JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

Hongera sana Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna suala la mfumo wa elimu. Hili tumeliongea ktk muktadha tofauti tofauti sana. Kwa ufupi nini kifanyike ktk suala la elimu?
Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Hili linahitaji jibu zito na refu sana, japo niseme tu: Pia naliandalia chapisho ambalo litatoka hivi karibuni.
Hili ni suala la kisera na kimfumo, nadhani tunahitaji kubadilika katika vyote.


Ukitenga Chama na Serikali kuna faida nyingi sana: Kwanza kabisa unajenga tabia ya uwajibikaji kwa viongozi ambao hutumia dola katika kuficha udhaifu wao wa kiuongozi. Pili, wananchi watajenga imani kubwa sana juu ya serikali yao. Tatu, tutakuwa tumehamia kwenye ngazi ya tatu kabisa ya kiungozi ambayo inategemea nguvu ya kitaasisi kuliko kuangalia watu binafsi.

Hili alilisema Prof Max Weber kwamba nchi inapoacha na kutumia Charisma kwenye uongozi basi hulazimika kujenga taasisi imara amabzo zina mifumo inayoyabirika. Mifumo inayotabirika ndiyo hujenga imani kwa wananchi. Tunahitaji sana uongozi wa kitaasisi za kitaalamu na siyo taasisi vyama.

Hoja ya pili, je tukikitoa chama kuna athari zake ??: Ndiyo athari zake ni nyingi sana endapo utakuwa huna chama mbadala chenye nguvu na utayari wa kushika dola. Hili ndilo liliwasumbua sana Wafaransa baada ya mapinduzi ya mwaka 1789. Walimpinua mfalme lakini The Republicans/Jacobins mbali na kuimba nyimbo za :"Liberty, Equality and Fratternity" hawakuwa na mkakati wa kuwawezesha kuongoza nchi. Kukawa na ombwe kubwa la kiuongozi. Sasa udikteta waliouchukia ndiyo ukazaliwa na Napoleon Bonaparte akajichukulia nchi. Au mfano mwingine ni ule wa Libya, wamemtoa Gaddafi halafu hawana mbinu mbadala, hadi Obama alikiri hili.

Swali ni je: CCM ikitoka kuna chama mbadala ambacho kimejiandaa kiungozi kuweza kujaza nafasi ya viatu vya CCM ?? Ambacho kimejiandaa kabisa kuweza kuongoza jeshi la Tanzania, Polisi wa Tanzania, Usalama wa Taifa, Kushika hatama ya sera za mambo ya nje, Kushika hatamu ya Sera za elimu. Kuongoza nchi huhitaji tu kuwa na sera bali watu wenye uwezo wa kusimamia hizo sera. CCM walijipanga sana lakini kilichowaangusha ni michezo ya Rushwa, Udikteta wa kukanyaga haki za binadamu na Kugawana madaraka kwa upendeleo ambapo tumepata watawala wasio na uwezo wa kuongoza. Lakini mbali na udhaifu wao wote CCM wana Sera nzuri sana na viongozi wazuri sana: Japo hawawezi kusimamia sera zao na hao wenye akili hawapewi nafasi, Ujinga umeshika hatamu ndani ya chama.

Sasa kama kuna chama chenye hizo sifa mbadala basi, hata CCM ikitoka kesho nchi itaendelea tu bila kutikisika. Lakini kama hakuna chama mbadala, hata tukifanya mapinduzi na kuwatoa CCM tutakuwa kama Libya . Hivyo kama ukitaka kukitoa chama basi tafuta chama mbadala wake chenye uwezo kuliko chenyewe. Displacement Theory.


Hili limekaa kichama-chama sana na naomba nisiliongelee kabisa, maana hata nikiliongelea ni wachache sana ambao watanielewwa na kukubaliana na mimi. Japo kiufupi tu, kuna mihemko pande zote mbili.....
 
Nadhani hili linachangia mno.. ila Ahsante kwa mada zako zenye madini adimu!!
Je ushauri kwa vijana 20-26yrs wako ni upi.. kijamii, kiuchumi na kisiasa

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Wafanye kazi kwa bidii, Wasome kwa bidii, Wapunguze starehe, Wampende Mungu.
Kubwa zaidi wasikubali kukata tamaa ya maisha na wawe na uthubutu.
Mambo mazuri hayaji kirahisi.
 
salama mkuu Malcom Lumumba . Ni hard talk lakini ipo chitchat!!. tutatembea mwote. Album gani kwako ni bora ya muda wote, huchoki kuisikiliza? vipi kuhusu series na movie? Comedian gani unamkubali mbaya?
Kama ni Album: Tango in the night by Fleetwood Mac ni Album ya mwaka 1987.
Series ninazozipenda sana: The Roots na Friends.
Movies: The God Father, The Good, The Bad and The Ugly na Pirates of the Caribbean
Comedians: Dave Chapelle na Richard Pryor
 
