πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ni noma
 
Wampe mafunzo yaishe, hata waliochanga hawakujua ni kosa.

Sasa ziwekwe pembeni, naamini mfuko wa serikalini wengi wanasema ndio wanaogopa kuchangia. Labda wasaka connections na kiki
Kwasababu anamdomo sana akionywa kwa maneno haitatosha achunguzwe chanzo cha mapato yake, ni muda gani kafanya biashara, record zake za kulipa kodi TRA zichunguzwe ikionekana kodi anayolipa haina uwiano na biashara zake afunguliwe kesi ya kukwepa kodi, liunganishwe na kosa la kukusanya fedha kwa jamii bila kufata sheria na afunguliwe kesi ya utakatishaji fedha akihangaika na hiyo kesi isiyo na dhamana hata akitoka itakua ni onyo zuri
 
Haya ndiyo ma umbwa kama yale yanayozunguka majalalani. Alichofanya Niffer ni kama wale vijana waliojitolea kuokoa maisha ya watanzania wakati serikali nzima imelala usingizi mzito
 
Serikali Yako Ina uwezo Gani kama mpaka Leo Kuna watu wamekwama kwenye kifusi?
Majanga yanatokea popote hata ingekua marekani acha ushamba wewe. Kwani serikali ndio ilimwambia huyo mwenye nyumba agonge gonge huko chini mpaka hilo jumba lidondoke? Mengine mnayasababisha wenyewe kwa tamaa zenu na ujuajii likitokea janga lawama kwa Serikali pumbavu sana.
 
πŸ™‹β€β™‚οΈπŸ‘πŸ‘πŸŽ―πŸ€πŸ™
 
Ila sio mbaya mashabiki wake wa huko social networks wanadai yupo vizuri kimkwanja ana range lenye plate namba ya jina lake cha msingi hasiwaangushe MASHABIKI wake wa huko mitandaoni. Baada ya hapa watajifunza reality na maigizo mitandaoni.
 
Jennifer ni mfanyabiashara wa kkoo?
Huo umoja ndo wanachangashina kwenye lipa namba ya biashara ya mtu?
Tumia akili kidogo basi
 
Katika information theory kuna somo moja kubwa sana.

Ulimwengu hautaki ombwe. Nature abhors a vacuum.

Kukiwa na ombwe, ulimwengu utaliziba.

Kukiwa hakuna habari ya ukweli, hata uongo utatokea tu kuziba ombwe la habari.

Kukiwa na ombwe la uongozi kutoka kwenye vyombo vya uongozi rasmi, watajitokeza watu ambao si viongozi rasmi kujiungaunga na kuongoza hivyohivyo kienyejienyeji.

Ndiyo maana unaona hatukuwa na juhudi za kueleweka za uokoaji kutoka wa waokoaji rasmi, lakini hilo halimaanishi kwamba hawakujitokeza watu wa kawaida tu kuokoa.

Vivyo hivyo, kutoonekana kwa vyombo rasmi kama Ofisi ya Waziri Mkuu au Tanzania Red Cross kuongoza michango, kumeacha ombwe la uongozi ambalo watu kama Niffer wanalijaza kwa kuongozana kienyeji.

Badala ya kumlaumu Niffer, mtu ambaye anaonekana hajui mengi kuhusu sheria wala itifaki za mambo haya, lakini anaonesha nia ya kuongoza harakati za uchangishaji, kwa nini vyombo rasmi kama Tanzania Red Cross au Prime Minister's Office vimechelewa kuanzisha michango?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…