Zanzibar 2020 Jeshi la Polisi Zanzibar limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani

Zanzibar 2020 Jeshi la Polisi Zanzibar limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani

Rais gani amefungwa huko
Jipendeleeni kujidanganya!!
Pumbavu.Kwa hiyo Polisi iwashangilie na kuwasindikiza waende zao nyumbani.Hatutaki ujinga huo.
ndiyo nakwambia hivi police isipotumia busara hapa mambo yanakwenda kubwa mabaya zaidi, Police yoyote duniani haiwezi kupambana na wananchi wake!! ikashinda...

Kinachoshinda huwa ni busara tu toka kwa Police.
 
USA Kwanini alijitoa kwenye hiyo mahakama ?

Jipendeleeni kujidanganya!!
ndiyo nakwambia hivi police isipotumia busara hapa mambo yanakwenda kubwa mabaya zaidi, Police yoyote duniani haiwezi kupambana na wananchi wake!! ikashinda...

Kinachoshinda huwa ni busara tu toka kwa Police.
 
Unguja. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar limesema limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Limesema waliokamatwa ni waliochoma matairi na kuyaweka katikati ya barabara na waliokwenda katika vituo vya kupigia kura wakati leo wanaoruhusiwa kupiga kura ni makundi maalum wakiwemo askari wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na kuyashambulia kwa mawe magari ya polisi.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Oktoba 27, 2020 na Kamanda Polisi wa Mkoa huo, Awadh Juma Haji wakati akizungumza na Mwananchi Digital.

Amesema mbali ya matumizi ya mabomu hayo, wanawashikilia baadhi ya vijana waliodai kuhusika katika matukio hayo.

Amebainisha kuwa vijana hao wanatuhumiwa kuchoma moto matairi ya magari na kuyaweka katikati ya barabara na maeneo mbalimbali kinyume na sheria, kuyashambulia kwa mawe magari ya askari polisi waliokuwa katika doria huku wakijua kuwa kazi ya polisi ni kusimamia amani na utulivu.
Dawa yake ni kukinukisha hadi maccm yote yafilie mbali hukooooo peponi
 
Watuambie maiti zinazoonekana kwenye mitandao ya kijamii nani amewaua wale watu?

Mnachukua muda mrefu kutoa majibu halafu mnakuja na taarifa laini isiyojitosheleza.
Ndugu yako amekufa au?
 
Jeshi haliwezi kushindana na wananchi wake likawashinda...kinachotakiwa hapo ni busara tu.
Inategemea ni wananchi wepi, walio timamu au wendawazimu wanaochoma matairi barabarani. Wendawazimu wanaoharibu mali za umma kwa hasira binafsi wanaweza dhibitiwa hata na mgambo wa kijiji.
 
..Polisi walitakiwa wasitishe kura ya mapema.

..Vifo vilivyotokea chanzo chake ni kura ya mapema.

..Kwanini Polisi waliruhusu kura ya mapema iendelee wakielewa kabisa kwamba kulikuwa na "viashiria" vya kuvunja amani?
Uchaguzi usitishwe kwa kuwa kuna wendawazimu hawawezi kutulia nyumbani wasipokuwa na kazi ya kufanya! Watu kama hao ni kuwashughulikia tu mpaka washike adabu.
 
Nasikia mtwara imevamiwa na alishababu vipi polisi wetu watakwenda na huko ?
Hivyo umefurahi siyo! Upinzani wa nchi hii wa hovyo kabisa. Raia anafurahia nchi yake kushambuliwa. Hivi huwa mnapewa viroba vya wapi nyie watu.
 
Wewe ndo ungekuwa polisi alafu vijana wanakulushia mawe, wakati huo wanaharibu magari kwa mawe ungetumia busara gani zaidi ya kuwadhibiti? [emoji848]

Ikiwa jeshi haliwezi kuwashinda wananchi wake kama usemavyo, Basi msilalamike huku mitandaoni, nendeni mkapambane nao.
Hawa keyboard warriors wa huku mitandaoni hamna kitu kabisa. Hata mawe hawawezi kuokota. Maneno matupu tu.
 
..inawezekana mambo yako vizuri kwenye vitabu vya sheria, ila unapoingia field na kuanza kuitekeleza sheria matokeo yake ndiyo hivyo vifo na vilema kwa wananchi.

..wahusika wangekuwa na busara, na wangekuwa wanayathamini maisha ya Watanzania, naamini wangeachana na zoezi la kura ya mapema.
Kuna vifo na vilema vya kujitakia. Unajua kura ya leo haikuhusu wewe unaiparamia.
 
Pumbavu.Kwa hiyo Polisi iwashangilie na kuwasindikiza waende zao nyumbani.Hatutaki ujinga huo.
Wanataka polisi kutumia busara ambayo wao wenyewe hawana na hawako tayari kuwa nayo.
 
Jeshi haliwezi kushindana na wananchi wake likawashinda...kinachotakiwa hapo ni busara tu.
Mbona limewashinda?
Pia ieleweke JESHI halijashindana na wananchi limeshindana na wahalifu.
 
MAALIM SEIF AACHIWA HURU SPANA ZA JINO KWA JINO ZIKO PALEPALE

 
Back
Top Bottom