TIMU ya Simba imemaliza kibabe mzunguko wa kwanza Ligi Kuu baada ya kuichapa Coastal Union mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani ikifikisha pointi 34.
Mabao mawili ya Moses Phiri dakika ya 53, 61 na moja la Clatous Chama dakika ya 89 yametosha kuihakikishia Simba ushindi huo mbele ya Wagosi Wakaya.
Simba imependa kileleni mwa msimamo wa ligi ikifikisha pointi 34 baada ya michezo 15, miwili zaidi ya Yanga yenye 32.
Wagosi wa Kaya wameendelea kusalia nafasi ya 13 kwenye msimamo ikiwa na pointi 12 baada ya mechi 14.
Simba ililazimika kucheza pungufu baada ya kiungo wake Sadio Kanoute kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Coastal.
FT: Coastal Union 0-3 Simba
[emoji460]️' Chama
[emoji460]️[emoji460]️' Phiri.