PreGE2025 Jeshi la Polisi Ruvuma latoa tamko kuhusu kukamatwa kwa Lissu, ni sababu ya Uchochezi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

WhatsApp Image 2025-04-10 at 14.07.09_d52a567e.jpg

​
TAARIFA KWA UMMA
Ndugu wanahabari, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma tunaendelea vyema na majukumu ya kusimamia sheria za nchi katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

TAARIFA YA KUKAMATWA MWENYEKITI WA CHADEMA NDUGU, TUNDU LISSU
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linapenda kutoa taarifa ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndugu, Tundu Antipas Lissu.

Mnamo tarehe 09.04.2025 katika Mtaa wa Soko Kuu, Wilaya ya Mbinga Jeshi la Polisi lilimkamata Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Kufuatia tuhuma zilizokuwa zinapelelezwa za kufanya uchochezi wa kutofanyika uchaguzi Mkuu 2025.

Mtuhumiwa huyo anahojiwa juu ya tuhuma hizo huko Dar-es- Salaam.

Jeshi la Polisi linatoa Onyo kwa vyama vyote vya siasa kutotoa maneno ya uchochezi, Kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na atakaye bainika kufanya hivyo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na, Kamanda wa Polisi (M) wa Ruvuma
 
Wachochezi, waropokaji na wafanya fujo wote inapaswa washughulikiwe mapema kwa mujibu wa sheria. Wao watoto wao wako ughaibuni sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
 
TAARIFA KWA UMMA
Ndugu wanahabari, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma tunaendelea vyema na majukumu ya kusimamia sheria za nchi katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

TAARIFA YA KUKAMATWA MWENYEKITI WA CHADEMA NDUGU, TUNDU LISSU
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linapenda kutoa taarifa ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndugu, Tundu Antipas Lissu.

Mnamo tarehe 09.04.2025 katika Mtaa wa Soko Kuu, Wilaya ya Mbinga Jeshi la Polisi lilimkamata Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Kufuatia tuhuma zilizokuwa zinapelelezwa za kufanya uchochezi wa kutofanyika uchaguzi Mkuu 2025.

Mtuhumiwa huyo anahojiwa juu ya tuhuma hizo huko Dar-es- Salaam.

Jeshi la Polisi linatoa Onyo kwa vyama vyote vya siasa kutotoa maneno ya uchochezi, Kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na atakaye bainika kufanya hivyo atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na, Kamanda wa Polisi (M) wa Ruvuma
Hahaha jeshi la polis linatoa onyo kwa vyama vya siasa, na ccm ikiwemo?
 
Kweli kabisa, mimi simo, kama Lissu aliniona kwenye mikutano akajua ntakuwa tayari kuandamana kwa ajili yake alijidanganya.

Mimi niliienda tu baada ya kumaliza shughuli zangu za shamba, nikaona sina issue nyumbani. Mila zetu haziruhusu kutukanana.

Niache mpunga wangu uharibikie shamba nikagombane na mapolisi ambao hawajanikosea
 
Back
Top Bottom