Jeshi siyo chama cha Siasa hadi utamani cheo cha Bosi wako mkuu. Hata kwenye Siasa tuliyaona yaliyomkuta Zitto alipotamani cheo cha Mwenyekiti

Jeshi siyo chama cha Siasa hadi utamani cheo cha Bosi wako mkuu. Hata kwenye Siasa tuliyaona yaliyomkuta Zitto alipotamani cheo cha Mwenyekiti

Tukiwa JKT kwa mujibu wa sheria tulifundishwa mambo mengi yakiwemo Uvumilivu, Nidhamu na Utii.

Ukiwa jeshini unatakiwa utumikie nafasi uliyopo kwa weledi na uzalendo uliotukuka na kuwatii Viongozi wako pamoja na kuwaheshimu walio chini yako.

Jeshini hutakiwi kutamani nafasi ya mtu bali juhudi zako zitaonekana na mamlaka kama kweli unastahili

Tusichanganye kabisa mambo ya Jeshi na Siasa.

Maendeleo hayana vyama!

Pia, soma=> RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

Hata kwenye siasa mambo hayaendi hivyo. Ukitamani kiti cha Ayatollah Mbowe, kwa mfano, lazima utaliwa kichwa!

Wahanga wake tumewaona wengi.
 
Hata huku kwenye chama chetu cha upingaji Sumaye alipotaka kugombea uenyekiti aliambiwa 'sumu haionjwi kwa ulimi', akaufyata!

Polisi sio chama kama unajiamini kazi yako na kuomba cheo sioni ubaya wowote.

Ushindani sio kitu kibaya. Hasa Polisi wenzetu nchi nyingine Polisi ni jeshi la Raia kweli na wakuu wa Polisi wa maeneo yao wanateuliwa na meya na sio Raisi.

System ya IGP kwa jeshi wa wananchi ni mfumo wa kikoloni hata kwao hawana huu utaratibu .

Waliweka huu utaratibu kusaidia kukandamiza watu
 
Ukiwa jeshini unatakiwa utumikie nafasi uliyopo kwa weledi na uzalendo uliotukuka na kuwatii Viongozi wako pamoja na kuwaheshimu walio chini yako.
Kama mtu amepikwa kimchongo na kupewa vyeo kimchongo usishangae kesho anakugeuka kukudhuru uliyemchonga
 
Ni heri kumkosoa amiri jeshi mkuu kuliko kumkosoa mwenyekiti wa chama.

Zito, Chacha Wangwe na wengine yaliwakuta makubwa huko kwa mwenyekiti baada ya kujaribu kutaka kurudisha demokrasia ya kweli ndani ya chama.
Sawa MM1
 
Back
Top Bottom