JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Ndio maana elimu ya kileo haina msaada mkubwa kwa watoto
Kabisa mkuu. Miaka yetu mnapo maliza elimu ya msingi mnaambiwa katika nyimbo na risala kua mnaenda "kujitegemea"(wachache ndio walikua wakiendelea na elimu ya sekondari)

Kilimo cha mbogamboga majumbani ilikua ni kilimo cha watoto. Saa zingine mnashindana kua na bustani. Tena hata bustani za maua ilikua ni shughuli za watoto na tukishindana kuonyesha ya nani zaidi😀😀😀
 
Kabisa mkuu. Miaka yetu mnapo maliza elimu ya msingi mnaambiwa katika nyimbo na risala kua mnaenda "kujitegemea"(wachache ndio walikua wakiendelea na elimu ya sekondari)

Kilimo cha mbogamboga majumbani ilikua ni kilimo cha watoto. Saa zingine mnashindana kua na bustani. Tena hata bustani za maua ilikua ni shughuli za watoto na tukishindana kuonyesha ya nani zaidi[emoji3][emoji3][emoji3]

Aisee hii ni kweli kabisa!
 
RIP Nicco Ye Mbajo

Tasnia ya Bongokomiki imepata pigo baada ya mmoja kati ya wachoraji wakongwe nchini Mzee Nicco Ye Mbajo kufariki dunia. Mzee Mbajo amefariki dunia usiku Jumamosi kuamkia Jumapili ya juzi jijini Dar es salaam.

Jina la Nicco Ye Mbajo linaweza kuwa geni kwa baadhi ya wapenzi wa Fasihi kutokana na kuwa kimya kwa kipindi kirefu kidogo lakini kazi za ubunifu wake hazijawahi kuacha kujulikana na mpenzi yeyote wa majarida ya kiswahili nchini.

Sidhani leo kama yupo Mtanzania yeyote mpenzi wa kusoma majarida ya Kiswahili nchini asiyelijua Jarida la SANI ambalo nathubutu kusema ndiye Baba wa Majarida yote ya burudani na vikaragosi nchini tangu mwanzoni mwa miaka ya 80.

Jina la SANI lilikuwa ubunifu wa muunganiko wa kifupi cha majina mawili ya mwanzo ya waasisi wa Jarida hilo ambao ni marehemu Saidi Bawji na Nicco Ye Mbajo, yaani SA (Saidi) na NI (Nicco). Marehemu Nicco ye Mbajo ndiye alikuwa mchoraji wa kwanza kabisa wa SANI.
Amezikwa Jana tarehe 27/11/2021 makaburi ya kinyerezi, bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.View attachment 2015154View attachment 2015155
Nilipata kukaa na kuongea kuhusu mambo mbali mbali na Marehemu Mzee said Bawji pale nyumbani kwake Kwanjeka Tanga katika kipindi cha mwishoni mwa Uhai wake.

Watoto wake wapo pale Tanga.

Allah awasamehe marehemu zetu hawa.
 
FB_IMG_1637640163415.jpg
 
Back
Top Bottom