Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 19,637
- 29,473
- Thread starter
- #61
AmelogwaJamaa anampenda huyu mwanamke kiasi kwamba alimpa taraka mkewe wa awali na kutelekeza watoto wao wawili wa kike baada ya kukutana huyu mrembo. mrembo akamwambia kama akiendelea kuwa na mapenzi naye yale yale kwa miaka kumi basi ndipo atamuoa.
Mnyamwezi akaendelea kuonyesha mapenzi kiasi kwamba kuna kipindi bidada alikuwa na madeni makubwa, jet li akasaini mkataba wa kucheza filamu sita na pesa itakayopatikana iende kulipia madeni ya huyu binti na kumbuka wakati huo hawajaoana ndicho kipindi cha hiyo miaka kumi ya demu kumwangalia jamaa kama ana mapenzi yale yale.
Unajua kwanini jet li movie zake nyingi alikuwa haonyeshi mahaba kwa wanawake? katika kipindi cha hiyo miaka kumi, kuna movie alicheza akiwa ana mpenzi. Baada ya hiyo movie kutoka fununu zikaanza kudai kuwa jet li anatoka na huyo actress. Huyo binti akakasirika na kutaka kuvunja mahusiano yao ambapo jet li alijitetea na kumbembeleza sana. Basi toka wakati huo Jet Li akawa kwenye mikataba yake inahusisha kipengele cha kutokuwa na scenes za mapenzi yaliyopitiliza na binti anayecheza naye.
Jamaa haambiwi kitu kwa huyo mwanamke.
Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app