JF Karibuni Tanzania Professionals Network


Kuhani Mkuu . . . . LOL naanza sasa kuelewa kwa nini unatumia jina la Kuhani . . . usijali tutaelewana tu. Kama nia yako ya kweli ni kuelewa basi utaelewa tu wala usitie shaka, ila kama nia yako ni tofauti, huenda nikashindwa kukusaidia. Sitaki kuhisi Matejoo, au Tumaini au Onyango Radical amreduri kwa staili ya Kuhani . . . LOL. Ngoja nijitahidi tena kufafanua Mzalendo . . .

Kwanza hakuna mahali ambapo Katiba inazungumzia juu ya Mwanachama mwenye Madigrii. Kama utarejea inazungumzia Graduates wa Higher Learning Institutions ambaye si lazima awe na Degree. Napenda kuamini unafahamu katika vyuo vya elimu ya juu wahitimu wanatunukiwa nini. Kwa Mtazamo wangu Graduate si lazima awe na Degree. Graduate ni mtu ambaye amehitimu na kugraduate anaweza kuwa na Stashahada, Stashahada ya Juu, Degee ya Kwanza, ya pili au hata Degree ya Falfasa. Katika kundi hili Mwanachama anayequalify inatakiwa awe na POSITIVE ATTITUDE. Naasume unaelewa kuwa unapokuwa na Positive Attitude ina maana gani. Kwahiyo sharti hilo ni muhimu na ndiyo maana Executive Committee imepewa jukumu na kukubali maombi pale inapoona una muelekeo wa kimaendeleo. Si Graduates wote wenye mtazamo wa kimaendeleo kwa vitendo na mawazo.

"Kama hawezi kujiunga basi Katiba yenu inaipiku ile sheria mbovu kuliko zote duniani inayosema Rais wa Tanzania asilipe kodi." Hili sijalielewa vema, ukipenda unaweza ukalifafanua kama unamwelekeo . . . LOL

Kama umeangalia vizuri katiba kuna sharti moja ambalo ni common sehemu zote nalo ni . . . who are interested in furthering the work of the Organization . katika 3.1.2 . . . . which is interested in furthering the Organization's work . Katika 3.1.3 . . .which supports the Vision, Mission and Objectives of Tanzania Professionals Network.

Kwa hiyo kuna sharti ambalo ni common katika category zote tatu za membership.

Juu ya incorporated body . . . nadhani hii ni lugha ya kisheria. Hivi ni vikundi au tasisi vinavyotambulika kwa maana ya kujiorganize na kuwa na mfumo wa kukiendesha kama katiba lakini ambavyo havijaandikishwa kisheria kwa maana ya kupata usajili.

Kuhani unakaribishwa kwa maoni au maswali yako zaidi au hata kutoa mapendekezo mbadala ya kuboresha kama unayo na ungependa kuyatoa.
 

Steve D asante sana Mzalendo . . . nikiangalia quote yako ya Fikra ni kitu kizuri, uzushi unatokana na fikra, fikra za uzushi ni kitu kibaya na ni uzushi, kutotenganisha uzushi na fikra ni kitu kibaya zaidi kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SDD6-07. napata matumaini jinsi attitude yako ilivyo. Pia hoja zako nimezikubali.

Karibu Steve D. Mapungufu tutayafanyia kazi mwezi wa nane wakati wa AGM. Jisikie huru kuwasiliana.
 
Well Spoken Sanctus, and thanks again for your invitation, in some sense umedemonstrate some sound leadership skills za kuhakikisha unazama na chombo chako, Congratulations! Count me in!

Asante sana GM . . . ni matumaini ya TPN na uongozi wake kuwa kama falfasa yako inavyosema . . "We are what we repeatedly do. Excellence, therefore is not an act but a habit" Inatupasa kulifanyia kazi hilo ili kuifanya TPN iwe na Excellence.

Nashukuru kwa michango yako yote.
 

Nashukuru sana Mzalendo Kichuguu kwa maneno yako ya kutia moyo, hakika nimefarijika pia na michango yako binafsi na wengine wengi hapa JF bila shaka yote itafanyiwa kazi.

Ni matumaini yetu kwamba TPN iundwe katika misingi ya umakini wa hali ya juu na ziadi ya hayo ni vizuri pia kuwa tayari ku accomodate mawazo yote as long as yana muelekeo wa kuboresha.

