mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake, ACP Jumanne Murilo limekiri kuwashikilia wanachama wa BAWACHA waliokuwa wanafanya mazoezi ya viungo(jogging) na mwanahabari Harlod Shemsanga wa MGAWE TV. "Walikuwa na viashiria venye kupelekea uvunjifu wa amani"
"Nimepokea taarifa ya watu waliokamatwa, walikuwa na viashiria vyenye kupelekea uvunjifu wa amani kwa kutengeneza hisia zenye mitizamo ya kisiasa kupitia kivuli cha mazoezi" amesema ACP Jumanne Murilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM akizungumzia kukamatwa kwa wanachama wa BAWACHA