Jeshi la Polisi lawashikiria wanachama BAWACHA walokuwa wanafanya mazoezi ya viungo (jogging)

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake, ACP Jumanne Murilo limekiri kuwashikilia wanachama wa BAWACHA waliokuwa wanafanya mazoezi ya viungo(jogging) na mwanahabari Harlod Shemsanga wa MGAWE TV. "Walikuwa na viashiria venye kupelekea uvunjifu wa amani"

"Nimepokea taarifa ya watu waliokamatwa, walikuwa na viashiria vyenye kupelekea uvunjifu wa amani kwa kutengeneza hisia zenye mitizamo ya kisiasa kupitia kivuli cha mazoezi" amesema ACP Jumanne Murilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM akizungumzia kukamatwa kwa wanachama wa BAWACHA
 
safi sana, ni vyema washughulikiwe ipasavyo, amani ya nchi sio ya kuchezewa.

vipo vya kuchezea, unaweza kuchezea; kitambi chako, kidevu chako lkn kamwe usijaribu kuchezea Amani ya nchi utashughulikiwa bila huruma.

waswahili husema;"mtoto wa nyoka ni nyoka" tayari walisha fundishwa vitendo viovu na viongozi wao, kama kiongozi wao anatuhumiwa kwa vitendo vya kihalifu sembuse wafuasi wake.

Haya yote ni matokeo ya Mwenyekiti muhalifu/Gaidi.
 
virungu tu hahaha
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake, ACP Jumanne Murilo limekiri kuwashikilia wanachama wa BAWACHA..
Au walikuwa wanataka kuchoma moto barakoa sorry barabara, halafu neno viashiria ni maalumu ka Chadema maana halitumiki kwa wanaccm.

Walikuwa wamebeba mikono yao au raba, hata wanawake wasio na silaha wanaogopwa hivyo!
 
safi sana, ni vyema washughulikiwe ipasavyo, amani ya nchi sio ya kuchezewa.
vipo vya kuchezea, unaweza kuchezea; kitambi chako, kidevu chako lkn kamwe usijaribu kuchezea Amani ya nchi utashughulikiwa bila huruma.
waswahili husema;
"mtoto wa nyoka ni nyoka"
tayari walisha fundishwa vitendo viovu na viongozi wao, kama kiongozi wao anatuhumiwa kwa vitendo vya kihalifu sembuse wafuasi wake.
Haya yote ni matokeo ya Mwenyekiti muhalifu/Gaidi.
wafuasi wa Mbowe sio wa kuwaamini hata kidogo, hawa watu ni washari, watukutu, wahuni, wahalifu,majambazi, wauza madawa n.k, yaani kuna mchanganyiko wa kila uovu.
yaani ni Genge la wahuni.
 
Jogging ni kuvunja amani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…