanyiwa vitendo vya ukatili.
Uchunguzi uliofanyika hadi sasa umefanikisha kumpata binti aliyefanyiwa ukatili huo na amehifadhiwa eneo salama na anaendelea kupata huduma zinazostahili kupewa mtu aliyefanyiwa ukatili wa aina hiyo.
Aidha uchunguzi umebaini tukio hilo lilifanyikia eneo la Swaswa katika Jiji la Dodoma mwezi Mei 2024.
Pia soma: Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa
Pia hadi sasa uchunguzi umefanikisha kukamatwa watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walipanga na kutekeleza uhalifu huo. Watuhumiwa hao wamekamatiwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nikson Idala Jakson.
Jeshi la Polisi lingependa kueleza pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne huko Dar es Salaam waliokiuka sheria na kusambaza picha mjongeo wa tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii ambao ni Frora Mlombola, Aghatha Mchome, Madatha Jeremiah Budodi na James Nyanda Paulo.
Pia watuhumiwa wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza taarifa za uongo mitandaoni zinazosema RIP.
Binti aliyebakwa na kulawitiwa akutwa amefariki. Taarifa nyingine ya uongo inasema Mama wa binti huyo amedondoka na kufariki. Watuhumiwa wawili wamekamatwa huko Arusha na wawili Mkoani Dar es Salaam ambao majina yao ni Amos Lwiza, Adam Dongo, Venance Mallya na Isack Elias.
Uchunguzi unaendelea kukamilishwa sambamba na kuwasaka watuhumiwa wawili ambao bado wamejificha ili wafikishwe mahakamani. Kwa hawa ambao bado wamejificha kama kuna yeyote anayefahamu wamejificha kwake atoe taarifa na asipofanya hivyo wakikamatwa wakiwa nyumbani au kwenye makazi yake atakamatwa na kufikishwa Mahakamani.
Jeshi la Polisi lingependa kutoa onyo kwa baadhi ya watu ambao hawana mamlaka ya kufanya hivyo waache tabia ya kwenda kwenye eneo ambalo lilitajwa kuwa huyo binti anaishi wakimtafuta yeye na familia yake ili wawahoji au kuwaona. Kufanya vitendo vya aina hiyo ni kuwatweza utu wao na kuwatonesha majeraha waliyonayo mioyoni mwao.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania
Wangetaja hata majina yao hao waliojifichasasa tutatoa taarifa vipi na nyie mnazuia video kusambazwa!sasa mm nitawajuaje watuhumiwa bila kuangalia video
Eti Harufu ya chenga ya akili🤣Swal lako gumu nani wakulijibu? Maanake huna Imani na mamlaka ya Uchunguzi. 🤣🤣 Safi umeanza kunusa harufu ya Chenga ya akili taratibu.
Kuna jamaa aliua MKOA wa Kilimanjaro mkewe na jamaa aliyemfumania. Haikuchukua dakika hata 10,wakafika chuo alipokuwa anasomea,hakuna aliyepata taarifa hata mmoja. Wakaitwa rafiki zake wa katibu bila wao kujua nani anawaita na wanaitiwa nini. Zikachukuliwa tu simu zao. Baba na mama pia wakakamatwa. Ila jamaa aanadunda mtaani na ni dereva wa gari za Serikali kwa Sasa. Na yupo kwenye mitandao ya kijamii. Wangeamua wangempotezaNi hivi jeshi la polisi la Tanzania liko vizur sana kwa upelelezi ,yaan ukiona jambo halijafanyika labda ujue hawajaamua tu
Kuna ishu moja ya karibu naifahamu,kuna mwamba alikabidhiwa gar kisha akaiuza,na laini akatupa akawa hapatikani ,lkn ulifanyika upelelezi wa maana,siku akanunua umeme wa luku huko lushoto,akasomeka na watu wakatia timu saa tisa au kumi usiku na kudakwa,wapo vizur sana ila basi tu
Una hakika wewe siyo punga kweli?Hii kari. CHADEMA na Rais wa TLS walituaminisha kuwa huyu alilawitiwa na kina Napena Makonda kule Gongo.la Mboto kumbe wala si Yombo Dovya. Kwa nini nao wasikamatwe kwa kusambaza chuki za kisiasa?
Una hakika wewe siyo punga kweli?Hii kari. CHADEMA na Rais wa TLS walituaminisha kuwa huyu alilawitiwa na kina Napena Makonda kule Gongo.la Mboto kumbe wala si Yombo Dovya. Kwa nini nao wasikamatwe kwa kusambaza chuki za kisiasa?
Inawezekana tukio lilifanyika huko nyuma. Na eneo pia lilikuwa ni dodoma? sio Dar es salaam, yombo dovya?
Inawezekana ndio katika hao 2 waliotoroka,tuwe na subira wajameniBila afande mwanamke aliyefadhili shambulio hili kukamatwa tutakuwa hatuelewi kitu no double standards
Huyu kijan kwenye picha hapo ndio Clinton alisoma shuke ya secondary mbagala kuu akahamishwa na kunalizia mbagala secondary. Chanzo ni utukutu na bangiJeshi la Polisi Tanzania limewakamata Watuhumiwa wanne kati ya sita ambao walipanga na kutekeleza uhalifu wa kumbaka na kumlawiti Msichana na kusambaza video yake mitandaoni ambapo imebainika tukio lilifanyika Swaswa Dodoma mwezi May 2024.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime aliyoitoa leo August 09,2024 imesema “Watuhumiwa hao wamekamatwa Mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani ambao ni Clinton Honest Damas kwa jina maarufu Nyundo, Praygod Edwin Mushi, Amini Lord Lema na Nickson Idala Jakson”
“Uchunguzi unaendelea kukamilishwa sambamba na kuwasaka Watuhumiwa wawili ambao bado wamejificha ili wafikishwe Mahakamani,
kwa hawa ambao bado wamejificha kama kuna yeyote anayefahamu wamejificha kwake atoe taarifa na asipofanya hivyo wakikamatwa wakiwa nyumbani au kwenye makazi yake atakamatwa na kufikishwa Mahakamani”
View attachment 3065469