Jeshi la polisi limebariki huu wizi Kariakoo?

Juice yenyewe ndio wanaweka kwenye hizo plastic?
Wajinga wajinga ndiyo wananasa kwenye upuuzi kama huu. Dunia ya leo mtu ambaye hata humjui, akumiminie hiyo mi-juice inayopigwa vumbi barabarani huko, ufakamie! Kama wameweka dawa za kulewesha? Kama ameweka sumu? Ujinga ulioje!
 
Aiseh kuna muda nakuwaga bored gheto natafuta ugomvi, jmosi ijayo nitaenda kujipitisha mitaa ya hapo ili ninywe hio juice maksudi niache kulipa ili nione mtu wa kunikaba nimtoe meno ya sebureni.

Mkuu (mtoa maada) week ijayo ukipita hapo utakuta huyo mtu wako wa juice hana meno ya sebureni.
 
Habari wana JF,

Kuna huu wizi sijui niite utapeli ambao binafsi nimeanza kuushuhudia tangu mwaka 2022 kwa maeneo ya Kariakoo na kila mara nikipita eneo hilo nakuta huo wizi unaendelea utapeli wenyewe unafanywa na jamaa wauza juice ya miwa mitaa ya karume mbele ya TBL (Tanzania Breweries Limited)

Wizi unafanyika kama ifuatavyo:
Muuza juice atakuita na kujifanya amekufananisha kisha atakuuliza ''Vipi mzee daah kitambo sana mwanangu, vipi siku hizi wapi?''

Wewe utajibu labda nipo Magomeni siku hizi.

Muuza juice: Anhaa ndiyo maana kule kitaa sikuoni siku hizi.

Wewe: Wapi? Kule kitunda au?

Basi hapo ndo utakuwa umeyavagaa jamaa atajifanya kukujua sana atakuuliza kuhusu story za vipi wale jamaa wanaopiga matizi uwanjani pale bado wapo?

Actually hakuna sehemu ambayo haina uwanja wa mpira so yote kwa yote jamaa atakuwa amekuteka akili kwa kujifanya anakujua sema ni vile tu umemsahau

Kinachofuatia jamaa atakumiminia juice " karibu juice kaka".

Ukimaliza kunywa tu hiyo juice jamaa anakubadilikia na kuanza kukudai hela ya Juice.

ukishindwa kulipa atakukaba, atakupiga hata kukuumiza.

Wahanga wakubwa wa haya matukio ni wale wa kuja lakini hata kama born town unaweza kujikuta umeingia mkenge vile vile

Kinachonifikirisha ni kuwa Kituo cha polisi Gerezani hakipo mbali na hapo Karume na pia maeneo ya China Plaza, hawa jamaa hawajanusa taarifa za huu ushenzi kweli? Au kuna mgawo, maana hawa jamaa wanafanya hii michezo kuanzia asubuhi hadi jioni tangu 2022 nimewaona hadi leo 2024 wapo.

Picha mojawapo ya mhuhusika wa hiyo michezo ni hiyo hapo huyo muuza juice na hapo alikuwa anamuingiza mkenge jamaa.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
sa buku tu ndo ikufanye uite jeshi la polisi! watoto wa mama bhanaaa[emoji848][emoji848]
 
Cha muhimu usinywe kitu kutoka kwa mtu usiemjua labda kama umenda kwa lengo la kununua hiyo juisi.
 
huo sio utapeli,inaitwa"KAA KIMASTA"

inaruhusiwa kabisa kumhadaa mteja kwa lugha ya ukarimu kisha kumdai pesa kwa huduma uliyompa.

kama huamini haya ninayokwambia ingia saloon kunyoa kisha baada ya kumaliza,itikia kila unachoambiwa,utakapodaiwa elfu 15,ndio utajua hujui.
 
Ukiwa unazubaa zubaa utatapeliwa tu,ukiwa busy na ratiba zako hakuna hata wa kukuuliza
 
Yani ninavyokuwaga makini kariakoo sitaki hata kuguswa wala kuitikia salamu yoyote ile haswa kwa hao wachuuzi maana unaweza kushtuka vitu vyako vimeibiwa vyote hata kwa mgusano tu😂😂😂. Hatakama nakufahamu nikikuona Town napita na mishe zangu niwahi nyumbani

Unaanzaje kupokea juice na kuitikia Wito wa mtu usiyemjua haswa njiani tena Karume?!
 
Hiyo haijaanza Leo nakumbuka mwaka 2015 nikiwa first year tumepata boom tukazama kariakoo na washikaji, kufika karume tukakaribishwa Juice tuliambiwa ni Tshs100 glass, tukanywa kujakulipa TSH 100 jamaa wakatubadilikia kuwa uliona wapi juice ikiuzwa Tsh100
 
Back
Top Bottom