Tetesi: Jeshi la Polisi Tanzania linawashikilia Maafisa wa Usalama kutoka Kenya

Tetesi: Jeshi la Polisi Tanzania linawashikilia Maafisa wa Usalama kutoka Kenya

Sio lazima uchangie, wewe soma post za wenzio utaelimika!!
Kwa elimu yako unayotoa kwa watu bora niende ngumbaru,kama wewe unajua na unaelimu jibu kwa maelezo.Mtu mjinga hukimbilia lawama na kejeli anapoulizwa swali ambalo kwa uhakika kabisa hana majibu yake.Ukiona mwalimu ameulizwa swali na mwanafunzi badala ya kujibu anakuwa mkali huyo ana vyeti feki.Nimeuliza je ukiwa na passport na ni usalama huruhusiwi kwenda nchi nyingine?utajulikanaje upo holiday au kazini katika ulimwengu huu wa sasa wa mitandao?Jibu swali usipayuke kama watu wa mataifa.
 
Propaganda za watu wa NASA hizo,

yaani watu 6 wa intelligence unawakamataje kama mbuzi,?

Wale wanakuwa na deepcover agents already inside ,kila ubalozi wa nchi huwa una kitengo cha intelligence,hawawezi kutuma mtu moja kwa moja toka nairobi badala ya kutumia watu wao walioko huku,
unless labda ilikuwa ni killteam,
kitu ambacho hakiwezekani kwani uhuru hana hiyo akili ya kummaliza odinga.
So kama ni surveillance tu ya kutaka kujua anakutana na nani na anafanya nini,hawawezi tuma lundo la watu tena directly kutoka nai
Nakubaliana na wewe 100%
 
Unaruhusiwa ila askari wana taratibu zao za clearance za kusafiri .Nchi husika hutakiwa kutaarifiwa kiofisi kuwa kuna askari anaingia kwao nk Kila askari kusafiri lazima katika masharti mmojawapo hutakiwa kuwa na kitu kinaitwa movement order ambayo huwa lazima aionyeshe mamlaka husika
Umenijibu vizuri mkuu.Haya ndiyo maelezo ninayotaka,unadhani kwa usalama wa taifa kama anamfuatilia mtu kama raila je hatakuwa na passport nyingine ya pili na ya tatu ya kawaida kucover up vitu kama hivyo vya movement order ili atimize haja zake za kiusalama?
 
Kwani hao deep covers agents toka ndani ya balozi huwa wanagundulika sometimes ndio maana hata nchi inaweza kumtimua afisa wa ubalozi, balozi mwenyewe au hata kuufunga ubalozi endapo Itabainika unajihusisha na shughuri za kajasusi.
CIA walitumia njia hizi kummaliza kwake Nkhuruma. Walipeleka watu kama mwambata wa jeshibkumbe walikua cia. Kazi yao kubwa ilikua kujifanya wanadiplomasia huku waki warubani baadhi ya viongozi katika serikali ya kwame. Kwame kustuka ilikua too late ikabidi akimbilie misri
 
Ujasusi siyo Interpol!
Duh taasis za kijasusi kushitikiana huyu jamaa anakijua anchokisema? Kasahau ya Snowden alipofichua mambo marekani na ujerumani walibidi wayamalize sababu CIA ilikua ina m wiretap Angela wa Ujerumani
 
Hujui kuwa taasisi za Kijasusi za nchi moja na nyingine, huweza kushirikiana katika baadhi ya mambo?
Usichanganye polisi na ujasusi. Wewe unazungumzia FBI Scotland yard MI5 hapa tunazungumzia CIA KGB MOUSAd na TISS
 
Ngoja wenyewe waje watoe majibu tujifunze zaidi na ingependeza zaidi
 
Hivi yule aliejifanya anauza madawa ya kienyeji anajifanya Mpare aliesomea Kenya,kazi yake ilikua vijiwe vya kawaha na vijiwe vya siasa Mnazi mmoja na pale chuo cha utumishi wa Umma barabara ya bibi titi mbona simuoni siku hizi?
 
Umenijibu vizuri mkuu.Haya ndiyo maelezo ninayotaka,unadhani kwa usalama wa taifa kama anamfuatilia mtu kama raila je hatakuwa na passport nyingine ya pili na ya tatu ya kawaida kucover up vitu kama hivyo vya movement order ili atimize haja zake za kiusalama?
It is OK but at owners risk .
 
Back
Top Bottom