JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

BTW msingi wa kuitwa daladala ulikuwa hivi: Shillingi tano za Kitanzania zilikuwa sawa na dola moja ya marekani na pound sterling 1 wakati huo tulikuwa tunabadili kwa shillingi 7 (saba). Hivyo mabasi hayo kuitwa daladala.
Sio sahihi usemacho, ngoja tumalize la Sokoine tukufahamishe chimbuko la daladala ambalo lilianzia Sumni sumni (yaani senti hamsini)
 
Food for thought. ITV walikuwa wakirusha hotuba za Nyerere kila mara (wosia wa baba). Lakini inashangaza kuwa nadra sana kukuta TBC wakifanya hivyo.

Hitimisho langu ni kuwa marais waliofuatia baada ya Nyerere kwa kiasi kikubwa hawajawa muafaka (comfortable) na urithi (legacy) wake. Wanautumia kujiinua kisiasa tu lakini hawautaki. They are averse to politics of poverty. None of them would follow Nyerere’s course to the letter. Naamini ndio sababu wanadhibiti sana TBC kurusha footage kamili za Mwalimu isipokuwa kutumia clips zake zinazowainua katika propaganda materials zao.
 
Nadhani haukuwa mjini zama hizo.....Joka Kuu yuko sahihi kwa 80%
 


Nakumbuka miezi ya kwanza kwanza 1984 kabla ya kifo chake nikiwa kijana mbichi baada ya kumaliza chuo na kuajiriwa wizarani (siitaji) muda mfupi kisha kuhamishiwa Singida na mkuu wa mkoa akiwa Kapteni Kafanabo ndio nilipojua kuwa Sokoine alikuwa kiongozi ambaye aliogopeka na sio wa mchezo mchezo.
Usiku mmoja Sokoine alimpigia simu Kapteni Kafanabo (RC) kumtaka taarifa ya hali ya chakula mkoani hapo, na kwa vile taarifa za kina hakuwa nazo alimuamuru kesho yake SAA 10 jioni aziwasilishe ofisini kwake Dar. Kumbuka enzi hizo barabara SGD to Dodoma haikuwa na lami na mbovu mno.
RC akawasiliana na RDD wake naye akamwambia ni mpaka asubuhi taarifa zitapatikana toka kwa maafisa mipango.
Kwa kukosa usingizi RC SAA 12 yuko ofisini na SAA 12.30 watumishi hatujafika maana SAA ya kazi ni 1.30 basi RC kichaa kikapanda "mbona watu wanachelewa hivi kazini? Nitafunga geti na wote nifukuze"!nk nk, hadi alipofika RDD na kumwambia atulie SAA za kazi bado ( na hakukuwa na mobile phone).
Jinsi alivyo hangaika Kapteni wa jeshi Kafanabo kwa woga wa amri za Sokoine sijasahau mpaka Leo.
Hakumuwahi PM hiyo SAA 10 licha ya kuwa na Range rover (gari la RC) kwani walipata ajali isiyo na human injury kati ya Dodoma na Moro ila sikumbuki eneo gani.
Sokoine hakutoa maagizo ya kutafuta sifa, Bali yalikuwa ya kazi tuu. Hakuwa na tabia ya kujikomba kwa Rais bali alitenda yaliyo ndani ya nafasi yake ya kazi tofauti na sasa wasaidizi wote wa Rais ni praise team yake bila aibu. Nadhani hata PM naweza sema hivyo.
Hivyo ndivyo ninavyo mjua Sokoine na jinsi walio kuwa wababe katika maeneo yao walivyo muogopa. Wapo ma RC na DC ambao wanalaumiwa sana wakati huu kwa tabia mbaya za kimaadili na utendaji hakika kwa Sokoine hangesubiri sijui mpaka nani aseme yeye angefyeka tuu.
 
Je uchunguzi wa kifo chake unaweza kufanyika upya ili ukweli ujulikane...yasemekana kifo hiki kilipikwa !!
 

..alionea wananchi kwasababu alisimamia zoezi la kuwakamata na kuwaweka kizuizini halafu mswada ukapelekwa bungeni kuanzisha sheria uhujumu uchumi na mahakama zake.

..pia uhaba wa bidhaa muhimu nchini haukusababishwa na walanguzi bali ulitokana na uzalishaji wa viwanda na mashirika ya umma kuwa mdogo.

..Mzee Mwinyi aliondoa tatizo la ulanguzi wa bidhaa bila kulazimika kukamata mali au kumuweka mwananchi yeyote kizuizini.

..Mwisho, Sokoine alifanya kazi kubwa wakati wa Vita vya Kagera akitumikia kama Waziri Mkuu.

