Jeshi la polisi linachunguza tuhuma za kuhusika askari katika kupotea kwa Mdude Nyagali

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu kupotea kwa mwanaharakati na kada wa Chadema, Mdude Nyagali, ambaye aliripotiwa kutoweka usiku wa kuamkia Mei 2, 2025, nyumbani kwake eneo la Iwambi, Mbeya.

Tukio hilo linadaiwa kufanywa na watu waliovamia nyumba yake, kuvunja mlango na kumchukua kwa nguvu.

=

TAARIFA KWA UMMA

JESHI LA POLISI LINACHUNGUZA TUHUMA ZA KUHUSIKA ASKARI KATIKA KUPOTEA KWA MDUDE NYAGALI

Jeshi la Polisi linafuatilia kwa karibu tuhuma zilizotolewa na mwananchi mmoja ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa akiwatuhumu askari wawili kupitia mitandao ya kijamii kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi pamoja na kumuahidi kumpatia fedha.

Kufuatia taarifa hiyo, Jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai limeunda kikosi kazi ambacho tayari kimeshafika mkoani Mbeya kwa ajili ya uchunguzi juu ya suala hilo.

Wakati uchunguzi juu ya suala hilo ukiendelea, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi, yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kubaini ukweli juu ya suala hili atoe ushirikiano kwa kutoa taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi.

View attachment 3324558
Nimejikuta nacheka yaani watekaji wajichunguze na kujihukumu..? Mbona tuna vunjana mbavu hivi..?
 
Jeshi la polisi linachunguza tuhuma za aliyetoa taarifa za polisi kuhusika na sio kuchunguza kutekwa kwa mdude
 
Attachments

  • 20250504_175227.jpg
    20250504_175227.jpg
    103.9 KB · Views: 19
Hawa watu ni ******* kweli, Mzee kataka Polisi shabai n mwingine.

Anasema Taarifa alipeleka mpaka Kwa RPC, na RCO.

Alafu bado wanatoa tamko lakijinga Jinga namna hii
Ushawahi kukaa na mjinga?
Huwa anadhani nawe mjinga mwezie,
Anafanya vitu kwa ukomo wa akili yake, akidhani ww pia ni wa akili ya ukomo wake!!
 
Yule jamaa mtoa taarifa ajihadhari wanaweza kumteka na kumpoteza
Mpaka anaenda kweenye media kueleza ameshajihakikishia hana cha kupoteza, km Hamza tu hata wakimuua na yeye sawa tu ila watu wameshajua nani wanaopiga hayo matukio ya utekaji
 
Nilitegemea kuwa polisi wangesema wamewakamata na kuwaweka ndani wale waliosema kuwa tukiwapoteza polisi musiwatafute.
 
Utaratibu wa kuchuja watu wakulitumikia jeshi hili siku hizi upoje? Nauliza tu..!
 
Jeshi la Polisi linafuatilia kwa karibu tuhuma zilizotolewa na mwananchi mmoja ambaye jina lake linaendelea kufuatiliwa akiwatuhumu askari wawili kupitia mitandao ya kijamii kuwa walimfuata kumtaka afanye nao kazi ya kijajusi pamoja na kumuahidi kumpatia fedha.

Kufuatia taarifa hiyo, Jeshi la Polisi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai limeunda kikosi kazi ambacho tayari kimeshafika mkoani Mbeya kwa ajili ya uchunguzi juu ya suala hilo.

Wakati uchunguzi juu ya suala hilo ukiendelea, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi, yeyote mwenye taarifa zitakazosaidia kubaini ukweli juu ya suala hili atoe ushirikiano kwa kutoa taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi.

View attachment 3324558
Soma
🤣🤣🤣🤣
Sijui wanatuonaje!
 
RPC alipewa Taarifa na akapuuza! Naomba Sana CHADEMA watafute mawakili watakaomsaidia mtoa taarifa asitishwe
 
Mtekaji anamchunguza aliyemtuma kuteka?. Usengelema huyo shabani anatakiwa kukamatwa na wananchi kumuua hapohapo.
 
Jeshi la policcm lina utajiri wa vilazaa kuanzia top mpaka bottom, linatoa matamko kana kwamba yanaelekezwa kwa wajinga wenzao...aibu kabisa!
Ndio maana linachojua ni kutumia nguvu badala ya akili...ktk dunia ya leo ukiwa na jeshi la aina hii vikitokea vita tutawazika hadi tuchoke!!.
 
Back
Top Bottom