JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

Mkuu 'Ole', nimekwishatambua wewe ni mtu wa aina gani. Inatosha sasa.
 

Mkuu MMm hongera sana kwa kutukumbusha kuhusu shujaa wetu na mzalendo namba moja wa Tanzania.

Hixi videos zinaweza kupatikana (kama anavyosema mkuu Paschal) kutoka hivyo vyanzo alivyovitaja.

Ila nimedokezwa kwamba kuna kulipa ada kiasi hivi.
 

..wananchi walikamatwa, wakawekwa kizuizini, halafu baada ya hapo bunge likapitisha sheria ya makosa ya uhujumu uchumi.

..mtitiriko huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala wa sheria.

..sasa waliiokamatwa kwa mtindo huo walikuwa ni wengi. Mashauri yao yalichukua muda mrefu. Na wengi wao hawakupatikana na hatia lakini maisha na mali zao ziliharibika.

..Serikali ilikuwa inajihujumu yenyewe kwa kushindwa kufanya marekebisho ya sera zake ili kuweza kukabiliana na changamoto za kiuchumi zilizokuwa zimejitokeza.
 

Mkuu lakini hao unaowatetea walificha bidhaa na baadae kuzilangua kwa bei ya juu.

Ndo maana kukawepo msako wa walanguzi na wahujumu uchumi.

Au mkuu hukuonja zie shubiri za kupanga mistari na madaftari?

Ugali wa Yanga je, waukumbuka?
 
"Quality" nadra sana kuwa nazo viongozi wengi.
Kassim Majaliwa, anajitahidi sana katika mazingira magumu

Mkuu Chakaza, umetoa 'ushuhuda' kama wa 'walokole', ila wao huweka chumvi nyingi. Pongezi kwako na heshima mkuu.
 
Hilo la kushindwa kuendesha uchumi ni analysis nyepesi sana kwa suala very complicated. Linahitaji mjadala unaojitegemea. Hukuwatendea haki hao magwiji wa uongozi.

..hata nyinyi mnaotoa SIFA ZA JUMLA-JUMLA hamuwatendei haki Mwalimu Nyerere na Edward Sokoine.

..sikatai kwamba walikuwa wazalendo, lakini tuseme ukweli kwamba walikuwa na mapungufu makubwa ktk usimamiaji wa uchumi wa nchi.

NB.

..unayafahamu makosa ya Mwalimu Nyerere yaliyosababisha kilimo cha mkonge na korosho kiporomoke?
 
Mkuu lakini hao unaowatetea walificha bidhaa na baadae kuzilangua kwa bei ya juu.

Ndo maana kukawepo msako wa walanguzi na wahujumu uchumi.

Au mkuu hukuonja zie shubiri za kupanga mistari na madaftari?

Ugali wa Yanga je, waukumbuka?

..nakumbuka sana.

..lakini Sokoine alipowakamata haikufanya bidhaa zifurike madukani na foleni ziishe.

..viwanda vyetu vilikuwa havizalishi bidhaa za kutosha.

..Sokoine hata kama alikuwa na nia nzuri hatua alizochukua hazikuleta matokeo chanya.

..Na zaidi hatua alizochukua hazikuzingatia RULE OF LAW.
 
Mtiririko huo kwa hakika ni "uvunjifu wa haki za binaadam na utawala bora," bila ya shaka yoyote. Hata hivyo, usisahau kuwa Katiba ilikuwa inatoa mamlaka kwa Rais katika mambo kadhaa ambayo yalihitaji kuchukuliwa hatua kama yanahatarisha usalama wa taifa.
Viongozi hawawezi kuacha kuchukua hatua na taifa lipate madhara eti kwa vile "sheria zilikuwa hazijatungwa." La mhimu hapa ni kuwa sheria ilitungwa na wahusika walishazuiwa wasilete madhara zaidi kabla ya sheria kutungwa.

Katika hali ya mapambano (vita), kuna watu wengi na mali huathirika bila ya kuwa wahusika wa moja kwa moja katika vita hivyo (collateral damage). Vita haiwezi kuacha kupiganwa kwa sababu tu ya hofu ya kuumiza wasiokuwa maadui, hii ndio bahati mbaya sana ya matukio kama haya unayoeleza hapa.

Lililo mhimu ni kwamba sheria ilitungwa na wale ambao hawakuhusika waliachwa huru. Kwa hiyo dhana ya 'kuonea' haistahili kutumiwa katika kulaani yaliyofanyika.
 
..sikatai kwamba walikuwa wazalendo, lakini tuseme ukweli kwamba walikuwa na mapungufu makubwa ktk usimamiaji wa uchumi wa nchi.
Ndio maana, mkuu 'Msuluhishi' kakwambia kwamba unatoa "Mahitimisho' bila ya maelezo katika jambo ambalo ni 'complicated' kama hili la uchumi. Huu hapa ni mfano mzuri.
 



Vyombo vingi vya habari vya nje vilielezea ajali na kifo chake kwamba aliuawa.

