Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta

Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro anazungumza na Vyombo vya Habari.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaaam linawashikilia wanaotuhumiwa wanne, Deogratius Paul Massawe (40), Bakari Idd Bakari (30), wote ni kuli wa Tegeta kwa Ndevu, Omary Issa mpigadebe wa Tegeta DAWASCO na Rashid Mtonga (29) kazi yake ni Bodaboda kwa mauaji ya mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Amani Simbayao.

Watuhumiwa hao, pamoja na wengine ambao bado wanashikiliwa kwa tuhuma hizo, wanahojiwa kwa kina, ikiwa ni pamoja na kumjeruhi mtumishi mwingine aliyefahamika kwa jina la Adriano Fredrick.

Watuhumiwa hawa ambao bado wanashikiliwa na Wanahojiwa kwa kina wakati wanawashambulia maafisa hao waliharibu pia gari la Serikali la TRA, gari namba STL 9922 aina ya Toyota Land Cruiser

======


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa wanne 1. Deogratius Paul Masawe miaka 49 kuli , mkazi wa Tegeta kwa ndevu 2. Idd Bakari miaka 30, kuli mkazi Tegeta kwa ndevu.3.Omar Issa miaka 47 ,myao, mpiga debe mkazi wa Tegeta Dawasco 4.Rashid Mtonga myao , miaka 29 kazi ya bodaboda , mkazi wa Bunju.

Wanatuhumiwa kufanya mauaji ya mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aitwaye Amani Kamguna Simbayao pia kumjeruhi Adriano Fredrick wa TRA. Watuhumiwa hao na wengine ambao bado wanahojiwa kwa kina walikamatwa baada ya kuwashambulia maafisa hao wa TRA wakati wakitekeleza majukumu yao ya kisheria. waliliharibu pia gari namba STL 9923 aina Toyota Land Cruiser Hardtop nyeupe mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Tukio hilo lilitokea tarehe 05 Desemba, 2024 majira ya saa 03 :00 usiku Tegeta kwa Ndevu Kinondoni baada ya Maafisa hao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kukamata gari namba T 529 DHZ aina ya BMW rangi nyeupe lililodaiwa kuwa na makosa ya kikodi

Jeshi la Polisi Kanda maaalum ya Dar es Salaam linawaonya vikali na halitavumilia watu ambao wanataka kujenga tabia ya kuwashambulia watumishi wa Serikali wakati wakitekeleza majukumu yao licha ya kuwa wanakuwa wamefuata taratibu zote za kisheria.Jeshi halitasita kuchukua hatua kali za haraka na za kisheria dhidi ya wahusika kwa kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za haki.

Imetolewa na;

Muliro J. Muliro -SACP

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam
 
Watu wanne washikiliwa Kwa mauaji ya Afisa wa TRA kufutia kushambuliwa na wananchi Tegeta kwa ndevu.

-Deodratius Paul Masawe(40) mkazi wa Tegeta kwa Ndevu
-Bakari Idd Bakari(30) Mkazi wa Tegeta Kwa Ndevu
-Omari Issa, Mkazi wa Tegeta DAWASCO
- Rashidi Mtonga(29)

Wanatuhumiwa kwa mauaji ya Afisa wa TRA, kuharibu magari 2, gari la Serikali na Gari la Mamlaka ya Mapato Tanzania, kujeruhi mtumishi mwingine wa mamlaka ya Mapato aitwaje Adriano Fredrick pia kuna wengine wanahojiwa kwa tukio hilo.

Kamanda Muliro anasema kuwa, Jeshi la Polisi linatoa Onyo kali kwa watu wanaotaka kujenga utamaduni wa kushambuliwa Maafisa wa Serikali wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao licha ya kuwa wanafata sheria na kanuni za kutekeleza majukumu hayo.

Amesema Jeshi la Polisi halitavumilia jambo hilo hata kidogo, hatua stahiki zitachuliwa dhidi ya vitendo hivyo ipasavyo.

1733562003161.png


Pia soma:
 
Back
Top Bottom