Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
- Thread starter
- #101
Mtu ambae yuko kundi la kwanza, la digrii, ambae haafiki malengo ya chama, anaweza kuwa member kwa mujibu wa katiba? Kama anaweza basi nyinyi mtakuwa hamna "sound mind" mnayoitaka kwa wengine.
Kama hawezi kujiunga basi Katiba yenu inaipiku ile sheria mbovu kuliko zote duniani inayosema Rais wa Tanzania asilipe kodi.
Let X = sharti la kuhitimu madigrii.
Let Y = sharti la kuwa shirika au chombo kingine, "unincoporated body."
Let L = sharti la kuafiki Lengo la chama.
Wanachama wa Kundi la kwanza: Sharti X, na sharti L
Wanachama wa Kundi la pili: Sharti Y, na shart L
Wanachama wa Kundi la tatu: Sharti L.
Kwa hiyo, huwezi kuingia kama hujatimizia L. Sawa?
Na ukishatimiza L, huhitaji X na Y tena!
Kwa hiyo X na Y hazihitajiki! Clause 3.1.1 na 3.1.2 zinauawa na Clause 3.1.3
Hapo mnachekesha.
Unless, unless, ukitimiza sharti la madigrii, basi sio lazima uafiki malengo ya chamaaa haa haaaa a haaaaaaa!
This is hilarious! Endrew Chenge couldn't write such legal comedy.
Swali la nyongeza: Je, "unincorparted body" mtakayo ruhusu inaweza kuwa kama nini, kundi la mtaa wa pili la wacheza ngoma ambao hawako organized kwa saaana?
Anza upya.
Tena!
Kuhani Mkuu . . . . LOL naanza sasa kuelewa kwa nini unatumia jina la Kuhani . . . usijali tutaelewana tu. Kama nia yako ya kweli ni kuelewa basi utaelewa tu wala usitie shaka, ila kama nia yako ni tofauti, huenda nikashindwa kukusaidia. Sitaki kuhisi Matejoo, au Tumaini au Onyango Radical amreduri kwa staili ya Kuhani . . . LOL. Ngoja nijitahidi tena kufafanua Mzalendo . . .
Kwanza hakuna mahali ambapo Katiba inazungumzia juu ya Mwanachama mwenye Madigrii. Kama utarejea inazungumzia Graduates wa Higher Learning Institutions ambaye si lazima awe na Degree. Napenda kuamini unafahamu katika vyuo vya elimu ya juu wahitimu wanatunukiwa nini. Kwa Mtazamo wangu Graduate si lazima awe na Degree. Graduate ni mtu ambaye amehitimu na kugraduate anaweza kuwa na Stashahada, Stashahada ya Juu, Degee ya Kwanza, ya pili au hata Degree ya Falfasa. Katika kundi hili Mwanachama anayequalify inatakiwa awe na POSITIVE ATTITUDE. Naasume unaelewa kuwa unapokuwa na Positive Attitude ina maana gani. Kwahiyo sharti hilo ni muhimu na ndiyo maana Executive Committee imepewa jukumu na kukubali maombi pale inapoona una muelekeo wa kimaendeleo. Si Graduates wote wenye mtazamo wa kimaendeleo kwa vitendo na mawazo.
"Kama hawezi kujiunga basi Katiba yenu inaipiku ile sheria mbovu kuliko zote duniani inayosema Rais wa Tanzania asilipe kodi." Hili sijalielewa vema, ukipenda unaweza ukalifafanua kama unamwelekeo . . . LOL
Kama umeangalia vizuri katiba kuna sharti moja ambalo ni common sehemu zote nalo ni . . . who are interested in furthering the work of the Organization . katika 3.1.2 . . . . which is interested in furthering the Organization's work . Katika 3.1.3 . . .which supports the Vision, Mission and Objectives of Tanzania Professionals Network.
Kwa hiyo kuna sharti ambalo ni common katika category zote tatu za membership.
Juu ya incorporated body . . . nadhani hii ni lugha ya kisheria. Hivi ni vikundi au tasisi vinavyotambulika kwa maana ya kujiorganize na kuwa na mfumo wa kukiendesha kama katiba lakini ambavyo havijaandikishwa kisheria kwa maana ya kupata usajili.
Kuhani unakaribishwa kwa maoni au maswali yako zaidi au hata kutoa mapendekezo mbadala ya kuboresha kama unayo na ungependa kuyatoa.