Jeshi la polisi limebariki huu wizi Kariakoo?

Jeshi la polisi limebariki huu wizi Kariakoo?

Kauza cheni ya bandia kapewa pesa ya bandia,halafu anataka polisi waingilie kati,are you serious?
Yeye kajifanya anakujua nawewe ukajifanya unamjua tena ukanywa na juisi yake,halafu unataka polisi aingilie kati,kweli mjini unakunywa juisi ya mtu ambaye humjui?
Acha utani mkuu.
Behave basi.
 
sasa mbona mnanishambulia utafikiri mi ndo nimekunywa hiyo Juice wakuu😂😂😂mki nimeandika kwa sababu nimeshuhudia wengi wakitapeliwa na pengine wengi wao wanaweza kuwa wageni wa jiji pia hii ni alert kwa wengine wasiingie mkenge

sasa naona watu mmenimaindi
haya karibuni juice na nyie basi😂😂
 
Sasa hapo wizi upo wapi?
Mimi naona NI mbinu tu za biashara.

Hata kondakta wa daladala kabla hamj
japanda gari atajifanya anawajua, utamsikia mamdogo Panda twende, anko ingia tuwahi. Mkipanda sasa ....
 
Vijana wa mkoani Kila siku wanaingia Dar na tamaa zao na ushamba wao!
Unawezaje kunywa juisi za burej? Tena za kwenye madeli! Check your personality bro! Kwa hayo madeli huyo muuzaji hawezi kumsimamisha mtu serious. Otherwise uwe mtafuna miwa na karanga njiani.
 
sasa mbona mnanishambulia utafikiri mi ndo nimekunywa hiyo Juice wakuu[emoji23][emoji23][emoji23]mki nimeandika kwa sababu nimeshuhudia wengi wakitapeliwa na pengine wengi wao wanaweza kuwa wageni wa jiji pia hii ni alert kwa wengine wasiingie mkenge

sasa naona watu mmenimaindi
haya karibuni juice na nyie basi[emoji23][emoji23]
Umeyavagaa Mwenyewe, mjini hapa sio Kila unalo liona lazima ulilete hapa JF, ishu imekaa ki-"Facebook" ndio maana unatolewa Mapovu.. [emoji23][emoji23]
 
Hiyo tabia ya kula ovyo hovyo mitaani emeitoa wapi?
Yaani unishobokee sikujui unipe juice niipokee?

Punguza njaa mambo mengine ni ujinga tu

Hiyo tabia ya kula ovyo hovyo mitaani emeitoa wapi?
Yaani unishobokee sikujui unipe juice niipokee?

Punguza njaa mambo mengine ni ujinga tu!
leo kila mtu humu halagi njiani,basi haina noma,fresh.
 
Aiseeeh! Nitaanza kuwa mstaarabu kwenye biashara yangu ya juice ili wateja wasinikimbie or kufikiri nitawaibia.
 
Habari wana JF, kuna huu wizi sijui niite utapeli ambao binafsi nimeanza kuushuhudia tangu mwaka 2022 kwa maeneo ya Kariakoo na kila mara nikipita eneo hilo nakuta huo wizi unaendelea utapeli wenyewe unafanywa na jamaa wauza juice ya miwa mitaa ya karume mbele ya TBL(Tanzania Breweries Limited)

Wizi unafanyika kama ifuatavyo
Muuza juice atakuita na kujifanya amekufananisha kisha atakuuliza ''Vipi mzee daah kitambo sana mwanangu, vipi siku hizi wapi?''
Wewe utajibu labda nipo Magomeni siku hizi
Muuza juice: Anhaa ndo maana kule kitaa sikuoni siku hizi
wewe: Wapi?Kule kitunda au?

Basi hapo ndo utakuwa umeyavagaa jamaa atajifanya kukujua sana atakuuliza kuhusu story za vipi wale jamaa wanaopiga matizi uwanjani pale bado wapo?

Actually hakuna sehemu ambayo haina uwanja wa mpira so yote kwa yote jamaa atakuwa amekuteka akili kwa kujifanya anakujua sema ni vile tu umemsahau

Kinachofuatia jamaa atakumiminia juice " karibu juice kaka"
Ukimaliza kunywa tu hiyo juice jamaa anakubadilikia na kuanza kukudai hela ya Juice
ukishindwa kulipa atakukaba, atakupiga hata kukuumiza.

Wahanga wakubwa wa haya matukio ni wale wa kuja lakini hata kama born town unaweza kujikuta umeingia mkenge vile vile

Kinachonifikirisha ni kuwa Kituo cha polisi Gerezani hakipo mbali na hapo Karume na pia maeneo ya China Plaza, hawa jamaa hawajanusa taarifa za huu ushenzi kweli?au kuna mgao, maana hawa jamaa wanafanya hii michezo kuanzia asubuhi hadi jioni tangu 2022 nimewaona hadi leo 2024 wapo.

Picha mojawapo ya mhuhusika wa hiyo michezo ni hiyo hapo huyo muuza juice na hapo alikuwa anamuingiza mkenge jamaa.

View attachment 2925320View attachment 2925321
Hili limewahi kunipata,ila kwa kuwa si mlaji hovyo jamaa tuliachana kwa amani tu,hata juice yake chafu sikunywa;

Hivi unakunywaje juice mtu anayetengeneza anavuja jasho?
 
Marehemu Zacharia na utajiri wake wote lakini alikuwa kila siku kabla hajaingia msikitini anakunywa juice ya kwenye madeli pale msikitini kitumbini nendeni mkaulize hata leo hii hayupo lakini mtaambiwa , sembuse watu wengine wa kawaida ??
 
Unasimamishwaje na mtu usiyemjua, usiyejua nia yake na kuongea naye kwa muda wote huo?

Kibaya zaidi, unakunywa vipi juisi yake kirahisi hivyo? Akikuwekea dawa za kukulevya na kukufanya kitu kibaya je?
Kwa jinsi unga ulivyo adimu( pongezi kama tume ya kuzuia madawa) then wakuwekee unga kumbe umebakiza nauli ya kigogo mburahati... Wanakuwekea piriton kupunguza gharama za uendeahaji wa utapeli wao.
Matepeli kiboko ni wale wanaonusa kuwa umetoka kuchukua mzigo wa kustaafu maeneo ya mlimani city.
 
Kwa jinsi unga ulivyo adimu( pongezi kama tume ya kuzuia madawa) then wakuwekee unga kumbe umebakiza nauli ya kigogo mburahati... Wanakuwekea piriton kupunguza gharama za uendeahaji wa utapeli wao.
Matepeli kiboko ni wale wanaonusa kuwa umetoka kuchukua mzigo wa kustaafu maeneo ya mlimani city.
Dawa za kulevya si lazima ziwe unga.

Bado sijaelewa inakuwaje mtu anasimamishwa hivyo na kukubali.
 
Hii mada nimeiona Twitter kitambo sana...yawezekana hapa imewah kujadiliwa ila hii system ya kufuta nyuzi yawezekana ndio inayosababisha tupate habar zilizopitwa na wakati
 
Unashindwa nini kumkatalia na kumwambia humfahamu?Achukue time yake!Cha kujiuliza:Amekupa juisi umekunywa na kukataa/kushindwa kulipa.Sasa,anakukoyonga makofi ili apate faida gani?Au anakuwa na hamu tu ya kumchabanga mpitanjia-mjinga mabanzi?🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom