JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

Nimeona ameshuka kutoka kwenye Mercedes Benz made in Germany baba wa Capitalism.

Usiamini communist hata siku moja, Stalin na Mao waliuwa watu zaidi milioni 100 kueneza communism, Mwalimu Nyerere alikuwa anatibiwa London na siyo Soviet Union au China!
Ujamaa ni mfumo wa kuwalinda watawala kwa kuwafanya watu wawe masikini ili watawaliwe kirahisi.Ujamaa haukuwa kwa ajili ya wananchi bali ubinafsi Wa viongozi,hata viongozi wajamaa awakuishi kijamaa huku wakiwalazimisha wananchi kuwa wajamaa.
 
JokaKuu,

Wote walikuwa na mawazo ya kimasikini na ndio chanzo cha umasikini wetu japo walirithi utajili toka hazina ya mkoloni.

Waliaminisha watu uzalendo ni kuwa masikini, waliwachukia matajiri na watu waliofanikiwa hata kuwafanyia hila za kupora Mali zao walizochuma kihalali toka enzi ya mkoloni, maana mkoloni akuwa na shida mwafrika ajimilikishe Mali ni baada ya wakoloni weusi walipopora Mali za wananchi kwa sababu ya wivu na chuki za malezi ya ufukara waliokulia hivo wakawachukia matajiri kwa kuwafanya waishi kishetani.

Kwa kudhulumu mali za watu Mungu aliwalaani wakafa masikini,ashukuriwe mzee ruksa ndipo watu wakaanza kuchuma mali tena na kuanza japo kupata matajiri kama kina Hayati Mengi, nk.

Dunia nzima matajiri ndio nguzo ya uchumi wa nchi huweziendelea bila wao,kwani ndio wanaokuza makusanyo ya kodi na kutoa ajira na kuleta utulivu kwenye nchi na ndio wamshibishae masikini.

Kuwafanya matajiri waishi kishetani ni kujipiga kabali kwani makusanyo ya kodi yatapungua,tatizo la ajira litaongezeka,njaa itaongezeka,chuki dhidi ya serikali itaongezeka sababu ya njaa,uhalifu na uasi ni rahisi kutokea.

Ujamaa ilikuwa ni nadharia zaidi ya kutawala watu kuliko uhalisia thus umeshindwa duniani kote, ujamaa ndio chimbuko la tawala za kidikteta duniani.Ujamaa hauruhusu utawala wa kubadilishana vijiti ukazania kukaa mda mrefu madarakani
 
muheza2007,
Umeeleza kweli ila sehemu ya chanzo cha sh 5 kuitwa dala sidhani kama uko sahihi (japo sina uhakika). Ila sehemu ya ni kwanini magari yakawa yanaitwa dala dala, ni kweli.

Makandokta walikuwa wanapiga debe kwa kusema: dala, dala, dala... (wakimaanisha bei yake ni sh 5.) basi watu wakaishia kuyaita dala dala. Tena hayo magari mwanzoni yalikuwa yana operate illegally kwa kijificha ficha na mengi yalikuwa ni vibasi vidogo kama vi-hiece lakini yalikuwa yamekongoronyoka sana na wamiliki wake wengi walikuwa wachaga.
 
mulaga,
Sio kweli. Kuna nchi zilikumbatia sana matajiri Afrika lakini sasa hivi mbona wako kwenye hali mbaya kabisa?

Hapo Kenya tu tangu zamani pamekuwa nchi ya kukumbatia matajiri lakini mpaka kesho na keshokutwa kuna umaskini wa kutupwa. Wachache ndiyo wanafaidi. Ni bora hata hapa kwetu.
 
Bobby,
Uko sahihi kabisa. Hizi za kuongeza neno ''kijana'', ''msomi'', ''injinia'' ni matambo ya siku hizi tu hasa baada ya wanasiasa kuona kuwa kizazi cha sasa cha nchi yetu hakitafakari lolote bali kinadanganywa na kuvutiwa kirahisi na sifa za kijinga.
 
Ujamaa ni mfumo wa kuwalinda watawala kwa kuwafanya watu wawe masikini ili watawaliwe kirahisi.Ujamaa haukuwa kwa ajili ya wananchi bali ubinafsi Wa viongozi,hata viongozi wajamaa awakuishi kijamaa huku wakiwalazimisha wananchi kuwa wajamaa.
Na mfumo wa kibebari haulindi watawala? Kuna mfumo mbaya kama wa ubebari katika kulinda watawala?
 
macho_mdiliko,

Hilo ni tatizo la kisera na ufisadi na hali ya viongozi kutowajibika kuleta sera za kuwainua masikini kwa kushindwa kuwatumia matajiri kupunguza hio gap,mbona nchi zilizoendelea serikali zao zimewatumia matajiri positive na wamepunguza gap.

Kimakusanyo kimapato Kenya wako juu zaidi yetu yanawasaidia angalau kupunguza utegemezi Wa bajeti yao hata ukitazama deni la taifa letu ni kubwa kuliko wao,Pesa yao inathamani,mauzo ya nje wako juu.Viwango vya uelewa angalau wako juu
 
Na mfumo wa kibebari haulindi watawala? Kuna mfumo mbaya kama wa ubebari katika kulinda watawala?
Ubepari uendana na demokrasia ujamaa uendana na udikteta demokrasia uzaa maendeleo ujamaa na udikteta uzaa umasikini madikteta wote dunia maendeleo ya watu si vipaumbele vyao
 
Hawezi kwa sababu ya unafiki tu. wakati wa miaka ile baada ya J K Nyerere kuonyesha kwamba asingegombea tena 1985 Sokoine was unchallenged kutokana na aliyokuwa anafanya. Baada ya kufariki SAS ndiye angechukua, lakini unafahamu what happened.
Nipo safu ya mbele kabisa kujua "what happened"
 
mulaga,
Kama unathubutu kusema Kenya wako vizuri kuliko sisi (nazungumzia wananchi wa kawaida na siyo matajiri) basi Kenya huwa unaisikia kwenye vyombo vya habari tu.

Sisi waafrika hatuna utamaduni wa kutembea lakini ungetembelea Kenya basi ungebadilisha mawazo.
 
Ubepari uendana na demokrasia ujamaa uendana na udikteta demokrasia uzaa maendeleo ujamaa na udikteta uzaa umasikini madikteta wote dunia maendeleo ya watu si vipaumbele vyao
Umebapari vs Ujamaa: Huu ni mjadala ambao umetawala dunia kwa muda mrefu. Uzoefu wangu unanimbia ujamaa ule ambao siyo extreem (kama waliokuwa nao warusi) ni mzuri kuliko ubebari. Ukitembelea nchi za Scandivia utaelewa zaidi.

Japokuwa wameegemea kwenye ubebari lakini mambo yao mengi ni kama wajamaa. Na hizi ndizo nchi zenye watu wenye maisha mazuri zaidi. Kila mtu ana apportunities sawa tofauti na nchi zenye ubebari mkali kama Marekani ambako kuna sehemu zenye umaskini wa kutisha.
 
Kma unathubutu kusema Kenya wako vizuri kuliko sisi (nazungumzia wananchi wa kawaida na siyo matajiri) basi Kenya huwa unaisikia kwenye vyombo vya habari tu. Sisi waafrika hatuna utamaduni wa kutembea lakini ungetembelea Kenya basi ungebadilisha mawazo.
Uchumi Wa nchi yaani GDP
 
Uchumi Wa nchi yaani GDP
Mkuu Kenya ina matatizo sana. Sidhani hata ukienda kule kama utafurahia maisha yake. Kwanza matatizo ya ardhi ni makubwa. Sehemu nzuri zote zilishachukuliwa na matajiri.

