JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

BTW msingi wa kuitwa daladala ulikuwa hivi: Shillingi tano za Kitanzania zilikuwa sawa na dola moja ya marekani na pound sterling 1 wakati huo tulikuwa tunabadili kwa shillingi 7 (saba). Hivyo mabasi hayo kuitwa daladala.
Sio sahihi usemacho, ngoja tumalize la Sokoine tukufahamishe chimbuko la daladala ambalo lilianzia Sumni sumni (yaani senti hamsini)
 
Food for thought. ITV walikuwa wakirusha hotuba za Nyerere kila mara (wosia wa baba). Lakini inashangaza kuwa nadra sana kukuta TBC wakifanya hivyo.

Hitimisho langu ni kuwa marais waliofuatia baada ya Nyerere kwa kiasi kikubwa hawajawa muafaka (comfortable) na urithi (legacy) wake. Wanautumia kujiinua kisiasa tu lakini hawautaki. They are averse to politics of poverty. None of them would follow Nyerere’s course to the letter. Naamini ndio sababu wanadhibiti sana TBC kurusha footage kamili za Mwalimu isipokuwa kutumia clips zake zinazowainua katika propaganda materials zao.
 
JokaKuu,
Vita ya uhujumu uchumi haikuweza kutekelezwa wacha uongo, sababu kubwa ni pale wahindi wengi walipokwenda kutupa TV sets baharini pamoja na mafridge nk. lile zoezi lilisitishwa ile pekua pekua ya kila nyumba haikufanyika. BTw Sokoine will be credited for so many things, hata bidhaa ambazo zilikuwa hazipatikani Tanzania yeye ndiye aliyesema zianze kuuzwa Tanzania baada ya ziara yake ya mikoa ya Tabora na Kigoma. (Kwa sababu wakati ule hata masufuria tu tulikuwa hatuna)
Nadhani haukuwa mjini zama hizo.....Joka Kuu yuko sahihi kwa 80%
 
Nakumbuka sana pale kanisani St Joseph akiwa amekaa katikati ya walinzi wawili benchi la pili kutokea mbele.

Akipenda kuvaa kaunda suit, alikuwa mtu mmoja mpole kwa muonekano wa nje.

Siku anafariki April 11 1984 nimetoka shule Forodhani nikaanza kusikia nyimbo za maombolezo, ilikuwa siku ya huzuni.

Nakumbuka sana pale kanisani St Joseph akiwa amekaa katikati ya walinzi wawili benchi la pili kutokea mbele.

Akipend kuvaa kaunda suit, alikuwa mtu mmoja mpole kwa muonekano wa nje.

Siku anafariki April 11 1984 nimetoka shule forodhani nikaanza kusikia nyimbo za maombolezo, ilikuwa siku ya huzuni.

Nakumbuka miezi ya kwanza kwanza 1984 kabla ya kifo chake nikiwa kijana mbichi baada ya kumaliza chuo na kuajiriwa wizarani (siitaji) muda mfupi kisha kuhamishiwa Singida na mkuu wa mkoa akiwa Kapteni Kafanabo ndio nilipojua kuwa Sokoine alikuwa kiongozi ambaye aliogopeka na sio wa mchezo mchezo.
Usiku mmoja Sokoine alimpigia simu Kapteni Kafanabo (RC) kumtaka taarifa ya hali ya chakula mkoani hapo, na kwa vile taarifa za kina hakuwa nazo alimuamuru kesho yake SAA 10 jioni aziwasilishe ofisini kwake Dar. Kumbuka enzi hizo barabara SGD to Dodoma haikuwa na lami na mbovu mno.
RC akawasiliana na RDD wake naye akamwambia ni mpaka asubuhi taarifa zitapatikana toka kwa maafisa mipango.
Kwa kukosa usingizi RC SAA 12 yuko ofisini na SAA 12.30 watumishi hatujafika maana SAA ya kazi ni 1.30 basi RC kichaa kikapanda "mbona watu wanachelewa hivi kazini? Nitafunga geti na wote nifukuze"!nk nk, hadi alipofika RDD na kumwambia atulie SAA za kazi bado ( na hakukuwa na mobile phone).
Jinsi alivyo hangaika Kapteni wa jeshi Kafanabo kwa woga wa amri za Sokoine sijasahau mpaka Leo.
Hakumuwahi PM hiyo SAA 10 licha ya kuwa na Range rover (gari la RC) kwani walipata ajali isiyo na human injury kati ya Dodoma na Moro ila sikumbuki eneo gani.
Sokoine hakutoa maagizo ya kutafuta sifa, Bali yalikuwa ya kazi tuu. Hakuwa na tabia ya kujikomba kwa Rais bali alitenda yaliyo ndani ya nafasi yake ya kazi tofauti na sasa wasaidizi wote wa Rais ni praise team yake bila aibu. Nadhani hata PM naweza sema hivyo.
Hivyo ndivyo ninavyo mjua Sokoine na jinsi walio kuwa wababe katika maeneo yao walivyo muogopa. Wapo ma RC na DC ambao wanalaumiwa sana wakati huu kwa tabia mbaya za kimaadili na utendaji hakika kwa Sokoine hangesubiri sijui mpaka nani aseme yeye angefyeka tuu.
 
