JF imekusaidia nini tangu uijue?

Kabisaaa sasa hv asilimia kubwa wengi ni wakolofi zaman ukiuliza kitu, utasaidiwa mpaka unapewa connection lakin sasa hv ukipewa connection ujue umeibiwa hahaha
 
Tunaomba JF ituanzishie mini forum ya Boys Boys na Ladies Ladies
Nina maana yangu mniulize
Na kweli ila wazamiaji hawatakosekana tu, maana kwenye magroup ya akina mama na akina baba pia wamo so mambo yamebadilika sna mkuu
 
Hapana, Mshana Jr is a good bro hajawahi nisimanga popote.! Wapo tu, wana majibu yao makavuuu.!![SUB] 😀 [/SUB]

Wewe pia uliwahi nishauri pahala last year, na kipindi ulipotea nilikukosa sana.!!
 
JF imenifunza mengi Sana, Ila pamoja na yote ule Uzi wetu pendwa wa "wazee wakuweka mzigo"umenifanya kuwa mtu katika watu. Namshukuru Sana alieanzisha ule Uzi japo ndio hivyo tena kanuni mpya za mtandaoni zimetuzulumu haki yetu.
 
Hapana, Mshana Jr is a good bro hajawahi nisimanga popote.! Wapo tu, wana majibu yao makavuuu.!![SUB] 😀 [/SUB]

Wewe pia uliwahi nishauri pahala last year, na kipindi ulipotea nilikukosa sana.!!
[emoji1752][emoji1548][emoji1534][emoji1545][emoji1545] BAK nimeshasafishwa huku[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ukiwa na jambo hulielew vizuri ujileta jamii forum unapata msaada mzuri wa kifikra na u atatua tatizo . Watu wengine hatu comment sana ila tunasoma sana yanayoandikwa . Kuna ma elfu ambao hawajajiunga na wanasoma vinavyoandikwa humu
 
Mimi huniondoa upweke na kunipa elimu,vituko na vitu nisivyoweza kuongea na jamii inayonizunguka maana kuna watu wanajifanya wako Makini na ustaarabu utadhani hawaogi uchi wanaoga na makoti ya mvua au wanavua chupi wakati wa kujamba
 
Imenisaidia mengi,Ila kikubwa ilinisaidia sana,
Wakati ambao nilihitaji watu kuliko kitu chochote.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuwashirikisha ninachopitia.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kunisikiliza (kunisoma).
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuelewa ninachopitia.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kunifariji.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuniambia hili litapita.
Hamna namna ambayo naweza kuelezea ikaleta maana.

Huu ulikuwa ni wakati mgumu sana, na ni wakati ambao umenifanya nione members wa huku ni watu wazuri, hata kama tutapishana kwenye mambo tofauti lakini wana utu na vitu vizuri sana ndani yao, mengine ni udhaifu wa kibinadamu.
 
Nadhani hii inahusu wakati ule unamuuguza mama aliyekuwa akisumbuliwa na cancer, kama sikosei, hadi kufariki kwake. Nakumbuka kuusoma ule uzi hapa jamvini.

 
1.nimepata marafiki
2.nimebadilika baadhi ya tabia mfano siingii Instagram,naingia JF na podcast
3.napata stori mbalimbali za kufurahisha almaarufu kama “chai”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…