..Kwa maoni yangu tunapaswa kumuenzi Edward Sokoine kwa mchango na utendaji wake wakati wa vita vya Kagera, ambavyo tulishinda, na siyo kampeni ya uhujumu uchumi ambayo ilikuwa na ukakasi wa kukiuka haki za msingi za raia.
 



Kwa nyongeza hapo, nasikia Mwl. Nyerere alimkataza kabisa asipande gari, atumie ndege. Lakini yeye alikataa. Na kuamua kupanda ndege. Nilishuhudia moja ya hotuba zake nikiwa mdogo sana. Nilimtazama siku hiyo nilipenyeza nikaa mbele kabisa, alitoa maamuzi kuwa ukifika ofisini ukakuta Boss au kiongozi wako hajafika, na muda wakazi tayari basi chukua kiti weka sehemu na utoe taarifa kwake, au kwa mkuu wa mkoa au wilaya. Nikiwa mdogo darasa la pili nilirudi nyumbani nimefurahi nikamwambia babu na bibi, nitawahi shule nitachukua kiti cha mwalimu wangu atakae chelewa na hasa kulikuwa na mwalimu mkorofi. Lakini baada ya hilo agizo watu wengi waliwahi kazini. Kweli alikuwa mtu wa watu na kiongozi asie na upendeleo.Nakumbuka alivaa kaunda suti na safari buti. Viatu hivyo alivipenda sana. Hiyo picha mpaka leo haijanitoka akilini. Niko kama namuona kwani tulitazamana mara nyingi. Tulikuwa na mtindo kiongozi akimaliza tu kuongea na kuondoka ndipo basi tunawahi kwenda kukaa katika kiti alichokuwa amekalia. Hivyo siku hiyo nilikaa katika kiti chake. Maaskari wa usalama walituangalia na kucheka.
 
Kingozi aliyenivutia sana mwenendo,tabia na unyoofu wake! RIP
 

Alikuwa anasali pale na kuna siku nafikiri IMF deligation walikuja kusali pale wakati wanatoka Moringe alikuwa anasalimiana nao kwenye ngazi pale, tena walikuwa wanatembea tu nafikiri walikuwa wamefikia Kilimanjaro Hotel. Kuna siku walikuwa wanasali na Mchonga pale wanakaa pamoja.
 

Kalamu 1 na Jokakuu et al. Nyinyi wapotoshaji wakati hamfahamu ukweli hayo majungu sijui huwa yanawasaidia vipi? Ni chuki ambayo mmeijaza mioyoni mwenu itawapelekea kufa siku si zenu. Mmeweka maslahi yenu binafsi mbele zaidi lakini hamtafanikiwa kwa sababu Watanzania sio wajinga. Tukiwapa ukweli mnabweka kama mbwa koko.

Nitakupa hint moja kubwa sana. Ukitafuta gazeti la Daily News wakati Sokoine alirudi kutoka kutibiwa JK Nyerere alikuwa safarini Musumbiji. Siku Mwl anarudi Dar Sokoine aliyekwenda kumpokea pamoja na viongozi wengine. Kama unaweza tafuta gazeti la Daily News waliweka front page yake picha iliyopigwa pale airport utafahamu jinsi 1. Moringe oops Sokoine alivyokua amevaa na jinsi Mwl Nyerere alivyokuwa anamshangaa kwa sababu alikuwa hakuamini, na Sokoine alipewa ulinzi mkali sana. BTW kama unaweza watafute watu waliokuwa wanafanya kazi naye karibu sana. Nitakupa jina moja tu la aliyekuwa mwandishi wake wa habari wakati huo anaitwa Accadoga Chiledi. Huyu alikuwepo hata kwenye ile ajali ya Dumila. Kuna mambo mengi ambayo ningeweza kusema lakini naweka kapuni. Sina sababu ya kupotosha kwa sababu nasema ukweli.

Kuhusu mabasi kuitwa dala dala muulize mtu yoyote atakwambia hiyo habari. Hiyo bei unayosema ati mlikuwa mnalipa senti hamsini haikuwa Dar itakuwa ilikuwa kwenu huko ulikokuwa. FYI wengi walikuwa hawaimudu hiyo shillingi tano, waliokuwa wanatumia wakati huo walikuwa wanafanya kwenye makampuni binafsi. Tulikuwa tunapanda taxi wakati huo Mjini hadi Temeke ilikuwa shillingi 30 hadi 40. Mkuu mimi nilikuwa shirika la umma wakati huo mshahara wangu ulikuwa shillingi 640.00 kabla ya kodi. na nakumbuka mshahara wangu wa kwanza niikwenda kununua pasi kwa shilingi 65.00 wakati ule unaitwa mtaa wa Independnce karibu na corner ya Morogoro Road.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…