Katika information theory kuna somo moja kubwa sana.
Ulimwengu hautaki ombwe. Nature abhors a vacuum.
Kukiwa na ombwe, ulimwengu utaliziba.
Kukiwa hakuna habari ya ukweli, hata uongo utatokea tu kuziba ombwe la habari.
Kukiwa na ombwe la uongozi kutoka kwenye vyombo vya uongozi rasmi, watajitokeza watu ambao si viongozi rasmi kujiungaunga na kuongoza hivyohivyo kienyejienyeji.
Ndiyo maana unaona hatukuwa na juhudi za kueleweka za uokoaji kutoka wa waokoaji rasmi, lakini hilo halimaanishi kwamba hawakujitokeza watu wa kawaida tu kuokoa.
Vivyo hivyo, kutoonekana kwa vyombo rasmi kama Ofisi ya Waziri Mkuu au Tanzania Red Cross kuongoza michango, kumeacha ombwe la uongozi ambalo watu kama Niffer wanalijaza kwa kuongozana kienyeji.
Badala ya kumlaumu Niffer, mtu ambaye anaonekana hajui mengi kuhusu sheria wala itifaki za mambo haya, lakini anaonesha nia ya kuongoza harakati za uchangishaji, kwa nini vyombo rasmi kama Tanzania Red Cross au Prime Minister's Office vimechelewa kuanzisha michango?