JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

Je Malcom Lumumba
• Shabiki wa mchezo upi?.
• Kama mpira ni timu gani pale EPL?.
• Siasa zako ni za mrengo upi?.
• Kwanini sio mpenzi wa masuala ya dini?, nini mtizamo wako kuhusu dini?.
• Were you a blacksheep in your family?, if not were you a role model to your peer?. if not then whats are your opinions regarding family raising!.
 
Siku hizi haupo kabisa, na ulikuwa ni utamaduni ambao tuliiga kutoka kwa waingereza tu. Siku hizi hata ukiingia chambers unakutaka na Jaji kavaa shati la Batiki na hana shida, mimi nilibaki nacheka sana tu. Japo nisema kabisa suala zima la Legal Practice sijahusika nalo kwa muda mrefu sana, mimi nahusika na Research na mambo mengineyo
Mzee baba kwa nn usitoa hata vitabu aise

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da Vinci hili swali naomba nisijibu leo, lakini mimi ni mkubwa japo siyo mbabu ni mchizi tu wa kitaa.
Ahaaa...
Hiyo siku nyingine itakua lini.. kalenda haina siku kama hiyo!!
Mkuu
Unazungumzia vipi sakata la stiglers Gorge (?) Na Wamarekani???
Nini hasa maoni yako

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Mkuu, hongera kwa majibu mujarab kwa maswali yanayoulizwa humu.

Kuna suala la mfumo wa elimu. Hili tumeliongea ktk muktadha tofauti tofauti sana. Kwa ufupi nini kifanyike ktk suala la elimu?

Pia, ktk baadhi ya mada uligusia utengemano wa chama tawala na mifumo ya kiserikali hapa Tanzania.

Je kuna athari gani au faida gani iwapo chama kilichopo madarakani kitatolewa madatakani? Kwa mifumo hii ilivyo je jambo la kukitoa chama tawala hapa madarakani inawezekana? Atahari zake ?

Kuna suala linaloongelewa sana mitandaoni kuhusu Mbunge Tundu Lisu na kadhia nzima ya kushambuliwa kwa risasi. Wanasema ' Dunia inakanuni zake' unaliongeleaje hili? Nani anaseti hizi kanuni zinazo fanya kazi kama iliyofanywa kwa Lissu.

Pia naomba comment chochote kwa mahojiano anayofanya Lissu ktk vyombo vya habari vya kimataifa.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Je Malcom Lumumba
• Shabiki wa mchezo upi?.
• Kama mpira ni timu gani pale EPL?.
• Siasa zako ni za mrengo upi?.
• Kwanini sio mpenzi wa masuala ya dini?, nini mtizamo wako kuhusu dini?.
• Were you a blacksheep in your family?, if not were you a role model to your peer?. if not then whats are your opinions regarding family raising!.
Shabiki wa mchezo upi na timu yangu: Nitakutag kwenye jukwaa la Sport halafu utajua Cousin.
Siasa zangu zangu: Mimi niko Conservative japo very pragmatic and Empirical (Open to new ideas)
Kuhusu dini: Kwangu dini ni kama siasa, japo naheshimu sana dini.

Black Sheep in the family: Ndiyo mzee, hadi mtaani, shule na chuoni.Sema walikuwa wanashindwa kunifukuza wakisema mimi ni very promising student, ilikuwa haupiti mwaka mzazi hajaitwa shule. Ngumi, Utoro, Ladies Man, you name it, nadhani ulikuwa ni utoto tu. Nakumbuka nilishawahi kuchoma msitu wa kijiji, kijiji kizima kikaja kuzima halafu mimi nikawa nimekula buyu tu nawacheki, hapo nakumbuka ni miaka 7. Chuoni nako hivyo hivyo, japo nikiri kabisa mbali na kuzingua sana nilikuwa naheshimu sana taaluma.

Role Model: Role model ndiyo mzee, japo nilianza kuwa role model sekondari na fujo zangu zote zikaanza kupungua. Baada ya kunipeleka shule ya mchanganyiko ndiyo nikawa mtulivu kabisa na fujo za chinichini. Simpy i was a teachers' pet na nikabadilikaga. Chuoni nilikuwa Al-Watan sana, wanafunzi wengi walikuwa wananikubali japo mimi ni mtu anayependa sana kulay low.

