Mkuu. "with all due respect" usiwe kama mtu ambae hatumii akili.
Yaani wanajeshi hawapaswi kuonekana hata kwenye vilabu vya pombe kusaka na kugombea wanawake (wenyewe huita wavila), upumbavu mtupu.
Jeshi shughuli zake zote ni makambini na hawapaswi kuwa mitaani mpaka pale hali ya dharura inapotangazwa.
Dharura hiyo ni maafa, uasi na vurugu ambazo ni jeshi la polisi huomba msaada.
Na ni serikali ndo hutoa mari kupitia waziri wa ulinzi kutuma wanajeshi kushika sehemu muhimu.
Tusijitwishe ujuaji uso na manufaa yoyote.
Wewe ndo hutumii akili kwa sababu hujui majukumu ya jeshi. Mmekariri vita tu. Ha ha ha! Ingekuwa jeshi linasubiri vita kwanini mabalozi wengi duniani ni wanajeshi.
Kwa nini maofisa wengi balozini ni wanajeshi. Si wangekaa kambini kusubiri vita kama unavyomaanisha.
Kwanini kamati za usalama za nchi nyingi hata hapa Tanzania kamati za usalama zinajumuisha wanajeshi, anzia wilayani, mkoa hadi Taifa. Unajua vikao vya ulinzi na usalama vinajadili maswala gani?
Ati serikali! Unajua hiyo serikali inavyoendeshwa? Unajua mambo yote unayoyaona kuanzia kijinini kwenu, wilayani, mkoani hadi Taifa jeshi wanahusikaje?
Kwa taarifa yako humu duniani serikali zote zinategemea jeshi. Si maswala tu ya vita hata na mengineyo.
Kagame, na ethiopia wanaongoza kwa kuwa na wanajeshi wengi nje hawako kivita wapo kwa kazi maalum. Marekani, Uingereza, Ufaransa, na nchi zinginezo wanajeshi ndo maintellijensia wa uchumi. Jeshi linakazi zaidi ya vita.
Tafakari ndugu yangu. Unajua mambo unayoyaona nje ni tofauti na inavyokuwa ndani.
Mfano tu wakati Rais Magufuli amefariki kulitokea matafaruku nani ashike nchi, kuna baadhi ya viongozi waliosema Makamu wakati huo Samia hawezi. Ili liko wazi. Mama Samia alilisema na Mkuu wa Majeshi wakati huo aligusia kidogo.
Ni Mkuu wa majeshi ndo alie toa msimamo kuwa katiba ifuate wote wakaufyata! Kwanini Mkuu wa jeshi aliingia katika kikao cha serikali si angekuwa kambini kwa msemo wako.
Narudia jeshi si vita tu!