Asante sana na nikuombe tu, tuendelee kuwasiliana kama utakuwa na mawazo zaidi.
 

Sanctus,

No Problem Sir! Anytime.
 

washomire watajulikana vipi
 
Kwa hiyo kuna sharti ambalo ni common katika category zote tatu za membership.

Na hapo ndio kuna tatizo.

Hili sharti, kuafiki au kusapoti malengo ya chama, ni lazima ulitimize kwa vyovyote vile. Na, ukilishalitimiza, huhitaji mengine. Hapo ndipo it gets funny!

Kwa hiyo, yale masharti mengine mawili - shahada au stashahada na kuwa shirika na shirikisho - ni masharti moot! Moot kwa maana kwamba, qualification moja ambayo ni lazima uwe nayo kwa vyovyote vile, inafuta, ina obviate the need to meet any other qualification. Any requirement which is mandatory but at the same time a sufficient requirement, becomes the only requirement. Clauses 3.1.1 and 3.1.2 are therefore moot! It would not make a difference if they were not there. But by being there they make the constitution look silly!

Katiba yenu haijakaa kama ina "sound mind" kama mnavyowataka wengine kabla ya kutoa boriti jichoni mwenu kwanza!
 
Sanctus Umelala saa ngapi maana unakabiliana na hizi nondo hatua kwa hatua toka jana na bado naona upo...

Kwa hakika ujumbe utafika. Kiongozi wa Kweli. Keep it up brother.
 

Ndugu yangu Kuhani, naomba nikubali pengine kuna tatizo la kuweza kuelewana hapa. Pengine sukuelewi vema au hunielewi vema. Kama uko sawa unaweza kunipa namba yako ya simu, nikakupigia ili tuongee maana wakati mwingine kuelewana katika maandishi inaweza kuwa vigumu.

Mimi nadhani ni vema wakati mwingine badala ya kuwa na jazba na kutoa kashfa, ni vizuri ukiwa na maoni mbadala kama walivyofanya wengine. It will save your energy.

Kama ni suala la kufanya analysis ningesema kuwa sharti la kuwa Professional (ambaye amehitimu higher education au yule ambaye amejifunza kwa njia yoyote nyingine na kuwa na hiyo taaluma) pamoja na kuunga mkono objectives za TPN ni masharti muhimu.

Kwa sasa ni-assume kuwa utanitumia maoni yako mbadala nikitarajia kuwa walau una mwanga wa kile tunachokusudia. Kama huwezi kutuma maoni bado tunaweza kuwasiliana kwa njia mbadala, kama hilo pia haliwezekani, basi wacha nikubali yaishe . . . . LOL. Ni vizuri kukubaliana pia kuwa mmeshindwa kuelewana inapobidi. Inawezekani sijakuelewa au inawezekana hujanielewa.
 
Sanctus Umelala saa ngapi maana unakabiliana na hizi nondo hatua kwa hatua toka jana na bado naona upo...

Kwa hakika ujumbe utafika. Kiongozi wa Kweli. Keep it up brother.

Asante sana Mzozo . . . . Sina uhakika nililala saa ngapi, lakini nadhani ni baada ya saa nane na nusu usiku . . . LOL wakulu bado hawajanitoa kwenye Tanuru la moto . . . LOL

Najitahidi kuzingatia na kuelewa yote yaliyo muhimu. Nashukuru tena kwa mchango wako pia.
 

Jamani hivi JF ni anti ccm tu? hili niswali ambalo naona niulize humu ndani. maana sielewi ccm imeingiaje hapa ktk tpn?
ina maana akifanya mbowe ufisadi haandikwi huku? mi naona humu tunachukia mabmbo maovu from what ever source ccm and the like. mnatutisha sisi tulio neutral na tunakaataa maovu yote sio nusu nusu je hatustahili?
msifanye huu ukawa mtandao wa upinzani naamini hata nia ya waanzishaji haikua hivyo. MODERATORS PLEASE HELP KAMA NIMEKOSEA HAPA.
Afterall kujiunga ni hiyari ameomba utembelee website uwasome ukikubaliana sawa au la basi . na hakika ww hata ujatake time kwenda huko ila basi tuu tunatumia uhuru wetu vibaya.
 
