PostGE2025 Jeshi la Polisi Mbeya lakiri kumshikilia Clemence Mwandambo kwa tuhuma za Uchochezi

PostGE2025 Jeshi la Polisi Mbeya lakiri kumshikilia Clemence Mwandambo kwa tuhuma za Uchochezi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali ya "Saint Clemence" ndugu Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni "A" Jijini Mbeya kwa tuhuma za uchochezi.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo Novemba 21, 2025 saa 5:20 asubuhi maeneo ya Uzunguni Jijini Mbeya akitoa na kusambaza maneno ya uchochezi na uchonganishi kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii za "Facebook" na "Instagram"

Upelelezi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

1000516138.jpg


Pia soma Mzee Clemence Mwandambo adaiwa kutekwa usiku wa kuamkia leo, Novemba 22, 2025
 
Ule msemo kuwa maarifa ni nguvu unakosa maana kwa sababu mtu anaweza akawa na nguvu ya maarifa mabaya na potofu.
 
Yani kipindi hiki polisi wakikamata mtu ni kosa tayari watu wanasambaza ametekwa😅😅
 
Jeshi la polisi mkoani mbeya linamshikilia mwalimu clemence mwandambo wa shule ya awali na msingi saint clemence kwa tuhuma za msudhui yasiofaa mtandaoni.

my Take:Wazazi ambao watoto wao wanafundishwa na mwalimu huyu wana kazi nzito sana
 
Back
Top Bottom