Jeshi la Polisi: Tumemkamata Boniface Jacob kwa makosa ya Jinai anayotuhumiwa nayo

Jeshi la Polisi: Tumemkamata Boniface Jacob kwa makosa ya Jinai anayotuhumiwa nayo

Hujielewi wewe kiande! Unajiroposha tu humu sijui unanufaikaje! Tangu lini jinai ikawa mauaji? Hivi ni vitu viwili tofauti mbele ya Sheria, sijui unanielewa? Punguza ujuaji!
Una kunywa mbege ukiwa wapi mke wa x Mayor

USSR
 
View attachment 3099730
Jeshi la Polisi limemkamata na lina mshikilia Boniface Jacob mkazi wa Mbezi kwa Msakuzi Jijini Dar es Salaam kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo.

Hivyo, wananchi wapuuze uwongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa.

Imetolewa na:
David A. Misime - DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania.

Pia soma: Boniface Jacob adaiwa kukamatwa na watu waliokuja na gari aina ya defender. Kamanda Kitwinkwi asema hana taarifa hizo
Safi sana, wazushi hawatakosa kuzusha lingine.
 
Naona sasa akili zime anza kuwarudia.
Inge kuwa juzi wange sema hako nae.
Ila jinsi walivyo mkamata hadi kumchania nguo bado sio taratibu za ukamataji
Inategemea na resistance yake kama alikataa kutii amri polisi wameruhusiwa kutumia nguvu yenye uwiano sana na ya mtuhumiwa
 
WANATAKA KUJIVUA UHUSIKA WA UTEKAJI KWA MBINU YA KUWAKAMATA SASA NA KUSEMA TUMEWAKAMATA!
Uko sahihi kabisa, hii kamata kamata lengo lake ni kutaka kulisafisha jeshi la polisi na huu utekaji na mauaji ya wapinzani wanayoyafanya.
 
Sasa ukamanda wa mitandaoni
Wewe hapa haupo mtandaoni?

Onyesha hapa huo uongo na hao unaowasema nimewadanganya.
unawadanganya wenzako kumbe wewe uko kwa mabeberu. Sasa wameanza kushughulikiwa kama alivyosema Rais
Beberu ni nani?
IMG-20240715-WA0000.jpg


Huyu huyu anayewajengea hadi choo?

Kama huwezi kujenga choo na bado mtu anayekujengea unamuita beberu sasa hapa nani ni beberu halisi?

Na bado safari za ndege za kutosha na misafara mirefu ya kuomba msaada je beberu anaweza kukupa msaada binadamu au binadamu ndio anamsaidia beberu?
 
Inategemea na resistance yake kama alikataa kutii amri polisi wameruhusiwa kutumia nguvu yenye uwiano sana na ya mtuhumiwa

Ukamataji wa kishamba, walitakiwa kumpatia wito afike Polisi kisha taratibu zingine zifuate.

Kumvamia mtu njiani kama vile ni jambazi sugu hatari muuaji aliyekuwa anakwepa mitego ya polisi mara kadhaa kumkamata kwa staili hii ni njia isiyo sahihi.

Wakili msomi Hekima Mwasipu asimulia jambo zima lilivyotokea, taharuki mtaani iliyoendana na kurupushani kubwa ... kituo Oysterbay kwa RCO wataelejea Msakuzi makaazi ya Bonuface Jacob kufanya upekuzi ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=TPyNi-GCCpA
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hivi ndio Taarifa ya Jeshi letu la polisiView attachment 3099758
Watekani walienda kumteka, ila baada ya zogo ikabidi waseme wamemkamata. Na hawana maelezo ya kwanini wamemkamata, lakini watatengeneza makosa akiwa humo humo sero. Ila sababu hasa ya kukamatwa ni kutokana na kumtaja kiongozi wa watekaji afande Mafwele.
 
Ukamataji wa kishamba, walitakiwa kumpatia wito afike Polisi kisha taratibu zingine zifuate.

Kumvamia mtu njiani kama vile ni jambazi sugu hatari muuaji aliyekuwa anakwepa mitego ya polisi mara kadhaa kumkamata kwa staili hii ni njia isiyo sahihi.

Wakili asimulia jambo zima lilivyotokea


View: https://m.youtube.com/watch?v=TPyNi-GCCpA

Siyo kila muhalifu anapewa wito kunawahalifu wanakamatwa bila wito ili wasiharibu ushahidi, we unaweza kumpa wito mtu alieficha bangi nyumbani kwake na utegemee utamkuta na hatia? Si ataficha ushahidi
 
Siyo kila muhalifu anapewa wito ukimpa kunawahalifu wanakamatwa bila wito ili wasiharibu ushahidi, we unaweza kumpa wito mtu alieficha bangi nyumbani kwake na utegemee utamkuta na hatia? Si ataficha ushahidi

Hizo ni drama za Polisi tu, kuna namna za kikachero kufanikisha yote hayo bila kurupushani za aina hizo.
 
Back
Top Bottom