Sanctus Mtsimbe,

You are the man. Baada ya kusoma post yako na majibu yako kwa hoja mbalimbali nashawishika kuamini kwamba upo makini katika kutekeleza malengo na ndoto za TPN. Hongera sana, mimi nakuunga mkono 100%. Kila hatua ya kutusogeza mbele na kulitoa taifa letu katika aibu tuliyo nayo inapaswa kuungwa mkono sana.
 

Hapo juu nadhani amejaribu kuitaja CCM pekee kutokana na kwamba ndio Chama Tawala na ndio Chama ambacho kimeshika Mpini na sisi tumeshika Makali. Sasa ukijaribu kufikiria utagundua kwamba aliyeshika mpini ndio yupo katika advantage kwa lolote.

Vyombo vyote vya kiserikali kuanzia Usalama wa Taifa vipo chini ya Serikali, ambayo ni Serikali ya CCM kwa hiyo hapa vyama vingine vya Upinzani haviasemwa kwa kuwa sidhani kama vinaweza kuwa an nguvu ya kuwadhibiti wale ambao watakuwa wameenda nyuma ya matakwa yao kama nguvu ambayo CCM inayo. misuko suko iliyotokea nyuma hapa JF inadhibitisha hilo.

Mbowe, Slaa, Lyatonga na wengine nao wakifanya ufisadi sidhani kama tutawaacha. JF sio mtandao wa Upinzani bali ni mtandao wa kupinga yale yote ambayo yanafanywa kuwaumiza Watanzania wa Kawaida kama mimi na wewe. Mtandao wa Watanzania wenye uchungu na Tanzania.

JF: WHERE WE DARE TO TALK OPENLY!!!
 


Sure, but we should not go that route blindly bila kuhoji. Nimefuatilia huu mjadala nikitegemea ningepata kuelewa what TPN is all about. Huenda nikaanza kuamini kuwa hawa TPN ni wasanii.

Mzee Mkumbo nilitegemea ungesema mawili matatu kuhusu mjadala huu?




.
 


washomire watajulikana vipi


Kuna watu natambua uwepo wao kwenye online community. Ila mnapokuwa wakimya, napata picha kwamba you guys know something we don't; but why the secrecy? Sanctus Mtsimbe is being so diplomatic on his responses. Nikisema TNP wasanii nitakuwa nimekosea? I'm outta here! 😡


"wakimya" - nikiwa na maana when someone say something but avoid to speak about what you expected her to say on the matter.



.
 

Kitila Na Mwana Msimbe!!

Nilichojifunza Humu Jamvini Ni Kwamba, Usipokua Makini... Unawez Kukosa Usingizi!!

Tpn Ni Nzuri Na Kama Haukidhi Kuwa Member Ni Bora Kuacha Walengwa Wa Tangazo, Nina Wasiwasi Na Baadhi Ya Walio-negative... Hawakubali Kwamba They Dont Fit In Every Network

Keep It Up BWANA Msimbe, Na Wapinzani Wa Tpn Kalaga Baho!!!!!!!!
 
Last edited:


Ndo maana hatupendelei watu kutumia majina yao halisi humu jamvini. Ukiwa rafiki na mtu na unajua anatumia jina gani JF mara nyingi kabla ya kuhoji chochote asemacho utasita kufanya hivyo, wakati ambavyo kutojua mtoa hoja ni nani pengine ungeshiriki kikamilifu.




.
 
The confirmation process continues, Senator Kuhani exhaustively expounges extreme extrapolations, as expected. Details aside, president Mtsimbe exhibits a rare flare of tenacious "toe-to toeing" and tenets of tough-cookieness without as Mwanakijiji put it "snapping" or getting condescending and cocky.

Whether this hue of humility will hang to heights or go to the hang heights remains to be seen.

With reservation, I will cut him and his organization some slack, short of joining at least during the vetting period due to privacy concerns.

Just as there is no trade of between having a phone with a sizable screen and having a small phone (challenge to engineers) there is also no trade off between joining an effective real world organization and anonimity.
 

It is unfortunate that some of us are reduced to labelling the few detail oriented (or pedantic, depending on your viewpoint) souls in here as "walio negative" and "wapinzani wa TPN"

The good president himself invited critical analysis in the hope that it will help check and even iron out a few things. If some senators are asking one too many questions, it is not because they love TPN and it's ideals less, it is because they love efficiency, transparency and accountability more and hope to have these to the maximum at TPN.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…