Je uchunguzi wa kifo chake unaweza kufanyika upya ili ukweli ujulikane...yasemekana kifo hiki kilipikwa !!
 
JokaKuu,
Tunaweza kuyajadili yote haya:
1. "kuonea wananchi katika kampeni dhidi ya 'walioitwa wahujumu uchumi"' Sijui hapa umewalenga 'wananchi' au 'walioitwa wahujumu uchumi'. Natambua 'wahujumu uchumi' nao ni wananchi; lakini wanatambulishwa na sifa yao hiyo ya nyongeza.

2. "Mwalimu Nyerere na Sokoine walishindwa kuendesha uchumi wa nchi."

3." Badala yake wakaanza kulaumu na kusingizia kuwa hali mbaya ya uchumi imesababishwa na wahujumu uchumi na walanguzi" Hapa nitapata fursa ya kujifunza kutoka kwako juu ya ushahidi wa hawa wawili kuzitumia sababu hizi kuwa ndio zilizosababisha anguko la uchumi.

4. Itakuwa ni fursa ya nadra pia kupata nafasi ya kujua heshima anayopata Sokoine imejikita zaidi katika "kutambua mchango wake alipokuwa waziri mkuu wakati wa vita vya Kagera." Bila ya vita hivyo "usingewaelewa wanaomkubali Sokoine".

Yote haya manne tunaweza kuyajadili vizuri tu.

..alionea wananchi kwasababu alisimamia zoezi la kuwakamata na kuwaweka kizuizini halafu mswada ukapelekwa bungeni kuanzisha sheria uhujumu uchumi na mahakama zake.

..pia uhaba wa bidhaa muhimu nchini haukusababishwa na walanguzi bali ulitokana na uzalishaji wa viwanda na mashirika ya umma kuwa mdogo.

..Mzee Mwinyi aliondoa tatizo la ulanguzi wa bidhaa bila kulazimika kukamata mali au kumuweka mwananchi yeyote kizuizini.

..Mwisho, Sokoine alifanya kazi kubwa wakati wa Vita vya Kagera akitumikia kama Waziri Mkuu.

..Kwa maoni yangu tunapaswa kumuenzi Edward Sokoine kwa mchango na utendaji wake wakati wa vita vya Kagera, ambavyo tulishinda, na siyo kampeni ya uhujumu uchumi ambayo ilikuwa na ukakasi wa kukiuka haki za msingi za raia.
 
Tanzania hatujaweza kupata Waziri Mkuu mchapakazi kama huyu. Sokoine ndiye aliyeanzisha daladala yaani alipita pale Posta (Opps posta ya zamani si hii mpya) na msafara wake akaona watu wengi wanasubiri usafiri akauliza pana nini hapa ? Akaambiwa wananchi wanasubiri UDA kwa usafiri wa kwenda nyumbani. Basi Kesho yake akaagiza mabasi yote ya mashirika ya umma wakati ule yakimaliza kuwaleta/ kuwarudisha wafanyakazi yaendelee kuwachukua wananchi kuwaleta kazini na wenye mabasi binafsi waanze kufanya hivyo kama wanaweza. Ndipo ikazaliwa daladala. Alikuwa anajali Maisha ya wananchi wa Tanzania.

Hata kabla ya kifo chake ndege iliyotakiwa kumrudisha Dar es Salaam kutoka Dodoma ilichelewa basi akasema hakuna shida nitakwenda Dar kwa gari, hapo ndipo alipokutana na mauti kule Morogoro (Dumila).

Watu wengi walikuwa wanasema kwamba JK Nyerere alikuwa anamwandaa kuwa Rais akiondoka kwa sababu hiyo ilikuwa ni mara yake ya pili kuchukua cheo hicho baada ya kujiuzulu, ikumbukwe Mawaziri wengi wanyakuaji walikuwa wanamuhara.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake peponi salama.



Kwa nyongeza hapo, nasikia Mwl. Nyerere alimkataza kabisa asipande gari, atumie ndege. Lakini yeye alikataa. Na kuamua kupanda ndege. Nilishuhudia moja ya hotuba zake nikiwa mdogo sana. Nilimtazama siku hiyo nilipenyeza nikaa mbele kabisa, alitoa maamuzi kuwa ukifika ofisini ukakuta Boss au kiongozi wako hajafika, na muda wakazi tayari basi chukua kiti weka sehemu na utoe taarifa kwake, au kwa mkuu wa mkoa au wilaya. Nikiwa mdogo darasa la pili nilirudi nyumbani nimefurahi nikamwambia babu na bibi, nitawahi shule nitachukua kiti cha mwalimu wangu atakae chelewa na hasa kulikuwa na mwalimu mkorofi. Lakini baada ya hilo agizo watu wengi waliwahi kazini. Kweli alikuwa mtu wa watu na kiongozi asie na upendeleo.Nakumbuka alivaa kaunda suti na safari buti. Viatu hivyo alivipenda sana. Hiyo picha mpaka leo haijanitoka akilini. Niko kama namuona kwani tulitazamana mara nyingi. Tulikuwa na mtindo kiongozi akimaliza tu kuongea na kuondoka ndipo basi tunawahi kwenda kukaa katika kiti alichokuwa amekalia. Hivyo siku hiyo nilikaa katika kiti chake. Maaskari wa usalama walituangalia na kucheka.
 