Nyerere hakuruhusu hilo litokee na ndiyo maana mpaka leo watu wa kawaida kbaisa wanaweza kumiliki ardhi. Shukrani anayopewa ni kuitwa alichukia matajiri. Nyerere ahakutaka ule utajiri wa kijanja janja, wa kunyakuwa na siyo kwamba hakupenda matajiri.

Tatizo lililotokea ni kwamaba watu alikuwa ana-apply ideology kwao siyo watu sahihi. Wamejaa elements za wizi na uvivu.
 
JokaKuu,
Mimi sina sababu ya kukunyanyasa wewe, na uwezo huo sina.

"kupitishwa sheria baada..." nimejibu hilo, lakini hutaki kuona niliyoandika kuhusu sababu ya kufanya hivyo, sasa unataka nifanye nini? Soma tena niliyoandika hapo, kama unayapinga, yapinge kwa hoja bila ya kunilalamikia mimi.

Sokoine haheshimiwi kwa sababu ya kuwa "Waziri Mkuu" tu wakati wa Vita. Hili nalo nimeeleza hapo juu, lakini hutaki kutambua nilichoeleza.
Marehemu Sokoine anaenziwa kwa sababu nyingi nyingine kuhusu uongozi wake, na sio kwa kuwa "Waziri Mkuu" pekee wakati wa vita kama unavyotaka wewe kuaminisha watu

"Uhujumu uchumi" ni kosa katika nchi yoyote ile duniani. Itakuwa ajabu sana kama ulitaka uongozi wa nchi wasilishughulikie hilo ipasavyo, ikiwa na pamoja na kutunga sheria kuwabana wanaohujumu uchumi.
 
Mkuu Kenya ina matatizo sana. Sidhani hata ukienda kule kama utafurahia maisha yake. Kwanza matatizo ya ardhi ni makubwa. Sehemu nzuri zote zilishachukuliwa na matajiri. Nyerere hakuruhusu hilo litokee na ndiyo maana mpaka leo watu wa kawaida kbaisa wanaweza kumiliki ardhi. Shukrani anayopewa ni kuitwa alichukia matajiri. Nyerere ahakutaka ule utajiri wa kijanja janja, wa kunyakuwa na siyo kwamba hakupenda matajiri. Tatizo lililotokea ni kwamaba watu alikuwa ana-apply ideology kwao siyo watu sahihi. Wamejaa elements za wizi na uvivu.
Hawa watu wengine wanasifia tu hata wasiyoyajua. Uchumi wa Kenya umeshikiliwa na watu wachache sana.

Walichofanikiwa Kenya kwa kiasi kikubwa ni elimu. Hili ndilo litakalowanyanyua haraka mbeleni.
 
mkuu Barbarosa kwenye hili eneo la kupinga ujamaa nakuunga mkono....... ila kumbuka hata jm anajitanabaisha na ujamaa!
Nimeona ameshuka kutoka kwenye Mercedes Benz made in Germany baba wa Capitalism.

Usiamini communist hata siku moja, Stalin na Mao waliuwa watu zaidi milioni 100 kueneza communism, Mwalimu Nyerere alikuwa anatibiwa London na siyo Soviet Union au China!
 
Cheki wanavyojipendekeza wazee wetu wa sasa, je viongozi wa namna hii wanaweza kutoa ushauri unaopingana na mkuu wao kwa ajili ya kumsaidia nchi isiteketee kijamii, kisiasa, kiuchumi na kisera?

15 Nov 2019
MAJALIWA Atokwa MACHOZI MAGUFULI Alivyomwaga MAMILION


Mkuu Bagamoyo, utamlaumu bure Kassim Majaliwa. Labda kama hutaki kuamini ugumu wa kazi anayoifanya katika mazingira aliyomo.

Kwa maoni yangu, huyu ni kiongozi mzuri akipewa nafasi ya kufanya kazi yake kwa ushirikiano na utashi wake.
 
Back
Top Bottom