Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Jeshi la Polisi hatimaye limemfikisha Mbowe mahakamani Kisutu "kisirisiri" likimtuhumu kwa Makosa ya jinai ya ugaidi.
Naliomba Jeshi hilo litujibie maswali yafuatayo kuhusu ugaidi wa Mbowe.
1. Ni kwanini wamempeleka mahakamani Kisutu kisirisiri, bila kumuarifu yeye mtuhumiwa, ili aweze kutumia haki yake kisheria, ya kuwa na mawakili wake kwenye kesi hiyo?
2. Hapo awali RPC wa Mwanza, alitueleza kuwa wamemkamata Mbowe, kutokana na kuandaa kongamano la Katiba mpya ya nchi, ni kwanini kwenye "charge sheet" ya mahakamani, kosa hilo liwe halipo na badala yake, aonekane Mbowe kuwa alipanga njama za kigaidi za kutaka kulipua vituo vya mafuta?
3. Hapo awali Jeshi la Polisi lilituambia kuwa wanamshikilia Mbowe, kwa tuhuma kuwa alipanga njama za kuwaua viongozi wa serikali, ni kwanini walipomfikisha mahakamani, kosa hilo pia halipo?
4. Kama Mbowe anaunganishwa na watuhumiwa wengine wa ugaidi watatu waliokamatwa mwaka Jana mwezi wa 8, ni kwanini basi ichukue muda mrefu kiasi hiki hadi hivi sasa inakaribia mwaka mmoja, kwa Jeshi la Polisi kumkamata Mbowe, kwa kesi hiyo ya hatari sana?
5. Jeshi la Polisi halijataja vituo vya mafuta, ambavyo Mbowe alivi-target kuvilipua na lini tukio hilo lilikusudiwa kufanywa, hivi hiyo inaweza kutufanya sisi wananchi tuendelee kuliamini Jeshi letu la Polisi?
Hivi sisi wananchi tukiamini kuwa hii kesi ni ya kisiasa na ya kubambika, ambayo lengo lake ni Jeshi hilo ku-side upande wa watawala wa CCM, tutakuwa tumekosea kweli?