Jeshi la Polisi liendelee kuwakamata wote wenye kuleta maneno ya Uchochezi na kuwatupa Ndani kwa mahojiano

Ndugu zangu Watanzania,

Nalipongeza jeshi la polisi kuanza kuchukua hatua za kuwakamata na kuwahoji wote wenye kutumia lugha za uchochezi, ubaguzi na zenye hatari ya kuligawa Taifa na kuleta machafuko na mpasuko nchini.

Japo naona ni kama hatua zinazoanza kuchukuliwa kwa sasa zilichelewa kidogo, hata hivyo ni jambo jema na imetupatia faraja na kutuliza mioyo yetu ambao tulikuwa tunaona hatari ya kauli zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya watu kwa kutumia vibaya uhuru wa demokrasia uliostawi hapa nchini pasipo kuchukuliwa hatua madhubuti.

Kila mtu ni lazima afahamu kuwa uhuru hauwezi kuwa kwa ajili ya kuwadhalilisha wengine, kuwavunjia heshima wengine,k umtukana na kumshambulia Mh. Rais kwa lugha zilizokosa hekima na adabu hata pasipo sababu. Ni lazima watu wazingatie sheria.

Kuwaacha watambe na matusi yao hadharani pasipo kuchukuliwa hatua ilikuwa ni kupanda mbegu mbaya, kuliweka Taifa katika hali ya hatari ya kuleta machafuko, mpasuko, ubaguzi, mgawanyiko na kuweka Rehani utulivu na amani ya Taifa letu.

Kilichokuwa kikiendelea hasa kutoka katika vinywa na midomo ya Viongozi wa CHADEMA ilikuwa siyo demokrasia wala uhuru wala ustaarabu wala ulikuwa hauwezi kukubalika katika Taifa lolote lile, bali ilikuwa ni uhuni, vurugu na hatari tupu kwa Taifa.

Hali ile haipaswi kuvumiliwa wala kuachiwa kuwa ni utamaduni au kawaida ya mtu kusimama jukwaani na kuanza kumtukana Rais,kutumia lugha za ubaguzi kwa misingi ya ukabila, ukanda, Udini na hata jinsia pamoja na kuhamasisha machafuko na chuki katika vifua vya Watanzania.

Kamwe tusikubali tena kuulea utamaduni uliotaka kuonekana kama kawaida, tusiwape nafasi wahuni na watu waliokosa adabu na malezi mazuri kutoka kwa wazazi wao wakaharibu amani na utulivu wa Taifa letu.

Jeshi la Polisi liendelea kwa kasi na nguvu kubwa kuwazoa na kuwahoji wote watakao endelea kutumia maneno yasiyo kubalika katika jamii yetu Kisheria na Kikatiba. Isikubalike na isitolewe nafasi ya watu kutumia vibaya uhuru uliopaliliwa na serikali yetu kupandikiza chuki miongoni mwao Watanzania.

Jeshi la polisi lisimuogope mtu au kikundi au chama wala kuogopa maneno ya watu au matamko ya watu au taasisi za kimataifa katika jambo linalogusa usalama wetu, maana ni sisi tutakao umia nchi ikipasuka na kupasuliwa na hawa wenye uroho wa madaraka.

Kamata wote tupa ndani kwa ajili ya mahojiano, msisikilize makelele wala nyaraka za vikundi vya wanaharakati kutoka mahali popote, maana ukikosa msimamo kiuongozi na watu wakijua kuwa huna msimamo na ni mtu wa kutetemeka na kutetereshwa lazima wakuyumbishee na kukufanyia kila aina ya vituko.

Sasa ni wakati wenu Jeshi la Polisi kusonga mbele bila hofu wala wasiwasi, ilimradi tu mnatekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na katiba ya Nchi.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Sasa ni 5 Rs, imeongezeka RUNGU
 
Antanana uone cha moto.
CCCM hakuna kitu wanaogopa kama maandamano!!!

Ni jambo la kawaida, Nchi zilizoendelea wametengewa na maeneo kabisa.

Mtu asiye na silaha, anayetembea na kupaza sauti kudai HAKI anatakiwa asikilizwe Si kukamatwa.

Msiogope
 
Nchi inaangamia kwa watu wake kukosa maarifa. Kizazi cha Chawa hiki tutaona na kusikia mengi
 
Watu hawawezi kuachwa tu wakawa wanatoa lugha za uchochezi na matusi halafu waachwe tu kana kwamba wanaogopwa. Ni lazima tulinde amani yetu kwa wivu mkubwa sana
 
CCCM hakuna kitu wanaogopa kama maandamano!!!

Ni jambo la kawaida, Nchi zilizoendelea wametengewa na maeneo kabisa.

Mtu asiye na silaha, anayetembea na kupaza sauti kudai HAKI anatakiwa asikilizwe Si kukamatwa.

Msiogope
Ingia barabarani uandamane na kuongoza maandamano ili uone kitakachokupata.siyo ulete lugha zako za uchochezi za kuhamasisha machafuko halafu wewe unajificha chooni kwako
 
Wewe ni mpuuzi
Wenzako tuko ccm kitambo lakini hatufurahishwi na baadhi ya mambo kandamizi
Nenda kaandamane huko kama unaunga mkono mimatusi ya wahuni wachache wanaotaka kuharibu amani na utulivu wa Taifa letu,. Lazima wachochezi wote wawajibishwe na kukamatwa popote walipo
 
Mimi sio muhuni wewe mpuuzi
Maisha mzuri tu na kadi ya ccm ninayo toka 2007
Bwege wewe

Wenzako tunapenda kuona haki na sio kila kitu kushabikia

#InIbrahimTraorevoice
 
Tangia lini kumtukana mwingine, kumshambulia mtu kwa lugha za matusi,ubaguzi na kila aina ya udhalilishaji ikawa haki? Mwana CM gani wewe usiye jitambua? Usiye na uchungu na Taifa lako? Usiye waza juu ya kesho ya Taifa letu? Usiye elewa athari ya ma kauli ya kihuni na kichochezi yanayotolewa na wachache wenye kutanguliza mbele matumbo yao.
 
Rudi shule wewe
IQ yako inaonekana iko low sana
 
Back
Top Bottom