Mkuu kuna kipindi kulikuwa na mjadala kuhusu mfumo wa serikali wa majimbo, unafikiri unaweza kutufaa?
Hata sasa hivi tunajiongoza kimajimbo lakini without fully autonomy: Tupo semi autonomous without a clear legal set up.
Nadhani mfumo wa majimbo ni mzuri sana na unaweza kuleta maendelea ya haraka sana kwa taifa letu endapo kutakuwa na full autonomy.

Kwanza kabisa kuna vyeo visivyo na mantiki sana kama wakuu wa mikoa na wilaya vitapotea kabisa: Viongozi watawekewa wajibu mkubwa sana kwasababu watakuwa ni watu wa kuteuliwa zaidi ya kuchaguliwa. Sanduku la kura humjengea mwanasiasa adabu.

Pili, tutakuwa na nguvu nzuri katika ukusanyaji wa mapato na kodi pia kuongezeka kwa uzalishaji maana ni jimbo ndiyo litakuwa linapeleka mapato na kuzalisha. Utoaji huduma utakuwa ni wa haraka sana. Uzalishaji utakuwa mkubwa kwasababu zile rasilimali ambazo hazitumiki ipasavyo itabidi zitumike ile kuongeza pato la jimbo:

Tatu, tutakuwa tumetatua tatizo la ajira kwa sehemu kubwa sana, kwasababu serikali itakuwa ni kubwa sana. Wengi wanaogopa sana lakini kama serikali imekuwa ni kubwa na tatizo la ajira linamalizwa nasema tu hewalaaa wapeni watoto wetu ajira. Maana kama uzalishaji utaongezeka huu mzigo wa kuendesha serikali hautaonekana kabisaa..
 
Mkuu hili limekaa kisiasa sana, na naomba kwa leo hii nisilichangie kabisa.
Lakini siku za mbeleni nitalizungumzia kwa uwazi kabisa.
 
im
Imperial president.kuna watu wakione hii kitu wanawaza ukapimwe mkojo tuu,kwamba haya ni mawzo ya kibeberu tuuu.

Nami naamini kabisaa bila kuondoa hiyo kitu tubakia wa kulaumiana tuu.
 
Nimekupata vyema sana mkuu.
 
Mie nina kiswali uchwara

Unazungumziaje structure ya muungano wetu na ufanisi wake? ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Muungano unahitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu. Kero za muungano hazitaisha kwa kuwa na katiba mpya pekee bali kwa kuwa na mjadala wa wazi kabisa kuhusu asili ya muungano wenyewe: Umetoka wapi , Uko wapi na faida zake, Unakwenda wapi na Nini kifanyike. Nadhani baada ya mjadala wa wazi ndiyo tutaanza kuzungumzia sasa masuala ya muundo na ufanisi....
 
Mkuu tutoke kidogo mpaka Africa mashariki ad beyond.

Iangalie Rwada. Leo inaonekana kuwa ni ya kupigiwa mfano Africa nzima ilihali vyanzo vyake vya mapato ni questionable. Je imefika wakati na sisi wa Tz kunufaika na migogoro ya majirani zetu kwa kufanya looting kama Kagame ili kupata maedeleo kwa kiasi fulani ?

Na je hizi rumors za mitandaoni kuwa Kagame anainfluence ktk serikali ya Tz unazichukuliaje?

Je Tanzania tunaanza kuondolewa na Rwanda ktk sehemu yetu kama influencer wa Afrika mashariki na kati?

Umesema wewe ni mwanasheria kwa taaluma. Unamchukuliaje Fatuma Bensounda na ofisi yake hasa kwa kuzingatia yale ya Ivory Coast na Garbo ambaye ameachiwa sasa, Kenyatta na Ruto pia wako huru sasa to mention te few. Je huwa anatenda haki ktk uandaaji wa mashtaka au hutumika kama mbwa tu anayewatisha waafrika wenzake huku akiwaacha wengi weyemakosa kama haya wasio waafrika?

Somaliland akipata uanachama Afrika mashariki tutegemee nini?

Pia naomba busara yako kuhusu Economic Freedom Fighting ( EFF) ya Julius Malema: Jana wamefanya manifesto Launch huku wakipigaia Sera ya kuteka ardhi bila malipo kwa Boers. Je atafanikiwa? Atachukua nchi? Watamwacha salama? Kuna la kuigwa na upinzani wa kwetu hapa?

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…