Jeshi la polisi limebariki huu wizi Kariakoo?

Kauza cheni ya bandia kapewa pesa ya bandia,halafu anataka polisi waingilie kati,are you serious?
Yeye kajifanya anakujua nawewe ukajifanya unamjua tena ukanywa na juisi yake,halafu unataka polisi aingilie kati,kweli mjini unakunywa juisi ya mtu ambaye humjui?
Acha utani mkuu.
Behave basi.
 
sasa mbona mnanishambulia utafikiri mi ndo nimekunywa hiyo Juice wakuu😂😂😂mki nimeandika kwa sababu nimeshuhudia wengi wakitapeliwa na pengine wengi wao wanaweza kuwa wageni wa jiji pia hii ni alert kwa wengine wasiingie mkenge

sasa naona watu mmenimaindi
haya karibuni juice na nyie basi😂😂
 
Sasa hapo wizi upo wapi?
Mimi naona NI mbinu tu za biashara.

Hata kondakta wa daladala kabla hamj
japanda gari atajifanya anawajua, utamsikia mamdogo Panda twende, anko ingia tuwahi. Mkipanda sasa ....
 
Vijana wa mkoani Kila siku wanaingia Dar na tamaa zao na ushamba wao!
Unawezaje kunywa juisi za burej? Tena za kwenye madeli! Check your personality bro! Kwa hayo madeli huyo muuzaji hawezi kumsimamisha mtu serious. Otherwise uwe mtafuna miwa na karanga njiani.
 
Umeyavagaa Mwenyewe, mjini hapa sio Kila unalo liona lazima ulilete hapa JF, ishu imekaa ki-"Facebook" ndio maana unatolewa Mapovu.. [emoji23][emoji23]
 
Hiyo tabia ya kula ovyo hovyo mitaani emeitoa wapi?
Yaani unishobokee sikujui unipe juice niipokee?

Punguza njaa mambo mengine ni ujinga tu

Hiyo tabia ya kula ovyo hovyo mitaani emeitoa wapi?
Yaani unishobokee sikujui unipe juice niipokee?

Punguza njaa mambo mengine ni ujinga tu!
leo kila mtu humu halagi njiani,basi haina noma,fresh.
 
Aiseeeh! Nitaanza kuwa mstaarabu kwenye biashara yangu ya juice ili wateja wasinikimbie or kufikiri nitawaibia.
 
Hili limewahi kunipata,ila kwa kuwa si mlaji hovyo jamaa tuliachana kwa amani tu,hata juice yake chafu sikunywa;

Hivi unakunywaje juice mtu anayetengeneza anavuja jasho?
 
Marehemu Zacharia na utajiri wake wote lakini alikuwa kila siku kabla hajaingia msikitini anakunywa juice ya kwenye madeli pale msikitini kitumbini nendeni mkaulize hata leo hii hayupo lakini mtaambiwa , sembuse watu wengine wa kawaida ??
 
Unasimamishwaje na mtu usiyemjua, usiyejua nia yake na kuongea naye kwa muda wote huo?

Kibaya zaidi, unakunywa vipi juisi yake kirahisi hivyo? Akikuwekea dawa za kukulevya na kukufanya kitu kibaya je?
Kwa jinsi unga ulivyo adimu( pongezi kama tume ya kuzuia madawa) then wakuwekee unga kumbe umebakiza nauli ya kigogo mburahati... Wanakuwekea piriton kupunguza gharama za uendeahaji wa utapeli wao.
Matepeli kiboko ni wale wanaonusa kuwa umetoka kuchukua mzigo wa kustaafu maeneo ya mlimani city.
 
Dawa za kulevya si lazima ziwe unga.

Bado sijaelewa inakuwaje mtu anasimamishwa hivyo na kukubali.
 
Hii mada nimeiona Twitter kitambo sana...yawezekana hapa imewah kujadiliwa ila hii system ya kufuta nyuzi yawezekana ndio inayosababisha tupate habar zilizopitwa na wakati
 
Unashindwa nini kumkatalia na kumwambia humfahamu?Achukue time yake!Cha kujiuliza:Amekupa juisi umekunywa na kukataa/kushindwa kulipa.Sasa,anakukoyonga makofi ili apate faida gani?Au anakuwa na hamu tu ya kumchabanga mpitanjia-mjinga mabanzi?🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…