Inatia sana Hasira kuona Chombo Cha Dola ambacho kinawajibika kuhakikisha Usalama wa Raia, kinakua Cha kwanza Kutafuta sababu za kipuuzi kabisa na ambazo ni mwendawazimu pekee ndio anaweza kuzikubali kuhalalisha Utekaji ,na Mauaji ya Raia Nchini.
View attachment 3374985
Padre KITIMA nusura auwawe, kwamba ni wivu wa mapenzi? Kisasi? Alikua anafanya Jaribio la KUJIUA?.
MDUDE kabebwa kwake Usiku na watu wenye Bunduki na Silaha, mbele ya Mke wake na watoto.
Soka kapotezwa
LISSU alipigwa Risasi 16
Majuzi tumeshuhudia Askofu akisimulia alivyokua anafuatwa Kwa Gari na watu wenye Nia Ovu.
Sheikh Zanzibar kakutwa kauliwa, Kuna Sheikh mpaka Leo hajulikan alipo .
Visa vya Utekaji zaidi ya watu 100 vimeripotiwa.
Endeleni kuleta Uhuni, Bahati mzuri Kila kitu kipo wazi, Matendo yenu Maovu mnayoyafanya, yanajulikana, Nyakati zinakuja ambazo mtaumbuliwa na kuwajibishwa.
Kama wanajiteka, kama wanatekwa sababu ya wivu wa mapenzi, kisasi na blaa blaaj zenu mlosema, kwanini hamuwakati hao watekaji?? Kwanini hamuwakamati wauaji??? Intelijensia yenu inawapa sababu za watu kutekwa na kuuliwa ila haiwaambii ni akina nani wanaoteka na kuua kiasi mnashindwa kuwakamata??.