Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
Hawa wadada wa mjini ukiwafuatilia kuna vitu vingine gizani wanafanya ambavyo vinawapa pesa, hivyo vipodozi ni zuga tu, si unakumbuka kuna yule mwingine alikuwa anawaambia wenzake ana kibubu kila siku anaweka milioni moja kama akiba, leo yupo jela maisha kwa ngada
😂😂😂😂😂😂😂 Ni noma
 
Wampe mafunzo yaishe, hata waliochanga hawakujua ni kosa.

Sasa ziwekwe pembeni, naamini mfuko wa serikalini wengi wanasema ndio wanaogopa kuchangia. Labda wasaka connections na kiki
Kwasababu anamdomo sana akionywa kwa maneno haitatosha achunguzwe chanzo cha mapato yake, ni muda gani kafanya biashara, record zake za kulipa kodi TRA zichunguzwe ikionekana kodi anayolipa haina uwiano na biashara zake afunguliwe kesi ya kukwepa kodi, liunganishwe na kosa la kukusanya fedha kwa jamii bila kufata sheria na afunguliwe kesi ya utakatishaji fedha akihangaika na hiyo kesi isiyo na dhamana hata akitoka itakua ni onyo zuri
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema hakuna mtu yeyote ambaye anaruhusiwa kuchangisha fedha kufuatia tukio la ajali ya kupomoka kwa grorofa la Kariakoo.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kuzungumza katika eneo hilo akasema JENIFER JOVIN maarufu Niffer atafutwe ili aeleze nani ambaye alimpa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia tukio hilo kwa sababu Serikali ina utaribu wake katika mafaa kama haya.

Pia, Soma: Maafa Kariakoo: Usichangishe fedha tumia akaunti ya Serikali

Aidha baada ya agizo hilo majibu yakatolewa eneo la Kariakoo wakati Waziri Mkuu anazungumza kwamba Mfanyabiashara Niffer ameshapatikana.
Haya ndiyo ma umbwa kama yale yanayozunguka majalalani. Alichofanya Niffer ni kama wale vijana waliojitolea kuokoa maisha ya watanzania wakati serikali nzima imelala usingizi mzito
 
Kumbe sio kosa kuchangisha kosa ni kuto declare
 

Attachments

  • IMG-20241118-WA0040.jpg
    IMG-20241118-WA0040.jpg
    57.8 KB · Views: 1
Serikali Yako Ina uwezo Gani kama mpaka Leo Kuna watu wamekwama kwenye kifusi?
Majanga yanatokea popote hata ingekua marekani acha ushamba wewe. Kwani serikali ndio ilimwambia huyo mwenye nyumba agonge gonge huko chini mpaka hilo jumba lidondoke? Mengine mnayasababisha wenyewe kwa tamaa zenu na ujuajii likitokea janga lawama kwa Serikali pumbavu sana.
 
Asome pamoja na sheria ya Maafa ambayo inasema siyo kosa kuchangisha kosa ni kutozipeleka fedha kwa kamati ya maafa. Swali ni je mchangishaji alikuwa amefika mwisho wa kuchangisha? Je, kuna dalili kwamba hakuwa tayari kuziwasilisha katika kamati hiyo?
🙋‍♂️👍👏🎯🤝🙏
 
Ila sio mbaya mashabiki wake wa huko social networks wanadai yupo vizuri kimkwanja ana range lenye plate namba ya jina lake cha msingi hasiwaangushe MASHABIKI wake wa huko mitandaoni. Baada ya hapa watajifunza reality na maigizo mitandaoni.
 
Kama wana umoja wao hao wafanyabiashara wa kkoo wasijichangishe?

Kwani serikali si kila bajeti huwa wanatenga fungu kwa ajili ya mfuko wa maafa sasa wanachangisha nini tena hela zilizotengwa ziko wapi mpk waanze kuwaonea wivu wengine wanaochangisha?

Mambo mengine ni aibu sana hasa yanapotendwa na kiongozi mkubwa hivyo
Jennifer ni mfanyabiashara wa kkoo?
Huo umoja ndo wanachangashina kwenye lipa namba ya biashara ya mtu?
Tumia akili kidogo basi
 
Katika information theory kuna somo moja kubwa sana.

Ulimwengu hautaki ombwe. Nature abhors a vacuum.

Kukiwa na ombwe, ulimwengu utaliziba.

Kukiwa hakuna habari ya ukweli, hata uongo utatokea tu kuziba ombwe la habari.

Kukiwa na ombwe la uongozi kutoka kwenye vyombo vya uongozi rasmi, watajitokeza watu ambao si viongozi rasmi kujiungaunga na kuongoza hivyohivyo kienyejienyeji.

Ndiyo maana unaona hatukuwa na juhudi za kueleweka za uokoaji kutoka wa waokoaji rasmi, lakini hilo halimaanishi kwamba hawakujitokeza watu wa kawaida tu kuokoa.

Vivyo hivyo, kutoonekana kwa vyombo rasmi kama Ofisi ya Waziri Mkuu au Tanzania Red Cross kuongoza michango, kumeacha ombwe la uongozi ambalo watu kama Niffer wanalijaza kwa kuongozana kienyeji.

Badala ya kumlaumu Niffer, mtu ambaye anaonekana hajui mengi kuhusu sheria wala itifaki za mambo haya, lakini anaonesha nia ya kuongoza harakati za uchangishaji, kwa nini vyombo rasmi kama Tanzania Red Cross au Prime Minister's Office vimechelewa kuanzisha michango?
 
Back
Top Bottom