TANZANIAN PREMIER IS KILLED

13/4/1984
TANZANIAN PREMIER IS KILLED; WAS LEADER'S HEIR APPARENT TANZANIAN PREMIER IS KILLED; WAS LEADER'S HEIR APPARENT?
Reuters


Hizi siasa za Afrika ni siasa mbaya sana na ndizo zimepoteza viongozi wengi wazuri na ambao kama wangeendelea kuwepo, basi baadhi ya nchi nyingi za Afrika ikiwepo Tanzania zingekuwa mbali kimaendeleo.

Hayati Mwalimu alianza kuzungumzia kustaafu siasa tangu katikati ya 1980 na hapo ndipo mapigano ndani ya corridors of power yalipoanza.

Kwa kwa mtizamo wangu ni kwamba hayati Sokoine huenda alitumia hiyo vita ya wahujumu uchumi kutaka kujijenga kisiasa na hivyo kusababisha mtafaruku ndani ya CCM ambamo kuna wanasiasa wengine walitamani kuwa maraisi.

Hivyo kufikia mwaka 1983 kuna viongozi kadhaa waandamizi ambao walianza kutajwa na miongoni mwao alikuwemo hayati Sokoine, hayati Rashid Kawawa na Aboud Jumbe Mwinyi, Cleopa Msuya na mzee wetu Salim Ahmed Salim.

Kumbuka Sokoine alifariki akiwa mdogo sana at 46 na hao wazee walikuwa mbele yakle kisiasa na kiuzoefu.

Kuna kitabu chaitwa The Dark Side of Nyerere Legacy ambacho kimeandikwa na Ludovick Mwijage na anaeleza mengi.

Ila naunga mkono juhudi za hayati Sokoine katika kuhakikisha kwamba hakuna wahujumu uchumi na walanguzi wa bidhaa kwa wakti ule.

Hivyo hata sasa tukiona kiongozi anapambana na nguvu nyingi za fedha na bidhaa kufichwa na kisha baadae akaja hadharani kubainisha majaribu juu ya I=uahi wake basi wapata fursa nzuri ya kuwaelewa wale wote wasoitakia mema nchi yetu.

Nina mengi sana ya kuyaeleza lakini naomba niishie hapo.
 
Ndio maana, mkuu 'Msuluhishi' kakwambia kwamba unatoa "Mahitimisho' bila ya maelezo katika jambo ambalo ni 'complicated' kama hili la uchumi. Huu hapa ni mfano mzuri.

..hata nyinyi mnaosifia mnatoa sifa za jumla-jumla ktk masuala ambayo ni complicated.
 
Alikijua kizungu? Yan kiingereza kimempiga tu chenga Magufuli Mungu wangu😀
 

..Nyerere alikuwa akimpenda nani zaidi kati ya Sokoine na Salim Salim?

..Mzee Kawawa hakuwa anautamani Uraisi.


..Kawawa alibebeshwa misalaba ya watu wengine na hakuwa na kinyongo.
 
..Nyerere alikuwa akimpenda nani zaidi kati ya Sokoine na Salim Salim?

..Mzee Kawawa hakuwa anautamani Uraisi.


..Kawawa alibebeshwa misalaba ya watu wengine na hakuwa na kinyongo.

Nafikiri aliwapenda wote.

Sokoine JMT na Salim kwa Zanzibar.

Rejea kesi ya A. Jumbe ilopelekea kulazimishwa kujiuzulu.
 
Mkuu JokaKuu ni kweli kabisa Nyerere na Sokoine kwa namna fulani walifanya makosa katika ujenzi wa uchumi wetu.
Lakini nadhani hata upungufu wa wataalamu wa kutosha ulichangia mengi kwenda kombo maana ukichunguza hawakuwa na dhamira chafu kama hawa wa sasa.
Wataalamu wa kutosha lakini hawatumiwi na wakitumiwa hawasikilizwi. Wizi sasa hivi umekuwa wa kimtandao unao ongozwa na chama kama alivyo weka hadharani Mkapa.
EPA na Escrow ni wizi wa kuifanya ccm ibaki madarakani. Ndio maana hata ripoti ya CAG kuhusu 1.5 trillion zisizo onekana CCM badala ya kuisimamia serikali itoe majibu yenyewe ndio inatetea hadi kumtuma Polepole akokotoe eti hesabu za CAG kuwa hajui matumizi ya hiyo hela!
Kwa hiyo pengine nchi wakati huo ingekuwa na wataalamu kama sasa mambo yangekuwa mengine tofauti na haya ma batch ya manyang'au yaliyo madarakani
 
Nafikiri aliwapenda wote.

Sokoine JMT na Salim kwa Zanzibar.

Rejea kesi ya A. Jumbe ilopelekea kulazimishwa kujiuzulu.

..nimeuliza alikuwa akimpenda yupi zaidi ya mwenzake?

..alimpenda Sokoine zaidi, au alimpenda Salim Salim zaidi?
 
Asante sana, Mleta mada. Nimefarijiaka haswa. Mungu akubariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…