JF imekusaidia nini tangu uijue?

JF imekusaidia nini tangu uijue?

JF ni Jamii Forum. Ni Jukwaa la Jamii.

Mada za siasa, uchumi, kijamii na kisayansi zimenijenga kifikra.

Jamii Forum ni kisima Cha fikra. Imenijenga kifikra na kimawazo.

Nimeifahamu Jamii Forum mwaka 2010 wakati ninakaribia kujiunga chuo, na ni wakati ule siasa zimepamba moto JK anatafuta muhula wa pili.

Kimsingi, purukushani za kisiasa za akina Makamba Yusuf, Nappe na wengineo walinifanya kutafuta maarifa zaidi na niliyapata Jamii Forum maana katika mijadala ile, hao wanasiasa waliihusisha Jamii Forum kwamba Kuna watu wanatoa Siri za chama JamiiForum, kwa hiyo pia nikawa na kiu kujua Jamii Forum Ni kitu gani.

Humu nilikutana na watu wenye weledi kifikra Kama vile Kiranga, king kong, miss chaga, @lara1, The bold, Nifah, Everlyn salt, Kongosho, Ben Saanane (RIP), @nappe nnauye, Mshana Jr ASHA dii na wengineo ambao walichambua mambo kwa kina na kuifanya Jamii Forum iheshimike hapa Tanzania na hata nje ya mipaka.

Pongezi kwenu @jamiiforum, Mhariri, na haswa Mello, M kwa kazi nzuri ya kukutanisha Watanzania katika jukwaa moja la mijadala huru.

Kazi kubwa iliyopo Sasa ni kuilinda heshima ya Jamii Forum japo irudi ilipokuwa mwaka 2013 maana humu wachangiaji wenye ueledi na staha wanapungua sana.
Kabisaaa sasa hv asilimia kubwa wengi ni wakolofi zaman ukiuliza kitu, utasaidiwa mpaka unapewa connection lakin sasa hv ukipewa connection ujue umeibiwa hahaha
 
Bila shaka ni Mshana Jr na Mshana Jr 2
😜😜😜 mie JF ni shule pia nimepata marafiki wengi sana humu wengine tulisoma pamoja shule mbali mbali.

Kuna watu humu wana shule kubwa sana lakini humu huwezi kuwagundua hadi upate bahati ya kufahamiana nao kwa karibu.
Hapana, Mshana Jr is a good bro hajawahi nisimanga popote.! Wapo tu, wana majibu yao makavuuu.!![SUB] 😀 [/SUB]

Wewe pia uliwahi nishauri pahala last year, na kipindi ulipotea nilikukosa sana.!!
 
JF imenifunza mengi Sana, Ila pamoja na yote ule Uzi wetu pendwa wa "wazee wakuweka mzigo"umenifanya kuwa mtu katika watu. Namshukuru Sana alieanzisha ule Uzi japo ndio hivyo tena kanuni mpya za mtandaoni zimetuzulumu haki yetu.
 
Hapana, Mshana Jr is a good bro hajawahi nisimanga popote.! Wapo tu, wana majibu yao makavuuu.!![SUB] 😀 [/SUB]

Wewe pia uliwahi nishauri pahala last year, na kipindi ulipotea nilikukosa sana.!!
[emoji1752][emoji1548][emoji1534][emoji1545][emoji1545] BAK nimeshasafishwa huku[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Ukiwa na jambo hulielew vizuri ujileta jamii forum unapata msaada mzuri wa kifikra na u atatua tatizo . Watu wengine hatu comment sana ila tunasoma sana yanayoandikwa . Kuna ma elfu ambao hawajajiunga na wanasoma vinavyoandikwa humu
 
Mimi huniondoa upweke na kunipa elimu,vituko na vitu nisivyoweza kuongea na jamii inayonizunguka maana kuna watu wanajifanya wako Makini na ustaarabu utadhani hawaogi uchi wanaoga na makoti ya mvua au wanavua chupi wakati wa kujamba
 
Imenisaidia mengi,Ila kikubwa ilinisaidia sana,
Wakati ambao nilihitaji watu kuliko kitu chochote.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuwashirikisha ninachopitia.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kunisikiliza (kunisoma).
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuelewa ninachopitia.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kunifariji.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuniambia hili litapita.
Hamna namna ambayo naweza kuelezea ikaleta maana.

Huu ulikuwa ni wakati mgumu sana, na ni wakati ambao umenifanya nione members wa huku ni watu wazuri, hata kama tutapishana kwenye mambo tofauti lakini wana utu na vitu vizuri sana ndani yao, mengine ni udhaifu wa kibinadamu.
 
Nadhani hii inahusu wakati ule unamuuguza mama aliyekuwa akisumbuliwa na cancer, kama sikosei, hadi kufariki kwake. Nakumbuka kuusoma ule uzi hapa jamvini.

Imenisaidia mengi,Ila kikubwa ilinisaidia sana,
Wakati ambao nilihitaji watu kuliko kitu chochote.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuwashirikisha ninachopitia.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kunisikiliza (kunisoma).
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuelewa ninachopitia.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kunifariji.
Wakati ambao nilihitaji watu wa kuniambia hili litapita.
Hamna namna ambayo naweza kuelezea ikaleta maana.

Huu ulikuwa ni wakati mgumu sana, na ni wakati ambao umenifanya nione members wa huku ni watu wazuri, hata kama tutapishana kwenye mambo tofauti lakini wana utu na vitu vizuri sana ndani yao, mengine ni udhaifu wa kibinadamu.
 
1.nimepata marafiki
2.nimebadilika baadhi ya tabia mfano siingii Instagram,naingia JF na podcast
3.napata stori mbalimbali za kufurahisha almaarufu kama “chai”
 
Back
Top Bottom