Jeshi la Polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo
Viherehere kwenye mitandao sio kitu kizuri.

Hata hivyo hatua zimechelewa kuchukuliwa. Sijui jeshi letu ni wazee sana wamejazana huko hadi wanashindwa ku ‘catch up’ na mambo ya kwenye mitandao upesi?

Mtu ameshakusanya mamilioni ya pesa tokea jana na alitangaza kila hatua wao walikuwa wapi?
Pm ana jaribu kufanya spining. Yeye ni kiongozi wa waokoaji. Ajikite kwenye kuokoa maisha ya watu hayo mambo ya michango waachiwe polisi! Kwani yanaibiwa mabilion mangapi huko serikalini? Mbona hawahamaki na kuchukia hatua????
 
Ujue serikali hii, unaona kabisa kuna watu ni zero brain, mtu akitumia umaarufu wake kuraise michango kuna shida gani, mie huyo niffer simjui, lakini mfano kama mwakinyo, akiraise michango kuna watu watapata msukumo sababu ya mwakinyo, kuna fans wa Diamond, simba sc ama yanga sc wakianzisha kuna watu watavutika kuchanga sababu ya simba ama yanga.

Huenda kukawa kuna kaupigaji kweli, mie sikatai mjini kila mtu anaweza tumia matatizo kama fursa, lakini jinsi walivyochukua hatua sio vizuri, kesho kutwa litatokea janga, mtu maarufu akaogopa kulivalia njuga.
Kati ya huyo binti niffer na serikali nani wa kwanza kuweka utaratibu wa kuchangia.
Kama ni huyo binti serikali ilikuwa wapi kutoa muongozo?
 
Hakutakuwa na kesi ataachiwa ila itakuwa funzo mambo ya serikali achia serikali hii sio tabia nzuri kuchangisha katika masuala ya kitaifa lazima kuwe na muongozo, wewe changisha harusi au msiba ya mitaani hata huko wanaweka utaratibu sio kila mtu anakusanya. Hii inazuia watu wenye nia ovu kuiba pesa. Hapa itabidi tu ahamishe kila cent iliyochangishwa kwenye mfuko wa serikali au zirudishwe zilikotoka.
Atulize komwe asijibizane na mtu huko social media.
Mihemko itamponza
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kumkamata mfanyabiashara maarufu nchini Niffer kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kuchangisha michango ya maafa ya Kariakoo kinyume na taratibu

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo, Jumatatu Novemba 18.2024 baada ya kufanya ukaguzi wa hatua iliyofikiwa kwenye zoezi la uokoaji linaloendelea kwenye jengo la ghorofa lililoporomoka kwenye soko la kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam

Majaliwa amesema Niffer amekuwa akitumia mitandao yake ya kijamii kuchangisha michango kinyume na taratibu, hivyo kuagiza Jeshi la Polisi limkamate mfanyabiashara huyo na kisha kumuhoji ni wapi amepata kibali cha kuchangisha fedha hizo

Sambamba na hilo ameagiza account zake alizokuwa anatumia kuendesha makusanyo hayo zote zifungwe haraka iwezekanavyo, katika hilo Majaliwa amesema amemsikia Niffer akisema amekusanya milioni 30+ na kwamba anasema amenunua maziwa kwa ajili ya Kariakoo jambo ambalo pia ametaka ahojiwe

Baada ya kutoa agizo hilo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila alimueleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa mtu huyo tayari ameshakamatwa

Katika hatua nyingine, Majaliwa ameagiza mmiliki wa jengo la ghorofa Kariakoo lililoporomoka na kuleta maafa atafutwe na vyombo vya dola haraka iwezekanavyo
20241118_144919.jpg
 
Viherehere kwenye mitandao sio kitu kizuri.

Hata hivyo hatua zimechelewa kuchukuliwa. Sijui jeshi letu ni wazee sana wamejazana huko hadi wanashindwa ku ‘catch up’ na mambo ya kwenye mitandao upesi?

Mtu ameshakusanya mamilioni ya pesa tokea jana na alitangaza kila hatua wao walikuwa wapi?
Kinachouma zile pesa najua hazitawafikia walengwa pindi zikiingizwa kwenye mikono ya wachumia tumboo
Watu wametoa kwa moyo ila sasa zitatafunwa mnooo na watu wa hovyooo
 
Viherehere kwenye mitandao sio kitu kizuri.

Hata hivyo hatua zimechelewa kuchukuliwa. Sijui jeshi letu ni wazee sana wamejazana huko hadi wanashindwa ku ‘catch up’ na mambo ya kwenye mitandao upesi?

Mtu ameshakusanya mamilioni ya pesa tokea jana na alitangaza kila hatua wao walikuwa wapi?
Kama unahisi Kuna jeshi pole sana kile ni kikundi Cha wahuni waliojificha kwenye kichaka Cha uniform.
 
Ok wakuu, tuwe serious, tuache mihemko na ushamba

Tukihararisha namna hii ya ufanyaji kazi matapeli wengi watatumia njia hii kujipatia pesa kwa majanga yetu.

Tuseme hapo mtaani kumetokea janga ghafla boda boda mmoja maarufu hapo mtaani anaanza kuchangisha pesa kwa ajili ya waliokubwa na tabu hio.

Kama wewe ni timamu lazima uone process anayofanya haipo katika mpangilip ulio na utaratibu na uratibu.

Hata kama ni kwa nia njema anafanya , una uhakika ataleta kweli hizo milioni 10 alizochangisha au kuna mbili atapitanazo.
 
Hakutakuwa na kesi ataachiwa ila itakuwa funzo mambo ya serikali achia serikali hii sio tabia nzuri kuchangisha katika masuala ya kitaifa lazima kuwe na muongozo, wewe changisha harusi au msiba ya mitaani hata huko wanaweka utaratibu sio kila mtu anakusanya. Hii inazuia watu wenye nia ovu kuiba pesa. Hapa itabidi tu ahamishe kila cent iliyochangishwa kwenye mfuko wa serikali au zirudishwe zilikotoka.
Na huko ndo zinaenda kuliwa sasa
 
Hii nchi inahitaji kuboresha juhudi za uokoaji baada ya changamoto zilizojitokeza. Serikali inapaswa kuwa makini zaidi na kuacha kuelekeza lawama zisizohitajika kwa wengine kama Niffer, ambaye hajahusika moja kwa moja.

Badala ya kuzingatia juhudi za mtu binafsi, ni muhimu kwa viongozi kuonyesha uwajibikaji wa kweli na kuhakikisha rasilimali zinatumiwa kwa manufaa ya wananchi. Kumbukeni, wananchi wanahitaji kuona matendo halisi, si maneno matupu.

Wakati wa majanga kama tetemeko la Bukoba na sasa ajali ya Kariakoo, imani ya wananchi kwa serikali hupimwa kwa vitendo. Ni muhimu kurejesha imani hiyo kwa uwazi na hatua madhubuti, badala ya kuunda kamati ambazo hazileti matokeo yanayoonekana.
 
Back
Top Bottom