Jeshi la polisi linachangia timu zetu kukosa matokeo mazuri viwanjani ,polisi mnawasaidia wageni kutamba nyumbani

Jeshi la polisi linachangia timu zetu kukosa matokeo mazuri viwanjani ,polisi mnawasaidia wageni kutamba nyumbani

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Polisi wetu kila mahali wao wanaleta upolisi mimi huwa nachukia sana ! Timu zetu zinakwenda kucheza nje ya nchi ,zikifika zinakutana na balaa la mashabiki ,, kulipua mafataki wakati mechi inaendelea,moshi kujaa uwanjani,kuwasha miale ya kila rangi ,nk ,si fifa wala caf waliowahi kusema kufanya hivyo ni kosa! Nenda Algeria ,tunisia ,na Misri.kaangalie ligi ya brazili ,kaone mechi za bocca junior huko brazili na Amerika ya kusini ,viwanja vinalindima kwa mafataki na miale ya moto! Pitieni mechi za liverplate mtaona maajabu ya soka kwa mashabiki ,mashabiki wanamtisha mpinzani hata kabla mechi haijaanza ,fifa hawajawahi kukataza utaratibu huu hata Karia anajua ,hapa kwetu nyumbani polisi ndio wanaotupangia sisi tushangilieje mechi za soka! Unaingia uwanjani na mdomo na makofi tu, wenzetu wanatupiga na makelele ya mafataki na kulipua moshi usio na madhara viwanjani ,lakini polisi wa hapa wanataka kudumisha amani hata ndani ya dakika tisini za mchezo wa soka ,kuwaruhusu mashabiki kuingia na kila zana ya kushangilia isiyo na madhara sio kosa ! Mashaka waruhusiwe kulipua mabaluti dhaifu viwanjani na kila rangi ya moshi isiyo na madhara iruhusiwe viwanjani ,shabiki hatakiwi tu kuingia na kisu au mawe na silaha yoyote lakini sio vifaa vya ushangiliaji ,tuache kichaa cha soka kifanye kazi viwanjani ,polisi mnawasaidia wageni kucheza bila presha yoyote ya mashabiki acheni kuleta upolisi kwenye mchezo wa soka ,maadamu fifa na caf hawajakataza vibe la mashabiki mnawaonea kuwapangia namna ya kushangilia ,mchezo wa soka ni vita ya miguu ! Ni vita ya nchi na nchi ,ni vita ya klabu na klabu ,hakuna siasa kwenye soka ,kamanda mambosasa soma hiyo !
 
Back
Top Bottom