Tukiendelea na mijadala mingine nimeonelea niwashikilishe video hii. Nimeulizwa mara kwa mara kuhusu video/ audio ya Edward Sokoine. Katikati upekuzipekuzi wangu nimekutana na hii. (Kuna mtu aliniuliza chemba kuwa angependa kumuona na kumsikia Sokoine) badala ya kusoma tu habari zake. Hii ni miongoni mwa video nzuri nilizopata kuziona au kuzisikia.


Kingozi aliyenivutia sana mwenendo,tabia na unyoofu wake! RIP
 
Nakumbuka sana pale kanisani St Joseph akiwa amekaa katikati ya walinzi wawili benchi la pili kutokea mbele.

Akipenda kuvaa kaunda suit, alikuwa mtu mmoja mpole kwa muonekano wa nje.

Siku anafariki April 11 1984 nimetoka shule Forodhani nikaanza kusikia nyimbo za maombolezo, ilikuwa siku ya huzuni.

Alikuwa anasali pale na kuna siku nafikiri IMF deligation walikuja kusali pale wakati wanatoka Moringe alikuwa anasalimiana nao kwenye ngazi pale, tena walikuwa wanatembea tu nafikiri walikuwa wamefikia Kilimanjaro Hotel. Kuna siku walikuwa wanasali na Mchonga pale wanakaa pamoja.
 
Mkuu, mimi sijawahi kusikia habari ya Ndugu Sokoine "...kushambuliwa na kwenda kutibiwa Europe etc." Hii habari ndio naipata toka kwako kwa mara ya kwanza kabisa. Itapendeza kama utaweza kuielezea zaidi.

Ninachojua ni kwamba alikwenda masomoni, baada ya kujiuzuru.

Na kuhusu 'time frame' kama ushahidi wa daladala ya Tanzania kuwa na thamani ya dollar moja ya Kimarekani, hata ungekwenda hadi 1961, hutapata US $ 1 kuwa sawa na Tsh. 5.00

Kalamu 1 na Jokakuu et al. Nyinyi wapotoshaji wakati hamfahamu ukweli hayo majungu sijui huwa yanawasaidia vipi? Ni chuki ambayo mmeijaza mioyoni mwenu itawapelekea kufa siku si zenu. Mmeweka maslahi yenu binafsi mbele zaidi lakini hamtafanikiwa kwa sababu Watanzania sio wajinga. Tukiwapa ukweli mnabweka kama mbwa koko.

Nitakupa hint moja kubwa sana. Ukitafuta gazeti la Daily News wakati Sokoine alirudi kutoka kutibiwa JK Nyerere alikuwa safarini Musumbiji. Siku Mwl anarudi Dar Sokoine aliyekwenda kumpokea pamoja na viongozi wengine. Kama unaweza tafuta gazeti la Daily News waliweka front page yake picha iliyopigwa pale airport utafahamu jinsi 1. Moringe oops Sokoine alivyokua amevaa na jinsi Mwl Nyerere alivyokuwa anamshangaa kwa sababu alikuwa hakuamini, na Sokoine alipewa ulinzi mkali sana. BTW kama unaweza watafute watu waliokuwa wanafanya kazi naye karibu sana. Nitakupa jina moja tu la aliyekuwa mwandishi wake wa habari wakati huo anaitwa Accadoga Chiledi. Huyu alikuwepo hata kwenye ile ajali ya Dumila. Kuna mambo mengi ambayo ningeweza kusema lakini naweka kapuni. Sina sababu ya kupotosha kwa sababu nasema ukweli.

Kuhusu mabasi kuitwa dala dala muulize mtu yoyote atakwambia hiyo habari. Hiyo bei unayosema ati mlikuwa mnalipa senti hamsini haikuwa Dar itakuwa ilikuwa kwenu huko ulikokuwa. FYI wengi walikuwa hawaimudu hiyo shillingi tano, waliokuwa wanatumia wakati huo walikuwa wanafanya kwenye makampuni binafsi. Tulikuwa tunapanda taxi wakati huo Mjini hadi Temeke ilikuwa shillingi 30 hadi 40. Mkuu mimi nilikuwa shirika la umma wakati huo mshahara wangu ulikuwa shillingi 640.00 kabla ya kodi. na nakumbuka mshahara wangu wa kwanza niikwenda kununua pasi kwa shilingi 65.00 wakati ule unaitwa mtaa wa Independnce karibu na corner ya Morogoro Road.
 
Back
Top Bottom