Jeshi la polisi linachunguza tuhuma za kuhusika askari katika kupotea kwa Mdude Nyagali

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Jeshi la Polisi linafuatilia kwa karibu tuhuma zilizotolewa na mwananchi mmoja ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa akiwatuhumu askari wawili kupitia mitandao ya kijamii kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi pamoja na kumuahidi kumpatia fedha.

Kufuatia taarifa hiyo, Jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai limeunda kikosi kazi ambacho tayari kimeshafika mkoani Mbeya kwa ajili ya uchunguzi juu ya suala hilo.

Wakati uchunguzi juu ya suala hilo ukiendelea, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi, yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kubaini ukweli juu ya suala hili atoe ushirikiano kwa kutoa taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi.


Soma
 
Mdude ametekwa nana kuvunja milango ya nyumba yake na watu waliovamia kwake usiku Sasa huko ni kutekwa na watu ambao ni askari sio kwamba amepotezwa na hao usalama,polisi,Sasa wanaotuhumiwa kumtekata tena wanafanyaje uchunguzi???? Wajichunguzr wenyewe tuache utani na uhai wa mtu,mungu atatuhukumu kwa uovu huu
 
Mbona taarifa ya malalamiko ya mkewe akishuhudia polisi kwa jina alihusika wanakwepa!
Mpaka hapa Mdude walimuua.
 
Yule jamaa mtoa taarifa ajihadhari wanaweza kumteka na kumpoteza ili kuficha ushahidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…