ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 16,871
- 39,881
Kuna habari zinaenea kuwa Jeshi la polisi liliwakamata, kuwatesa na baadaye kuwasafirisha Kwa njia ya barabara na kuwatekelekeza mipakani mwa nchi zao.
Inasemekana Mwanaharakati wa Uganda aliteteswa na kutelekezwa mpakani km 30 kutoka border ya Mtukula pia Boniface Mwangi wa Kenya alitelekezwa kwenye km 100 kutoka mpaka wa Holoholo.
Binafsi hainiingii akili kama jeshi la polisi lilishindwa kuwafungulia mashitaka Kwa makosa Yao ya wazi ya kutoa taarifa za uongo kipindi wanaingia Tanzania.
Pia hainiingii akili kama police wa Tanzania anaweza kuvuka border za nchi jirani na kusafiri km kadhaa na kumtelekeza raia wa nchi hiyo.
Natamani polisi watoke hadharani watupe picha halisi ya matukio haya na walichukua hatua gani dhidi ya wahalifu hao.
Nina uhakika Kwa hili Jeshi la polisi na Vyombo vya usalama vinachafuliwa maksudi.
Tanzania kwanza.
I love Tanzania.