Kuna suala la mfumo wa elimu. Hili tumeliongea ktk muktadha tofauti tofauti sana. Kwa ufupi nini kifanyike ktk suala la elimu?
Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Hili linahitaji jibu zito na refu sana, japo niseme tu: Pia naliandalia chapisho ambalo litatoka hivi karibuni.
Hili ni suala la kisera na kimfumo, nadhani tunahitaji kubadilika katika vyote.
Pia, ktk baadhi ya mada uligusia utengemano wa chama tawala na mifumo ya kiserikali hapa Tanzania.
Je kuna athari gani au faida gani iwapo chama kilichopo madarakani kitatolewa madatakani? Kwa mifumo hii ilivyo je jambo la kukitoa chama tawala hapa madarakani inawezekana? Atahari zake ?
Ukitenga Chama na Serikali kuna faida nyingi sana: Kwanza kabisa unajenga tabia ya uwajibikaji kwa viongozi ambao hutumia dola katika kuficha udhaifu wao wa kiuongozi. Pili, wananchi watajenga imani kubwa sana juu ya serikali yao. Tatu, tutakuwa tumehamia kwenye ngazi ya tatu kabisa ya kiungozi ambayo inategemea nguvu ya kitaasisi kuliko kuangalia watu binafsi.
Hili alilisema
Prof Max Weber kwamba nchi inapoacha na kutumia Charisma kwenye uongozi basi hulazimika kujenga taasisi imara amabzo zina mifumo inayoyabirika. Mifumo inayotabirika ndiyo hujenga imani kwa wananchi. Tunahitaji sana uongozi wa kitaasisi za kitaalamu na siyo taasisi vyama.
Hoja ya pili, je tukikitoa chama kuna athari zake ??: Ndiyo athari zake ni nyingi sana endapo utakuwa huna chama mbadala chenye nguvu na utayari wa kushika dola. Hili ndilo liliwasumbua sana Wafaransa baada ya mapinduzi ya mwaka 1789. Walimpinua mfalme lakini The Republicans/Jacobins mbali na kuimba nyimbo za :
"Liberty, Equality and Fratternity" hawakuwa na mkakati wa kuwawezesha kuongoza nchi. Kukawa na ombwe kubwa la kiuongozi. Sasa udikteta waliouchukia ndiyo ukazaliwa na
Napoleon Bonaparte akajichukulia nchi. Au mfano mwingine ni ule wa Libya, wamemtoa Gaddafi halafu hawana mbinu mbadala, hadi Obama alikiri hili.
Swali ni je: CCM ikitoka kuna chama mbadala ambacho kimejiandaa kiungozi kuweza kujaza nafasi ya viatu vya CCM ?? Ambacho kimejiandaa kabisa kuweza kuongoza jeshi la Tanzania, Polisi wa Tanzania, Usalama wa Taifa, Kushika hatama ya sera za mambo ya nje, Kushika hatamu ya Sera za elimu. Kuongoza nchi huhitaji tu kuwa na sera bali watu wenye uwezo wa kusimamia hizo sera. CCM walijipanga sana lakini kilichowaangusha ni michezo ya Rushwa, Udikteta wa kukanyaga haki za binadamu na Kugawana madaraka kwa upendeleo ambapo tumepata watawala wasio na uwezo wa kuongoza. Lakini mbali na udhaifu wao wote CCM wana Sera nzuri sana na viongozi wazuri sana: Japo hawawezi kusimamia sera zao na hao wenye akili hawapewi nafasi, Ujinga umeshika hatamu ndani ya chama.
Sasa kama kuna chama chenye hizo sifa mbadala basi, hata CCM ikitoka kesho nchi itaendelea tu bila kutikisika. Lakini kama hakuna chama mbadala, hata tukifanya mapinduzi na kuwatoa CCM tutakuwa kama Libya . Hivyo kama ukitaka kukitoa chama basi tafuta chama mbadala wake chenye uwezo kuliko chenyewe.
Displacement Theory.
Kuna suala linaloongelewa sana mitandaoni kuhusu Mbunge Tundu Lisu na kadhia nzima ya kushambuliwa kwa risasi. Wanasema ' Dunia inakanuni zake' unaliongeleaje hili? Nani anaseti hizi kanuni zinazo fanya kazi kama iliyofanywa kwa Lissu.
Pia naomba comment chochote kwa mahojiano anayofanya Lissu ktk vyombo vya habari vya kimataifa.
Hili limekaa kichama-chama sana na naomba nisiliongelee kabisa, maana hata nikiliongelea ni wachache sana ambao watanielewwa na kukubaliana na mimi. Japo kiufupi tu, kuna mihemko pande zote mbili.....