Kuhusu malezi: Nashauri wazazi wafanya sana kazi lakini wasisahau muda wa kukaa na watoto wao. Hili ndilo tatizo la kizazi hiki, tunakaa sana maofisini na tunawaachia wasichana wa kazi watoto. Hili lina madhara sanaaa na nimeshuhudia kwa macho yangu. Mtoto huwa anakua kila siku na kama hutakuwa unakaa naye basi vitu vingi sana kuhusu yeye vitakupita. Anapokuwa anapata mabadiliko ya kiakili, sasa mzazi usipokuwa naye karibu itakula kwako.

..
 
Ahaaa...
Hiyo siku nyingine itakua lini.. kalenda haina siku kama hiyo!!
Mkuu
Unazungumzia vipi sakata la stiglers Gorge (?) Na Wamarekani???
Nini hasa maoni yako

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Shida ya Wamarekani ni moja tu: Ndani ya miaka mingi imekuwa ni nchi ambayo inaihujumu Tanzania hivyo hata kama leo inakuwa na nia njema sidhani kama Tanzania itakubali kuwasikiliza na kuupokea huo ushauri vizuri. Walileta ushauri kuhusu Structural Adjustment Program na wakavuruga nchi, hadi Nyerere akawauliza wazi wazi: Mimi mlinikosoa, ninyi mefanya nini ??

Upande wa pili sasa, Marekani atakuwa na Moral Position ya kutambia sisi tuache kuharibu mazingira pale tu ambapo yeye atakubali kwamba anachangia sana katika kuvuruga hali ya hewa ya dunia na pale atakapokubali kwamba dunia inakumbwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Kama hakuna mabadiliko ya hali hewa kama asemavyo Donal Trump, basi hata Stiegler's gorge nako hakutakuwa na madhara yoyote.

Wataalamu wa Marekani wamesema dunia haina Global Warming, je tutawaaminije kwenye hili la Stiegler's gorge ???

NB: Yote tisa, hata kama Tanzania haiwapendi wamarekani hili halizuii sisi kufanya utafiti wetu wa kitaalamu juu ya hilo lisemwalo.
Kama litakuwa na madhara basi tutafute njia mbadala, lakini kama kuna uwezekano nashauri wajenge tu.
 
Mchizi wa kitaa kwanini siku izi huleti nondo kama alizokuanazo THE EMPEROR??
Upo kwenye ndoa mwaka wa ngapii? ?

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Kipindi kile nilikuwa nina muda sana wa kuandika, hivyo nilituma sana mabandiko.
Siku hizi naamka saa 11 na kulala saa 7 au 6, inaniwia vigumu saa kuandika mada mpya.
 
Kipindi kile nilikuwa nina muda sana wa kuandika, hivyo nilituma sana mabandiko.
Siku hizi naamka saa 11 na kulala saa 7 au 6, inaniwia vigumu saa kuandika mada mpya.
Nadhani hili linachangia mno.. ila Ahsante kwa mada zako zenye madini adimu!!
Je ushauri kwa vijana 20-26yrs wako ni upi.. kijamii, kiuchumi na kisiasa

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Shida ya Wamarekani ni moja tu: Ndani ya miaka mingi imekuwa ni nchi ambayo inaihujumu Tanzania hivyo hata kama leo inakuwa na nia njema sidhani kama Tanzania itakubali kuwasikiliza na kuupokea huo ushauri vizuri. Walileta ushauri kuhusu Structural Adjustment Program na wakavuruga nchi, hadi Nyerere akawauliza wazi wazi: Mimi mlinikosoa, ninyi mefanya nini ??

Upande wa pili sasa, Marekani atakuwa na Moral Position ya kutambia sisi tuache kuharibu mazingira pale tu ambapo yeye atakubali kwamba anachangia sana katika kuvuruga hali ya hewa ya dunia na pale atakapokubali kwamba dunia inakumbwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Kama hakuna mabadiliko ya hali hewa kama asemavyo Donal Trump, basi hata Stiegler's gorge nako hakutakuwa na madhara yoyote.

Wataalamu wa Marekani wamesema dunia haina Global Warming, je tutawaaminije kwenye hili la Stiegler's gorge ???

NB: Yote tisa, hata kama Tanzania haiwapendi wamarekani hili halizuii sisi kufanya utafiti wetu wa kitaalamu juu ya hilo lisemwalo.
Kama litakuwa na madhara basi tutafute njia mbadala, lakini kama kuna uwezekano nashauri wajenge tu.
Honestly inaniuma sana.. Nayasikia maumivu na machungu aliyonayo Rais juu ya hilii. Asee ni wakati wa kushikamana kizalendo. Hii ni nchi yetu.
Tumuweke rais kwenye maombi yetu ya kila siku na Tanzania kwa ujumla.
Anapitia wakati mgumu sana. Hekina na ujasiri wahitajika

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom