antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Wacha porojo..Ndio demokrasia hiyo ya kutukana watu?
Wametukana matusi gani?!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wacha porojo..Ndio demokrasia hiyo ya kutukana watu?
Rubbish from a rabid mindNadhani nimeeleweka ,tuifanye nchi yetu sehemu ya amani, ni Bora kula kande huku tukiwa na amani ,kulikoni kula nyama utumwani,,polisi hakikisheni kila mwenye viashiria vya uhaini anakamatwa hata mwenye dalili za uhaini asiachwe ! Inchi iwe salama ,
Nadhani nimeeleweka ,tuifanye nchi yetu sehemu ya amani, ni Bora kula kande huku tukiwa na amani ,kulikoni kula nyama utumwani,,polisi hakikisheni kila mwenye viashiria vya uhaini anakamatwa hata mwenye dalili za uhaini asiachwe ! Inchi iwe salama ,
Soma ufahamu kwanini nimemjibu hivyo huyo ndugu yangu mtanzaniaUnapomwambia mwenzako aende mahakamani, Kwani wewe umeenda mahakamani?
Mimi sina haja ya kutumia jina langu hapa maana sitafuti cheo kama ww. Na isitoshe sijavunja sheria zozote za hili jukwaa kwa kutumia jina bandia.Kibaya zaidi na cha kuchekesha unaandika huku umejificha kwako na inatumia jina bandia,kama wewe mwanaume toka hadharani na hayo maneno yako ili ukione cha mtema kuni
Hujajibu swali langu, nimekuuliza kwa nini wewe hujaenda mahakamani? sasa hilo la kuniambia nikasome, mh!!!!Soma ufahamu kwanini nimemjibu hivyo huyo ndugu yangu mtanzania
Mahakama ziko Kenya, hapa kuna majengo ya mahakama yaliyo chini ya Makada wa CCM. Labda ungemshauri aende kwenye mahakama za kimataifa, huko serikali huwa haishindi maana hakuna amri toka juu.Soma ufahamu kwanini nimemjibu hivyo huyo ndugu yangu mtanzania
HahahahaNadhani nimeeleweka ,tuifanye nchi yetu sehemu ya amani, ni Bora kula kande huku tukiwa na amani ,kulikoni kula nyama utumwani,,polisi hakikisheni kila mwenye viashiria vya uhaini anakamatwa hata mwenye dalili za uhaini asiachwe ! Inchi iwe salama ,
post nzuri sana, serikali iwe makini sana tulinde tunu yetu hii adhimu sana duniani namaanisha amani na upendo kwa watanzania.Nadhani nimeeleweka ,tuifanye nchi yetu sehemu ya amani, ni Bora kula kande huku tukiwa na amani ,kulikoni kula nyama utumwani,,polisi hakikisheni kila mwenye viashiria vya uhaini anakamatwa hata mwenye dalili za uhaini asiachwe ! Inchi iwe salama ,
Ni kweli na hapo ndio jeuri yenu ndogo ilipo, hiyo mbeleko itakatika haina muda. Narudia tena, mapinduzi ya kijeshi ama machafuko ndio yataleta mabadiliko ya kweli ya kimfumo hapa nchini.Toka hadharani ukaandamane uone utakavyonyakuliwa kama kifaranga na kutupwa ndani. Siyo kujificha huku na kuandika porojo zako za kila siku
Toka hadharani ukaandamane uone utakavyonyakuliwa kama kifaranga na kutupwa ndani. Siyo kujificha huku na kuandika porojo zako za kila siku
Naunga mkono hoja 100% tumeshasema sana hapa JF, "sikio la kufa halisikii dawa" watu wanajifanya hawaelewi.Ndugu zangu Watanzania,
Nalipongeza jeshi la polisi kuanza kuchukua hatua za kuwakamata na kuwahoji wote wenye kutumia lugha za uchochezi, ubaguzi na zenye hatari ya kuligawa Taifa na kuleta machafuko na mpasuko nchini.
Japo naona ni kama hatua zinazoanza kuchukuliwa kwa sasa zilichelewa kidogo, hata hivyo ni jambo jema na imetupatia faraja na kutuliza mioyo yetu ambao tulikuwa tunaona hatari ya kauli zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya watu kwa kutumia vibaya uhuru wa demokrasia uliostawi hapa nchini pasipo kuchukuliwa hatua madhubuti.
Kila mtu ni lazima afahamu kuwa uhuru hauwezi kuwa kwa ajili ya kuwadhalilisha wengine, kuwavunjia heshima wengine,k umtukana na kumshambulia Mh. Rais kwa lugha zilizokosa hekima na adabu hata pasipo sababu. Ni lazima watu wazingatie sheria.
Kuwaacha watambe na matusi yao hadharani pasipo kuchukuliwa hatua ilikuwa ni kupanda mbegu mbaya, kuliweka Taifa katika hali ya hatari ya kuleta machafuko, mpasuko, ubaguzi, mgawanyiko na kuweka Rehani utulivu na amani ya Taifa letu.
Kilichokuwa kikiendelea hasa kutoka katika vinywa na midomo ya Viongozi wa CHADEMA ilikuwa siyo demokrasia wala uhuru wala ustaarabu wala ulikuwa hauwezi kukubalika katika Taifa lolote lile, bali ilikuwa ni uhuni, vurugu na hatari tupu kwa Taifa.
Hali ile haipaswi kuvumiliwa wala kuachiwa kuwa ni utamaduni au kawaida ya mtu kusimama jukwaani na kuanza kumtukana Rais,kutumia lugha za ubaguzi kwa misingi ya ukabila, ukanda, Udini na hata jinsia pamoja na kuhamasisha machafuko na chuki katika vifua vya Watanzania.
Kamwe tusikubali tena kuulea utamaduni uliotaka kuonekana kama kawaida, tusiwape nafasi wahuni na watu waliokosa adabu na malezi mazuri kutoka kwa wazazi wao wakaharibu amani na utulivu wa Taifa letu.
Jeshi la Polisi liendelea kwa kasi na nguvu kubwa kuwazoa na kuwahoji wote watakao endelea kutumia maneno yasiyo kubalika katika jamii yetu Kisheria na Kikatiba. Isikubalike na isitolewe nafasi ya watu kutumia vibaya uhuru uliopaliliwa na serikali yetu kupandikiza chuki miongoni mwao Watanzania.
Jeshi la polisi lisimuogope mtu au kikundi au chama wala kuogopa maneno ya watu au matamko ya watu au taasisi za kimataifa katika jambo linalogusa usalama wetu, maana ni sisi tutakao umia nchi ikipasuka na kupasuliwa na hawa wenye uroho wa madaraka.
Kamata wote tupa ndani kwa ajili ya mahojiano, msisikilize makelele wala nyaraka za vikundi vya wanaharakati kutoka mahali popote, maana ukikosa msimamo kiuongozi na watu wakijua kuwa huna msimamo na ni mtu wa kutetemeka na kutetereshwa lazima wakuyumbishee na kukufanyia kila aina ya vituko.
Sasa ni wakati wenu Jeshi la Polisi kusonga mbele bila hofu wala wasiwasi, ilimradi tu mnatekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na katiba ya Nchi.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Wenzako wana akili siasa za kenya huwezi fananisha na siasa za bongo, maskini wapo dunia nzima, au hulijui hilokahamie huko kenya, Kenya siyo nchi ya kuitolea mfano. umeona mitaa ya maskini wa Kenya. Usifananishe vitu visivyoendana, hatutaki siasa za hovyo km zile za Kenya.